Gazeti la mtanzania la tarehe 29/06/2012 - SOMA TAFADHALI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la mtanzania la tarehe 29/06/2012 - SOMA TAFADHALI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Jun 29, 2012.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Leo tarehe 29/06/2012 asubuhi mishale ya saa moja na nusu asubuhi nilikuwa naangalia mapitio ya magazeti katika televisheni ya ATN ambapo kelvin moto alikuwa akisoma mapitio ya magazeti. Alianza na gazeti la mtanzania na habari iliyokuwa kwenye ukurasa wa mbele ilisomeka siri ya kutekwa dk. ulimboka...........akisoma habari hiyo kwa masikitiko makubwa kelvin motto alisema dokta ulimboka alimtambua mmoja wa wanajopo wanaounda timu ya uchunguzi iliyoundwa na jeshi la polisi kuwa ni mmoja kati ya watu waliomteka na hivyo kumwambia amrudishie simu yake na waleti yake. Pia alisema afande huyo ambaye hakutajwa jina kwenye gazeti alimuuliza dk ulimboka kama chadema wanahusika na utekwaji wake. Habari hiyo ambayo iliripotiwa na gazeti hilo kutoka chanzo cha uhakika iliendelea kusema mara baada ya kuona ametambulika afande huyo alitoka wodini kimya huku ameinamisha kichwa chini.

  Nilipatwa na shauku kubwa sana ya kusoma gazeti hilo ili nipate undani wa mkasa huo. Kitu cha ajabu nilipoenda kununua gazeti la mtanzania nikakuta ukurasa wa mbele kuna habari inayosomeka hivi "madaktari waanza kusimamishwa kazi" nilishangaa ikabidi nifungue kurasa za ndani kuitafuta habari niliyoitaka bila mafanikio. Nilijiuliza maswali mengi bila majibu. Kwanza nikawaza inawezekana mtanzania wametoa version mbili za gazeti lao leo, pili nikasema inawezekana nilisikia vibaya labda lilikuwa ni gazeti la tanzania daima lakini hailkuwa hivyo, tatu nikasema kuna mazingara yamefanyika au, nne nikawaza au nilikuwa naota lakini nikasema hapana. Nauliza kama kuna mwanajamvi yeyote aliye angalia ATN na kusikia wakati kelvin motto akisoma mapitio ya magazeti ili anisaidie kunipa majibu. Maana kelvini aliisoma kwa msisitizo na kuwataka wananchi wanunue nakala ili waone nchi yetu ilipofika. Natamani ningekuwa na namba ya simu ya kelvin motto nimuulize huenda angenipa jibu.
   
 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hujakosea kabisa. Ni kweli kwamba leo gazeti la Mtanzania lina habari 2 zinazochanganya kwenye front page.Ukiingia kwenye gazeti la mtanzania online unapata habari tofauti na iliyojitokeza kwenye gazeti hilo asubuhi. Ukiangalia kwenye millard ayo blogspot,gazeti la mtanzania linaonyesha kwamba Dr. Ulimboka amemtambua mtuhumiwa na kumwomba wallet na simu yake. Angalia hata sasa kwenye millard ayo blogspot kwenye sehemu ya magazeti ya leo.

  [​IMG]


  Source: Millard Ayo blogspot,29.06.2012
   
 3. Kakati

  Kakati Senior Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  jamani ukweli ni upi hapa JF ina watu wengi m akini, tusaidieni
   
 4. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Inawezekana wametoa version mbili leo ila mimi nimenunua lenye habari iliyosomwa ATN. Kuna jina moja la askari limehifadhiwa ila ametajwa mtu anayeitwa Ayoub kuwa ndie aliyempigia simu dr. Ulibomka kabla ya kutekwa.
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  inategemea habari hiyo wameipata muda gani. habari moto zikifika wakati gazeti liko mitamboni kuna kitu kinaitwa stop press ambapo uchapaji
  husimama na gazeti kupangwa upya. sasa nakala za awali hutumwa mikoani hivyo magazeti hayo yataikosa hiyo habari moto.
   
 6. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Nikweli inachanganya lakini ukiangalia vizuri habari hiyo ipo imelezea kisa kizima ya jinsi ilivyotokea ukiangalia vizuri kurasa kama sikakosea ya tatu utaiona hata mimi ilinichukuwamuda kuiona.
   
 7. Eraldius

  Eraldius JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2012
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hukumu ya lema
   
Loading...