Gazeti la MwanaHALISI lashinda kesi mahakamani na kurudi mtaani

Mwanahalisi limeshapitwa na wakati wale wavujishaji siri wa ndani wameshadhibitiwa na awamu ya tano,labda liwe la kufungia vitumbua.
Badilisha Avatar,weka picha ya BASHITE
Unamdhalilisha Tupak Amar Shakur
 
Ngoja wAkaeneze tena uzushi. Nachukia sana magezeti ya uzushi kama mwanahalisi, tz daima na jamhuri.

Ungeenda mahakamani kutoa ushahidi wa uzushi wao. Nyie ndio wale wanaume mlioajiriwa na wanaume wenzenu, na hamuwezi kuendesha maisha yenu sharti mjipendekeze.
 
Kwa hali hii ya siasa ya jiwe..sitashangaa hata huyo Kubenea akaingia CCM.

Kama gazeti limeachiwa huenda ni kumsafishia njia ya maongezi.
 
Said Kubenea anasema, "tumepata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 2.2, tunaenda mahakamani kudai fidia na tutamshitaki binafsi aliyekuwa Naibu Waziri wakati huo Anastazia Wambura
Kuna mwanasheria fulani huwa anasema kuiwa inawezekana kumshtaki mtumishi wa serikali yeye binafsi kwa makosa aliyofanya aliwa mtumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yake - nitafuatilia sana kesi hiyo
 
Mwanahalisi limeshapitwa na wakati wale wavujishaji siri wa ndani wameshadhibitiwa na awamu ya tano,labda liwe la kufungia vitumbua.
wewe kwa akili yako unadhani kwa nini hiwe siri?tangu lini jambo jema likafanywa siri,unatakiwa usikitike kwa kukosa watu wa kukuambia siri inayofanywa dhidi yako
 
Kuna misemo inasemwa na watu wa mtandao kwamba vigezo na mashariti kuzingatiwa hapa lazima Kuna kubadilishana gazeti kwa kadi ya chama yajayo
 
Wameona hakuna haja tena ya kulifungia maana nao wana gazeti lao la kujibu mapigo, tanzanite
 
karibu mwanahalisi, kwaheri kubenea tunakutakia kila lililo la kheri huko ccm
 


Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi wachapishaji wa Gazeti la Mwanahalisi Said Kubenea amewaambia Waandishi wa habari kuwa Gazeti la Mwanahalisi limeshinda kesi Mahakamani na Mahakama imeamuru lirejee mtaani tena.

Mahakama imetengua amri iliyotolewa kwa Mkurugenzi wa Hali Halisi ya kumtaka aombe tena upya usajili wa Gazeti na imesema amri iliyotolewa haikuwa halali ilikuwa batili na haikumtendea haki" - Nashon Nkungu Wakili wa Kampuni ya Hali Halisi

Sisi kama Mwanahalisi tumepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama na tulitegemea uamuzi kama huo Uamuzi umethibitisha kuwa Gazeti letu limekuwa likiandika ukweli na hiyo ndio sera yetu kwa miaka yote tuliyoa huduma" - Said Kubenea Mkurugenzi wa Hali Halisi

Niwaombe sana ndugu zangu tusiache kuamini Muhimili wa Mahakama, tusiache kudai haki zetu mahakamani, tunaamini Mahakama zetu bado ziko huru" - Said Kubenea

Said Kubenea anasema, "tumepata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 2.2, tunaenda mahakamani kudai fidia na tutamshitaki binafsi aliyekuwa Naibu Waziri wakati huo Anastazia Wambura

"Kwakuwa tulimwachia muda mrefu Dk. Abbas awajulishe kuwa Mahakama imetengua uamuzi wa kufungiwa kwa Gazeti la Mwanahalisi na ameshindwa kuwajulisha sisi tumeamua kuwajulisha na mpaka jumatano ijayo Gazeti litakuwepo mtaani."- Said Kubenea

Yamekuwepo maneno hasa baada ya Mwita Waitara kujiunga na ccm mimi kwanza sijawahi kuzungumza na mtu yeyote wa CCM, madhira niliyopitia mimi Serikali ikakataa kunitibu, naomba niwaambie mimi siondoki humu (CHADEMA) - Said Kubenea

Said Kubenea akizungumzia maamuzi ya Mwita Waitara kuhamia ccm anasema anaheshimu maamuzi ya Waitara ila kuwaacha wananchi wa jimbo la Ukonga sio jambo zuri, anaaema ndoa zina matatizo, maisha yana matatizo na hata siasa nazo zina matatizo

leo Dr. Abbas amekana kwamba hawana taarifa ya mahakama najiuliza walivyoenda kusikiliza hukumu ya kesi hakukuwa na mwakilishi wa serikali na mwanasheria mkuu mbna tunaona mizengwe jamani
 
Ngoja wAkaeneze tena uzushi. Nachukia sana magezeti ya uzushi kama mwanahalisi, tz daima na jamhuri.

Tatizo lako kubwa ni kutokujua tofauti kati ya UKWELI na UZUSHI, Zao Kayumba skuli!!! Pole.
 
Heko zao Kubea na Hali Halisi Publishers.....
Ukweli ni kwamba katika Magaezti yenye Habari za Uchunguzi(Investigative Journalism) Mwanahalisi lilikuwa likishika namba ya kwanza...!!!Haya mahgazeti mengine hasa ya Serikali, CCM na vikaragosi vyake yamejaa UMBEYA, UDAKU na UCHOCHESI dhidi ya UPINZANI.....Tunarikaribisa Mwanahlisi lianze kutuletea habari moto zilizokweda shule...!!

Natamani wangeongeza ubunifu hasa kwa kurudi huku wakafanya yafuatayo
Kufanya chambuzi kwa kushirikisha wanataaluma wote muhimu (task force) mfano Sheria, Uchumi, Fedha, Habari, Retired Police or similar Investigators, Public relations, Engineers, Business men, Wananchi, Wanasiasa pande zote (Oposition and ruling party), Raslimali watu, nk. Kisha taarifa hizo zikawa zinatoka kila week mara moja. Taarifa hizo zikajikita kwenye kutunza kumbukumbu (investigations reports/findings), kupendekeza corrective actions, kufuatilia wenye mamlaka kuhusu utekelezaji wa mapendekezo, updates zikawa zinatoka kila week.
Lengo kubwa zaidi ikiwa ni kuhakikisha kwamba jambo lolote kubwa lenye maslahi kwa Taifa linachambuliwa kwa kina, mapendekezo natolewa na kutekelezwa. Hii itaondoa tabia ya watu kuanzisha mijadala ya muda mfupi kwa malengo yao.
 
Back
Top Bottom