Gazeti la Mwananchi kuna mchawi kaingia........ litakufa muda si mrefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la Mwananchi kuna mchawi kaingia........ litakufa muda si mrefu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, May 4, 2011.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa siku za hivi karibuni nimeanza kuona tofauti katika utoaji wa habari wa gazeti la mwananchi (MCL) na nina wasi wasi kwamba kuna mchawi kaingia hapo ili kuli sambaratisha.

  Habari ya kwanza iliyotiliwa shaka ni ile ya kutowataja kwa majina mafisadi wapya ambao walitajwa hadharani na Dr Slaa. Habari ya pili kwa mimi binafsi ni hii ya Osama kuuawa, karibu vyombo vyote vya habari duniani vinaandika kile kilichotokea lakini Mwananchi linaandika eti Osama yupo hai........ nahisi kifo cha gazeti hili kimafika.
   
 2. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wamenunuliwa na mafisadi
   
 3. c

  chante Senior Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ndugu magezi,
  moja ya ethics za proffesional journalism ni ku CROSS CHECK, yaani km ilvyotajwa ile list,wale watuhumiwa wangetafutwa,wangejuzwa kuhusu yalosemwa(km hawakuckia) then wangetolea maelezo hzo kashfa..hapo mwandshi acngeonekana anaegemea upande gani..yaani katenda haki kwa pande zote mbili na angejitofautsha na makanjanja..! hii haitofautiana sn na natural justice ktk sheria,! Kuhusu kifo cha osama,hata ww naamini una querries ktk hlo,!na2mai ulfuatilia vzuri jnc member wa jf walvozchambua picha znazosemekana ndo za maiti ya OBL..,you dont have to be a rocket scientist kujua kama zilpikwa! then wangetoa vdeo ya mazshi yake yanayosemekana yalfanyka baharin & na DNA proof ingekuwa basis kubwa ya kuamini km ndo yeye!ila naamini soon julian assange atatuambia ni nani hasa aliekufa!coz naskia cable za US embasy in pakstan zmesha LEAK!
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Kwenye suala la habari za kisiasa hasa za hapa nyumbani, sasa hivi mwananachi wanachakachua kwa kwenda mbele.

  Inawezekana mapacha watatu wamewatembelea wahariri maana mwananchi limekuwa ni gazeti linaloaminiwa na kusomwa na watu wengi kwahiyo sio ajabu kila mwenye mkakati akaufanya kupitia mwananchi.

  Kwa suala la osama hata mimi bado siamini kama kweli wamarekani walimuua kama kweli amekufa.

  Mazingira, picha na maelezo yanayotolewa bado yana utata mkubwa na yanazua maswali mengi mno kuliko majibu.
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,139
  Trophy Points: 280
  Hujawaelewa mwananchi ktk hili la osama, ukurasa wa mbele wameandaki kuuwawa kwa Osama na kuweka makazi yake ya awali lakini kumbuka Al Qaeda wamekanusha kuhusu kuuwawa kwa Osama na ndicho ambacho mwananchi wamekiandika ktk kurasa za ndani.

  Hawajapendelea isipokuwa wameandika habari ambazo zimepatikana, kuuawa kwa osama ni habari moja kutoka Marekani na kutokuuwawa kwa Osama ni habari nyingine kutoka Al Qaeda.

  Inawezekana hukulielewa hili, hilo la kutaja mafisadi na mimi nilishangaa kutoona list of shame
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mafisadi at work!!
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Lakini vipi kwa upande wa Al Qaeda kusema OBL yu mzima wa afya bila ya wao kuonyesha uzima wake? Any way tusubiri kwani kwenye dunia ya leo huwezi kuficha kila kitu pamoja na imani za vijiweni. Hata Sadam Hussein ilikuwa hivyo hivyo!
   
 8. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Gazeti hilo ni la Kenya, pamoja na The Citizen, yanamilikiwa na kampuni ya Nation Media, ya watu wa Kibaki, Tanganyika ni Shamba la Bibi, kazi yao kelele tu, kwa Nchi ya Zanzibar na nchi Kenya ya kenya wachukua vyao Tanganyika itabaki na Manzese tu
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Haliko strong tena kama miezi kadhaa nyuma.Limeshavamiwa na mafisadi.
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Limechuja sana sasa hivi hawana zile habari za investigative journalism wananchi wengi tulilitegemea sana lakini sasa wako hoi bin taabani
   
 11. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  WE vipi mwana yaani unataka uone habari zinazokufurahisha tu. hahaha
   
 12. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Samahani kama nitakuwa nimekosea, kuna makala nilishawahi kuisoma mahali kuwa Mwananchi Communications Ltd ni sehemu ya The Aga Khan Foundation... Hili la kuwa ya Wakenya ndio kwanza nalisikia kwako.
   
 13. moblaze

  moblaze JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ngugu, umeamka kweli?
   
 14. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni kweli, limeanza kufuata mwelekeo wa Majira jinsi lilivyoanza kuchuja.
  Wanatakiwa kurudi na kujichunguza nini kimetokea miongoni mwao.

  Hata ukiifuatilia ile habari ya juzi kuwa kuna mgogoro ndani ya CDM na kwamba makundi ya Mbowe na Zitto yanavutana, na jinsi Lema alivyokwaruzana na Zitto. Utagundua kuna sehemu mwandishi akaandika "muda wote wakati Lema akiyasema hayo Dr Slaa alikuwa kimya" plus maneno mengine yaliyofuata yakionyesha Slaa alitakiwa kuingilia kati.(mtu anaweza ku-paste hiyo portion). Swali la kujiuliza hivi mwandishi hajui kuwa Dr Slaa ni Katibu na kwamba kikao kinaongozwa na Mwenyekiti?
   
 15. h

  hoyce JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kwa kiwango kikubwa linatumiwa na Zitto Kabwe kupitia urafiki wake na Msacky, Mhariri Mtendaji. Hiyo story ya CHADEMA, ililenga kumfichia aibu Zitto aliyesimamia kuteuliwa kwa Shibuda.

  Kaingiza ishu ya magari iliyojadiliwa kikao kilichotangulia, Lema alipambana kuhusu ishu ya Shibuda, lakini story ikahusisha na magari, na kupenyeza kuwa walioyapinga walisema yangemnufaisha Mbowe, bila kujali kuwa chama kimekuwa kikiyatumia tangu yakiwa mapya wakati wa uchaguzi.
   
 16. m

  mohamed ally Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakweli mi mwenyewe nina wacwac nalo nilikuwa mteja wao sana lakini siku ile wilbrod alipotangaza mafisadi niliingiwa na wasiwasi
   
 17. Mfatiliaji

  Mfatiliaji Senior Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kuandika habari ya Kufa au kutokufa kwa osama kuna uhusiano gani na kununuliwa kwa gazeti na mafisadi?
   
 18. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Inawezekana wameuza hisa nyingi kwa RA/New Habari CO.2006Ltd,waandishi wengi n mamluki hawaheshimu taaruma yao vueni 'gamba' kama Mayage jamii iwaamini kuwa 'Press is the fourth estate'vinginevyo hamna lolote
   
 19. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Inawezekana wameuza hisa nyingi kwa RA/New Habari CO.2006Ltd,waandishi wengi n mamluki hawaheshimu taaruma yao vueni 'gamba' kama Mayage jamii iwaamini kuwa 'Press is the fourth estate'vinginevyo hamna lolote
   
 20. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Unajua nami nilianza kuhisi hivyo. Leo nikalipekua nikaona hata. My sixth sense inaniambia kuna tatizo.
   
Loading...