Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

tukiliona limepotea nitaamini lakini all in all tumeshamjua aliyemteka dr ulimboka hata wakilifungia ushaidi upo,sidhani kumbe kusema ukweli ni uchochezi????????
 
jamani mwenye makala za uchunguzi ziivyoandikwa na gazeti hili juu ya Dr Ulimboka anitumie kwenye PM maana akiziweka hapa mods hawakawiikuzifuta hata kama kuna blog ambayo imeweka naomba link tafadhali...
 
Kuanzia leo Julai 30, 2012; Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa na serikali kwakuwa linadaiwa kuandika habari za uchochezi.

CHANZO: TBC1

Wajameni serikali hii inataka kutufunga mdomo tuendelee kuwa gizani tusijue madudu yao.

Pole sana KUBENEA tupo na wewe habari zako za kiuchunguzi zinatusaidia sana na ndizo zinazotufungua macho tujue nchi yetu inavyoliwa.

Yes ni kweli kabisa hata mimi nimesikia live.

Hili ni jambo lililotegemewa na wapenda haki. Serikali ya kidikteta huwa siku zote haikubali kuambiwa ukweli. Kile kilichoandikwa na MWANAHALISI ni ukweli,ukweli mtupu. Mwanahalisi limekuwa likijidhihirisha kwa ule msemo wa enzi za Nyerere wa TANU kuwa, ''Nitasema kweli Daima,Fitna Kwangu mwiko''.

Mimi nina ushauri kwa Baraza la Habari Tanzania(TMC) na Media zote hili jambo wasilinyamzie na walikatae kwa nguvu zote kabisa. Tunataka viongozi wake wazungumze na Serikali na iwathibitishie kuwa Habari zilizoandikwa na gazeti hili ni za Uchochezi. Wawaulize watu wa Serikali kama kuandika ukweli usiotiliwa shaka pamoja na ushahidi wa Majina,Namba za simu,nyadhifa zao na idara za wahusika wa sakata la Dr. Ulimboka ni uchochezi. Lakini pia Serikali waulizwe kwanini mpaka sasa watuhumiwa wa sakata la Dr.Uli hawajakamatwa wala kufikishwa Mahakamani ukiachilia mbali The Comedy Show ya Kamanda Kova na Mkenya wake wa kutengeneza!

Kama serikali hii ya Mafisadi haitawasikiliza TMC na media zote Tanzania basi swala hili lipelekwe Mahakamani. Tuna amini Mahakama itatenda HAKI ambayo kila siku inazidi kusiginwa na Serikali ya Magamba.

Hivi mtu akiitwa Mahakamani kutoa ushahidi au kuisaidia Polisi kwenye tukio husika ili mhusika akamatwe au kushtakiwa ni UCHOCHEZI???Nauliza tu!

 
Top of the Toppest Hopelessness of this Era in Mankind History!
Look this resemblence:
-Mtu anasema ukweli na kudai haki za kundi lake, anatekwa na kusulubiwa!
-Gazeti linaongea ukweli, linafungiwa kwa kipindi kisichojulikana!

Huu ni mfanano wa aina yake na inaonyesha aliyemteka Ulimboka ndiye huyo aliyelifungia gazeti!
Sometimes mtu anafanya matendo ambayo anajivua nguo na kujidhihirisha jinsi alivyofika mwisho wa fikra!


RIP TISS
 
Hili ni muhimu sana. Wasiogope kufungiwa na hii Serikali dhalimu ni lazima waibane kwa kuandika ukweli wa madudu mbali mbali kuonyesha kwamba haturidhiki na utendaji wake sasa badala ya kusubiri hadi 2015 huku vitisho, mauaji na ufisadi wa hali ya juu ukiendelea kufanywa ndani ya nchi yetu.

Magazeti mengine yaanzie hapo mwanahalisi lilipoishia,tunataka magazeti yaandelee kuandika ukweli....yakifungiwa yote then safari ya kwenda magogoni itakuwa imekamilika
 
Wakuu hivi MwanaHalisi wakienda mahakamani huu uamuzi hauwezi kupinduliwa? au ndo hivi tena Kikwete ndo jaji mkuu,ndo spika ndo kila kitu...
 
nilidhani wamemfungia kubenea kutoandika kumbe ni gazeti mbona akili ya kitoto sana hii. si ataanzisha gazeti jingine?
 
Ukiona umeshindwa kutumia njia zozote zile mbadala unafikiri njia gani itakayotumika? Ni maguvu tu
 
Magazeti mengine yaanzie hapo mwanahalisi lilipoishia,tunataka magazeti yaandelee kuandika ukweli....yakifungiwa yote then safari ya kwenda magogoni itakuwa imekamilika

Kubenea hana ukweli wowote, yeye ni mchonganishi na mzushi, na kama uko karibu nae mwambie hivyo hivyo na wananchi wanajua hivyo
 
Watanzania tumuogope sana mtu anaechochea chuki na fitna katika nchi yetu.ni hatari sana kwa ustawi wa jamii iliyostaarabika.mwanahalisi ilikuwa inaipeleka nchi kubaya.
 
Wanaweza kutumia mabavu kwa kipindi kifupi kwa wanaosema ukweli unaouma, lakini hawawezi kuzuia ukweli usipite wakati wote. Muda utasema...Kubena nakupa big up! Mwanahalisi nawapa big up too! Waandishi wengine mngejifunza kutokana na hili kwa kuandika habari za ukweli sasa ili wafungie magazeti yote tuone kama hatutapata habari. Huu ni udictator!
 
Back
Top Bottom