Gazeti la Mtanzania kusitishwa kuanzia Mei 20, 2019 ili kupisha marekebisho

Magazeti yanayochapwa nchi hii yasipobadilika na kujikita katika habari za uchunguzi,maoni na makala yote yataenda katika kaburi la kibiashara, ni watu wachache sana wamebaki kununua magazeti ili kusoma breaking news, kiongozi kasema nini na ziara za wanasiasa.Mitandao,televisheni na redio vimechukua nafasi hiyo vizuri kwa sasa.
Njia pekee iliyobaki kuwavutia wanunuzi ni habari za kina za kiuchunguzi,maoni na makala.
 
ccm mbele kwa mbele
FB_IMG_1557949711703.jpeg
 
Wengine wajiandae. Mzee wetu Marhum Mengi aliishaliondoa sokoni lake la Sunday Observer...
 
Tumejipangaaaa hao wanaopunguzwa kazi mafao yao wakayadai wakifika miaka 55
Pombe hoyeeeeee
 
Namba inaendelea kusomwa teh!

#HapaKaziTu
#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi huwa nashangaa sana hawa wamiliki wa magazeti. Wanashindwa kusoma alama za nyakati. Sasa hivi almost 50% ya wanaotumia simu, wanamiliki smarttphone. Habari zinapatikana kwenye mitandao all the time. Watu hawasomi tena magazeti zaidi ya kuangalia vichwa vya habari baada ya hapo ni kuingia mtandaoni kutafta habari iliyomvutia na kuisoma kwa undani zaidi.
Kwa taarifa yako kaka,kuchapisha habari kwenye mitandao haijaanza bongo,ulaya huko ni muda mrefu sana wanatumia mitandao na wanachapisha habari zao kwenye mitandao na hardcopy ya magazeti yanaendelea kila siku.

Shida ya Bongo magazeti ya sasa hayana Content ya kueleweka, watu wenye akili hawawezi kutoa pesa zao na kununua gazeti zenye habari sizoeleweka. Wao wapambane na Content,wapambane na sheria kandamizi za magazeti ili watoe habari za haki au waache kukumbatia serikali. Kama wataendelea kuandika habari za mapambio za serikali bila ili wawafurahishe,basi magazeti yote yatakungwa muda si mrefu.
 
Kwani lilikuwa linatumia mifuko ya plastic a.k.a Rambo ktk uzalishaji wake?
 
Kwa hiyo zile gari za kupeleka magazeti Moshi/Arusha kwa mwendo kasi hazitakuwepo tena? alimaarufu "gari za magazeti" ukipanda ushike roho mkononi
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom