Bashite lingine hili hapa.....Mawakala wa mapapa ya unga utwajua tu.
Mapapa wa unga wamechangishana zaidi ya bilioni moja kummaliza Makonda kisiasa kupitia bungeni mwezi ujao.
Itatumika style iliotumika kwa Professor Muhongo,kila mbunge atakae simama kumsema Makonda akitoka nje tu,anakwenda kuchukua bahasha yenye uzito unaolingana na makombora,litafanyika jaribio la kumtishia kumng'oa Majaliwa bungeni ili kuitisha serikali itii matakwa ya maharamia hawa,
Hawa mapapa wa unga wanaoungwa mkono na Chadema wakishirikiana na Gwajima,wanatumiana wenyewe kwa wenyewe ili kufikia malengo yao ya kisiasa na kijamii.
Chadema wanatumika kwa kuwa kwao wameona ndio njia ya kujipandisha chati yao ilioshuka vibaya sana,baada ya kukosa hoja ya kusimamia.
Gwajima anatumika ili kujiongezea wafuasi hatimaye sadaka inapanda,kama jana,alivunja rekodi tokea kanisa la kufufua watu lianzishwe haijapata kupokea sadaka kama jana lakini kwa mshangao wa walio wengi hakuna vyeti vya Makonda vilivyooneshwa wala wazee waliojitokezakuthibitisha kuwa Makonda ni Daudi!
Sisi tulioamua kuwa upande wa Mungu hatupo tayari kuona kijana wetu anayumbishwa na watu wachache wenye nia mbaya na nchi yetu.