Gazeti la Jamhuri: TBL ni Jipu

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Leo nimepitia Gazeti la Jamhuri kwa kweli ninawapa HONGERA KUBWA kwa utafiti wa kina mnaoufanya kabla ya kutoa taarifa kwa umma.

Kichwa cha habari ya leo TBL NI JIPU nimelisoma na kujua kweli nchi hii inavyoibiwa na Kampuni ya TBL.

Jinsi wanavyokwepa kodi, kuuza konyagi kwa bei ya chini, Hakimilki yya konyagi, kibuku inayouzwa kwa fedha za kigeni, jinsi wazawa wanavyofukuzwa kazi hovyo akiwemo Ndugu Mgwassa,Jinsi wazawa wanavyonyimwa nafasi za juu, Jinsi Bodi ya Wakurugenzi wanavyotekeleza matakwa ya wazungu,jinsi wazungu 43 wanavyolipwa mamilioni ya fedha nk.

Hongereni sana mmetufumbua macho haya yote hatukuyaelewa.

Namshauri Mhe.Magufuli wafanyakazi wa Gazeti la Jamhuri wapewe tuzo na ulinzi na ikiwezekana wanunuliwe vitendea kazi.
 
Konyagi "the spirit of the nation' inamilikiwa na nani?
Tanzania Distillers kwa knowledge yangu na hii haihusiani na TBL. Hata hiyo Kibuku haimilikiwi na TBL sijui taarifa hii ina ukweli kiasi gani.
 
Tanzania Distillers kwa knowledge yangu na hii haihusiani na TBL. Hata hiyo Kibuku haimilikiwi na TBL sijui taarifa hii ina ukweli kiasi gani.
kuna kitu inaitwa TBL Group; inamiliki Dar Brew (chibuku), TDL (konyagi) na wenyewe TBL. watu washapiga hela kitambo
 
Mkuu ingekuwa vema kama ungeweka gazeti lenyewe alafu mwishoni ndo ungetoa mawazo yako kuliko kuwasifia kulikoni sisi hatujui kilochoandikwa. Naomba uattach kipande cha gazeti hilo.
 
Kuna yanayofanyika na TBL ambayo ni Majipu makubwa kabisa,mfano

.Mwekezaji kaburu wa Tbl kufanya transport/kusambaza bidhaa zake mwenyewe kinyume na makubaliano ya mkataba wa uwekezaji.Kazi ambayo ilitakiwa ifanywe na kampuni za kizawa.

Tbl kumiliki vituo vya usambazaji mikoani,kinyume na taratibu za uwekezaji,ambapo depot hizo zingemilikiwa na wazawa.

Tbl kunyanganya wawekezaji wa ndani tender bila sababu ya msingi,huku wakitaka kujipa tender kampuni zao kwa tender price kubwa kuliko za kampuni za ndani ambazo hata hivyo zilikua zinafanya vizuri sana na kwa bei shindani mpaka kufikia mafanikio waliyonayo sasa Tbl.

Tbl /Makaburu kukataa kuongozwa na Mtanzania Bw Mgwasa,hivyo kupelekea kumfuta kazi bila kufwata taratibu,
Wakati huo wawekezaji hao hawana CV iliyoshiba kama ya Bw Mgwassa ambaye ameifanyia mambo makubwa TBL.

Hayo na Mengine meengi yataendelea kuanikwa hapa juu ya uozo wa Tbl.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom