Gazeti la "Kulikoni" lafungiwa miezi mitatu; kutoka Jumatatu?

ndugu zanguni nashindwa kuwaelewa wote waliochangia mada hii. mada ni kuhusu gazeti la kulikoni kutoka kwa nini isijadiliwe mada hiyo badala ya kuanza kujadili mtu binafsi. nilitamani sana tujadili uhalali wa gazeti kufungiwa na uhalali wa gazeti kuendelea kutoka. tufikie wakati tujifunze jinsi ya kuchangia mada kwa kuzingatia mtoa hoja mama.
nimeboreka sana na thread hii!! watanzania bado tuna safari ndefu ya kuchambua mambo!!. du du du du du!!!
Nat'

you have just missed the train... just go bck to this thread and read it through, some of contributors didnt take it personal kabisaaa, unless ninamiss kitu!!!

Yes we have a long way to go, but i think you too have a long way to go because you just took afew striking posts and wrapped up the thread... :confused:
 
Kulikoni lipo mitaani na mimi ninalo hapa nasoma mezani, moja ya habari ni kwamba JWTZ linakodisha meli za kivita kusindikiza meli za watu binafsi kuogopa mahalamia wa kisomali!!. Which is True, hata leo hii kuna meli ingine ya kivita ipo bahari ya hindi inailinda meli ya kinorsk inayofanya utafiti wa mafuta na itakuwepo huko kwa miezi mitatu kuanzia December 25th 2009.

Thanks Mpendanchi... I wish SteveD naye angechangia hii mada, yuko deep sana aisee
 
nasikia moja ya habari kwenye kulikoni , ni kuhusu dowans, kwamba hajasajiliwa kokote kule duniani, wenyewe wana haha kuisajili?
 
SIKU tatu tangu kufungiwa kwa gazeti la kila wiki la Kulikoni, mmiliki wa gazeti hilo, Reginald Mengi ameingia katika mzozo mpya na ofisi ya Msajili wa Magazeti na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Tanzania Daima limebaini.
Mzozo mpya kati ya mfanyabiashara huyo maarufu anayemiliki mtandao wa vyombo vya habari nchini na serikali umekuja kutokana na hatua ya msajili huyo kumuandikia barua akitaka atoe maelezo ni kwa nini amekiuka amri ya serikali ya kulifungia gazeti hilo kwa siku 90 kuanzia jana.

Hatua hiyo ilimkera Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti wa muungano wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini na kuliambia Tanzania Daima: "Mimi nashangaa. Sijawahi kuona serikali inayogombana na vyombo vya habari hasa katika mwaka wa uchaguzi. Ni jambo la kusikitisha sana. Huku ni kuzusha mtafaruku na kuruhusu ufisadi uendelee. It's very sad!"

Leo Kulikoni limeonekana mitaani kama kawaida.......yetu macho tusubiri tuone nani zaidi, Mengi au Mkuchika.
 
Wakuu wanasheria wa JF msaada kwa mwalimu hapa
Hivi sheria inakataza kutoa online edition ya gazeti kama limefungiwa?
 
hivi mbona nchi hii .serikali yetu inavutuko vingi sana .. viongozi akili zao zimelala ..sijui lini itaamka
eti nchi huru na yenye amani ...inasikitisha
 
nasikia moja ya habari kwenye kulikoni , ni kuhusu dowans, kwamba hajasajiliwa kokote kule duniani, wenyewe wana haha kuisajili?
Baada ya hii habari kuonekana kwenye gazeti la jana naamini itakuwa imeongeza hasira za wakubwa. Hii itasababisha mkwaruzano mkubwa zaidi! Let's wait n see
 
Baada ya hii habari kuonekana kwenye gazeti la jana naamini itakuwa imeongeza hasira za wakubwa. Hii itasababisha mkwaruzano mkubwa zaidi! Let's wait n see
Hata ilipofika machweo ya jua , Giza kuu likatanda juu ya nchi, watu wakaingia na hofu, mara mngurumo mkubwa ukapiga, hata pazi kwenye hekalu kuu ukapasuka katikati, naam watu wakasema hakika "Dowans ni Serikali na Serikali ni Dowans"
 
Hata ilipofika machweo ya jua , Giza kuu likatanda juu ya nchi, watu wakaingia na hofu, mara mngurumo mkubwa ukapiga, hata pazi kwenye hekalu kuu ukapasuka katikati, naam watu wakasema hakika "Dowans ni Serikali na Serikali ni Dowans"


Una maana Serikali ilikuwa inakimbia kivuli cha Dowans? Bongo ni tamu kweli kweli. Huwezi kuwa kwenye payroll ya mtu halafu ufanye kinyume na matakwa yake. Kwa maana hiyo walitumia hadithi ya jeshi kama kisingizio??:confused:
 
Wakuu wanasheria wa JF msaada kwa mwalimu hapa
Hivi sheria inakataza kutoa online edition ya gazeti kama limefungiwa?
.
Bahati mbaya Tanzania hatuna cyber law, hivyo limepigwa marufuku kuchapishwa, on line kwa tafsiri ya Tanzania sio kuchapishwa.

Majira lilipigwa marufuku Zanzibar, baada ya kuchapisha picha za unyanyasaji wa polisi. Lilipopigwa marufuku, on line edition ikawa more popular ZnZ kuliko print out yake.
 
Rafiki yangu anayefanya kazi kwenye gazeti la Kulikoni ameniambia kumbe Mkuchika alikurupuka tu kwenda kwenye vyombo vya habari kutangaza kufungiwa kwa gazeti lao bila kuwasilisha barua rasmi kwa wahusika. Eti barua imepelekwa Kulikoni siku ya Jumatatu tarehe 11 Januari, siku tatu baada ya kutangaza kufungiwa kwa gazeti. Najiuliza hivi serikali inafanyaje kazi zake. Walitegemea kweli watu wasikie redioni na kutekeleza agizo? Hata hivyo, nadhani cha kujadili hapa ni kama kweli habari inayohusu jeshi au taasisi nyingine kama usalama wa taifa haipaswi kuandikwa?
 
i1418_untitled.bmp

 
ivi kuna mtu ana kopi na hiyo story ya Kulikoni ambayo serikali inasema threatens national security?>
 
Back
Top Bottom