Gazeti hili la TANZANIA DAIMA linalomilikiwa na mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Aikael Mbowe siku hizi limepoteza mvuto kwa wateja limekuwa kama gazeti la UHURU la chama cha mapinduzi kwa kugeuka kuwa gazeti la Propaganda la CHADEMA nilikuwa ni mteja mzuri wa gazeti hili la TANZANIA DAIMA lakini kwa sasa nimekuwa hata kuliona sitaki, kama ilivyo vile vile kwa gazeti la UHURU, nawaomba mhariri mkuu abadilike kwani huko tuendako litakosa soko kabisa na litashindwa kujiendesha.