Gazeti la Jamvi la habari lifungiwe kwa kuandika habari za uongo kwa nia ya kumsifia Rais

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,378
21,070
Kwa hakika nchi yetu kwa sasa imekuwa feki kwa 100%.

Kitu pekee kilichobaki ni kumsifia Rais Magufuli hata kama anachokifanya si sahihi ili mradi tu na wewe upate tonge la ugali.

Kwa hakika nimesikitika sana kuhusu gazeti la Jamvi la habari kuandika habari ambazo ni uongo uliopitiliza kwa nia ya kumfanya Rais Magufuli aonekane anafanya mambo makubwa makubwa hapa nchini hususani kwenye suala zima la jeshi.

Kuna habari imeandika mambo haya kuhusu makomandoo wa Tanzania waliopatikana kipindi Rais Magufuli yupo madarakani, waliainisha sifa zao kama ifuatavyo;

1)Hawawezi kudhurika hata kidogo wakipigwa panga au kitu chochote chenye ncha kali, huwa kinadunda tu na wakati mwingine kinapinda kabisa bila kumdhuru huyo Komando wala kumpa maumivu au alama ya aina yoyote ile.

2)Hawa makomando wakikupiga teke moja unakufa hapo hapo ila kama mtu mwenye mafunzo unazimia siku tatu.

3)Wanapiga mateke futi kumi na mbili.

4)Wanaweza kupiga teke moja watu kumi kwa mkupuo.

5)Wanaweza kukaa bila kula chochote kwa miezi mitatu bila kudhurika.

NB: Bora hili gazeti lifungiwe tu kama wanavyofungia magazeti mengine kwa kuandika taarifa za uongo.

Screenshot_2017-12-10-17-42-04.jpg
 
Acha kabisa.......
Magu ni nouma. Hata majengo aliyosimamia yanaweza kutanuka na kusinyaa bila shida yoyote kwa kutumia mfumo wa expansion joints....... Hapo sijazungumzia kivuko cha kipekee kuwahi kutokea ulimwenguni. Kilifanya kazi miezi mitatu na kupotelea kusikojulikana kabla ya kuwa Mali ya jeshi. Uuzaji wa nyumba hapo usiseme, alijali sana wanyonge katika hili.
Huyu ndiye RAHISI wa wanyonge.
 
unamfungia mtu kuuza maindi yake lakini unamlisha kwa muda wote ambao hatouza maindi maana imekubidi kumfanya mfano japo maindi alikuwa anakuletea kwa bei rahisi nia ikiwa ni kutisha wasiokuuzia......tafakari
 
Acha kabisa.......
Magu ni nouma. Hata majengo aliyosimamia yanaweza kutanuka na kusinyaa bila shida yoyote kwa kutumia mfumo wa expansion joints....... Hapo sijazungumzia kivuko cha kipekee kuwahi kutokea ulimwenguni. Kilifanya kazi miezi mitatu na kupotelea kusikojulikana kabla ya kuwa Mali ya jeshi. Uuzaji wa nyumba hapo usiseme, alijali sana wanyonge katika hili.
Huyu ndiye RAHISI wa wanyonge.
Haki ya Munguuuuuuu!
 
Naomba kujua yale mabegi ya makomandoo yana uzito kiasi gani, kwani jana MC wa shughuli alisema 75kg, ila mtangazaji wa TV alisema 150kg.
 
Back
Top Bottom