Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,011
- 144,371
Kichwa cha habari kinasomeka:
"Njaa kali yaja"
Chini yake kuna maandishi madogo yanayosomeka:
"Akiba ya chakula yakauka"
Kwa kifupi, gazeti hili la Agosti 15-21,2016, Toleo Na.352,limeandika habari ya serikali kutokuwa na akiba ya kutosha ya chakula na zaidi limenukuu maelezo ya Kafulila kuhusu kushuka kwa akiba ya chakula alipoongea katika kongamano liliokuwa limeandaliwa na Baraza la Vijana wa Chadema mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ukisoma habari nzima ambayo inayohusisha pia sehemu ndogo ya taarifa/maelezo ya Waziri wa Kilimo wakati akisoma bajeti ya wizara yake Bungeni mwaka huu,utagundua hakuna habari yoyote ya nyongeza kwa lengo la kuongeza chumvi zaidi ya kutumia taarifa ya Kafulila na maelezo ya Wazi Nchemba Bungeni kama chanzo tu cha taarifa hii.
Sasa wadau, licha ya habari yenyewe kutokuwa na kitu kipya, lakini kwa kutumia hiyo heading,gazeti hili litasalimika?
Labda swali la msingi ni je, kinachogomba ni kichwa cha habari au ni habari yenyewe?