Gazeti la MwanaHalisi lafungiwa kwa muda usiojulikana!

Aliyemteka Ulimboka ni Ramadhan Ighondu a.k.a Rama na Jack Zoka wote wa Usalama wa Taifa. Haya Serikali nifungieni na mimi!

TUMBIRI (Tunduru, Ruvuma - Tanzania),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Hivi nani aliwambia UN wapo kwa ajili ya kusaidia watu...mnapoteza muda wenu subiri majibu ya UN wataiwekea vikwanzo Tanzania kama Iran.
 
Ushauri, Kwakuwa serikali imetumia mabavu yake kukandamiza uhuru wa kupata habari; hasa kwa waandishi wazalendo kama hawa wa mwanahalisi waliotufungua macho juu ya utekwaji na hatimaye uteswaji wa dr ulimboka na pia vitisho kwa viongozi wa vyama vya upinzani ambao ni wapigania masilahi ya watanzania; Napendekeza vyombo vyote vya habari binafsi viungane na kutoa tamko la pamoja la kususia habari yoyote inayoihusu serikali ya kikwete ili kushinikiza kufunguliwa kwa gazeti la mwanahalisi kwakuwa wahenga walishasema, ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji nywele zako. Coz wakitoka mwanahalisi watakuja mwananchi n.k. Tafakari.

Hii walitakiwa waifanye Jana.
 
217869_266396890138231_439668299_n.jpg

Tatizo la watendaji wetu wanatumwa nao wadhaifu wenzao nao wanaenda kichwa kichwa kuuza sura kwenye TV, Hivi nani anatoa hukumu, mahakama au huyo aliyeshika magazeti??? @#%&^*#@%^&* Sana.
 
Ni mkakati mzuri, lakini Tanzania magazeti yasipogusa habari za Serikali yataandika kuhusu nini? Kwa kuwa habari nyingi za nchi hii kwenye magazeti zimejikita kuandika habari za mijini tu, ambazo Serikali ni mchangiaji mkubwa wa habari hizi...basi ushauri wangu, waandishi waanze kuandika habari za jamii, hususan za wananchi wanaoishi vijijini...zinaweza zikaonekana ni habari za kitabaka lakini mwisho wake zitaanza kuzoeleka na kuonekana ni habari muhimu na ndizo zinazopaswa kuandikwa, ili kumkomboa mtanzania mnyonge katika ujinga, umasikini, maradhi, dhuluma n.k

Waandike habari za CWT, CHADEMA M4C, Maendeleo ya Dr. Ulimboka, zinalipa sana!waachane habari za kiserikali! Hasa zinazohusu mawaziri, Watumie Tbccm tu kwa taarifa zao, ambayo wananchi tumeisusia kitambo!
 
Mtu ukikata tamaa na ukaamini umefika mwisho wa kuruhusu ubongo wako kutafuta suluhu yaan ile halisi ya chanzo cha matatizo yanayokuzunguka, unakuwa hayawani.
My take, tunaelekea kuna watu ndani ya system wapo ktk stage hiyo. Mungu asipotuepusha kuna siku mtu ataamlisha vifaru viingiye barabara kuzuia wanafunzi wanaodai haki yao ya kufundishwa. Tafakari
 
tena kwa sababu tz ina uhusiano wa kujificha na iran afadhari watufungie misaada maana ccm wakula hiyo misaada
 
wanaogopa sana,ila waliomtesa uliomboka kwa matesa ya namna ile hata shetani aligeuka pembeni na kusema mimi cjawatuma kufanya hivi.
 
Usemi wa kwamba ukweli UNAUMA ndo unajidhihilisha hapa;why mwanahalisi tu sio majira wala uhuru?may god curse this
 
mtc%20kajabu.jpg

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mkajanga


MCT yasikitishwa kufungiwa MwanaHalisi


Baraza la Habari Tanzania (MCT), limesema limesikitishwa na kitendo cha kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi kwa kipindi kisicho na ukomo na kwamba haliungi kusimamishwa wala kufungiwa kwa chombo chochote cha habari kwa sababu yeyote ile.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mkajanga, alisema baraza linaamini makosa na matatizo ya kitaaluma hayawezi kumalizwa katika kufungia magazeti ama aina yeyote ya chombo cha habari.

“Kufunga ama kusimamisha vyombo vya habari ni ukiukwaji wa wazi wa uhuru wa vyombo vya habari kwa sababu kunawanyima wateja wa chombo hicho haki yao ya kupata habari za chaguo lao,” alisema.

“Kunawanyima raia ambao wamekuwa wakitumia chombo hicho haki ya kueleza maoni yao, kunanyima uhuru wa kujieleza na kukwaza demokrasia, hivyo kusimamishwa kwa gazeti la MwanaHalisi ni jambo la kusikitisha,” aliongeza.

Aidha MCT ilisema sheria ambayo serikali imeitumia kulifungia gazeti hilo ni ile ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wadau wa vyombo vya habari.​
 
Liwalo na liwe, swala hili limeamuriwa na waziri, marufuku kujadiliwa...poor kikwete
 
Aisee yaani CCM sijui unaweza kuilezea kwa maneno gani ukaipatia juu ya UDHAIFU wake maana sioni maneno ya kutumia
 
Me nashindwa kuelewa ina maana hii serikali inajiamulia tu ina maana waziri yeye ndo mahakama?? Kama kuna habri ya uchochezi kwanini wasipeleke kesi mahakamani?? Walijua kabisa kesi atashinda mwanahalisi sababu anasema kweli me sikubaliani na hawa madikteta washenzi kabisa wanafanya Nchi kama yao......................na hawa wengne hawapendi nao wangegoma kuandika habari yeyeto ya serikali au kufanya maandamano nasi tutakuwa nyuma yao
 
Back
Top Bottom