Gazeti la Jamhuri laponza uhamiaji?: Watimuliwa kazi! Picha zao hizi gazetini! Ni ukiukwaji wa haki za binadamu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Baada ya mfulilizo wa Makala mbili gazetini kuhusu madudu ya Uhamiaji kwenye suala la e-passport, leo watumishi kadhaa wa Uhamiaji wametimuliwa kazi kwa picha zao kuwekwa gazetini, bila makosa yao kutangazwa!. Inawezekana ni kutokana na Makala za gazeti la Jamhuri?.

Makala zenyewe ni hizi.
Wakubwa "wampiga" Rais Magufuli e-passport

Habari ya UCHUNGUZI: Wajue vigogo walioshiriki kufanikisha dili la 'e-Passport'

Mimi niliwahi kuwa mtumishi wa umma, na nilitimuliwa kazi kwa summary dismissal, na ilikuwa nitangazwe gazetini, lakini niliusoma muongozo wa Utumishi wa Umma kupitia Standing Orders za Civil Service Regulations, Mtumishi wa Umma, hawezi kufukuzwa kazi na kisha picha yake kubandikwa gazetini, kuwa fulani sii mtumishi wa umma bila kuweka sababu, au kosa alilofanya!.

Angalieni hiki kilichofanywa na Idara yetu Uhamiaji.
UHAMIAJI: Wafanyakazi 18 watimuliwa kazi, picha zao zaanikwa hadharani
whatsapp-image-2018-02-14-at-10-28-38-jpeg.695411

whatsapp-image-2018-02-14-at-10-28-42-jpeg.695410

Huu ni ukiukwaji Mkubwa wa haki za binaadamu, hawa waliofanyiwa hivi, wakipata wakili mzuri, wanafungua kesi mahakamani kudai fidia, na Serikali inabagwa asubuhi tuu mapema!.

Mtu kufukuzwa kazi na picha yake kutangazwa gazetini, hatua ya kwanza ni mtu huyo kuwa amefanya kosa la uhalifu, criminal offence, pili ofisi yake imemfungulia mashitaka ya jinai, tangazo hili linatakiwa kuelezea kosa lililotendwa, ili kuisaidia public kujua Fulani ni mhalifu!.

Utaratibu mzima wa kuachishwa kazi kwa watumishi wa umma, uko wazi kabisa, huwezi kumfukuza kazi mtumishi wa umma, na kuitoa picha yake gazetini as if ni mhalifu fulani!, huku ni kinyume cha haki za binaadamu.

Kwa vile tangazo hili halikusema hawa watu wamefanya kosa gani, then inawezekana hawa watu wameponza na wana JF wenzetu wawili humu jukwaani, Manyenyere Jacton na Deodatus Balile kupitia gazeti lao la Jamuhuri, kufuatia mfufulizo wa Makala hizi.

Ombi kwa watendaji wa Serikali, Utumishi wa umma unaongozwa kwa sheria, taratibu na kanuni za Utumishi wa umma, hivyo katika kutimiza majukumu yao, wanawajibika kuzingatia sheria, taratibu na kanuni, hivyo hata kama ni kuwatimua watumishi wake kwa kosa lolote, sawa watimuliwe tuu, lakini katika kutimuliwa huko, haki zao zizingatiwe!.

Kama Mhimili wa Serikali ndio wenye jukumu la kutenda haki, serikali isipotenda haki, Mhimili wa Mahakama upo, kuhakikisha unaisimamia Serikali katika kutenda haki, hivyo wote waliotimuliwa kazi Uhamiaji kwa udhalilishaji huu, msikubali, nendeni mahakamani mkapate haki yenu. ikiwemo fidia dhidi ya udhalilishaji huu mliotendewa!.

Paskali
Update
Kumbe ni sababu nyingine na sio e -passports na tangazo ni la tahadhari tuu na sio la kufukuzwa kazi.
Idara ya Uhamiaji imewatahadharisha wananchi kuwa makini na waliokuwa watumishi wake walioacha kazi kwa sababu mbalimbali ikiwamo kufukuzwa mwaka 2016/17.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala alisema jana kuwa kati ya watumishi hao 18, baadhi yao wamekuwa wakiendelea kujinasibisha kama bado ni wa idara hiyo.

Alisema idara imewatangaza hadharani ili kuisaidia jamii kuwatambua kwamba si watumishi wa Uhamiaji, hivyo ikitokea miongoni mwao akaendelea kujitambulisha, wachukue hatua ikiwamo kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Aliwataka watumishi hao kuwa ni Thobias Lyewe, Julieth Mrema, Nina Mliga, Loveness Wilson, Wilbard Ompapson, Salama Dilunga, Philbert Chaula, Mkombozi Chodri na Alfred Mrema.

Wengine ni Imakulata Mwakatika, Ramadhani Ally, Ritha Maganga, Jovin Mkuchu, Veronika Max, Angela Mwambwiga, Peter Bally, Elizabeth Kibinga, na Lucy Munyanga. Msemaji wa Uhamiaji, Ally Mtanda alisema, “Kuna shida inatokea kwa watu wengi kujitambulisha kuwa wanatoka Uhamiaji. Wanakwenda viwandani na maeneo mengine kisha kuwarubuni watu na kuchukua fedha.

“Wale kwa namna moja au nyingine walifukuzwa kazi na wengine wameacha wenyewe lakini wanaendelea kujitambulisha kuwa watumishi ndiyo maana tumeamua kutoa orodha ili wananchi wawatambue kwamba hawa si watumishi wetu na hatutahusika kwa lolote likitokea,” alisema. Nyongeza na Ibrahim Yamola.
Chanzo: Mwananchi.co.tz
Asante kwa hii, lakini kosa la kuwatangaza wote bado ni ukiukwaji wa haki za binaadamu.
P.
 
kwa upo upande wa wala rushwa? gazeti la Jamhuri ilitoa taarifa jinsi majamaa walivyopiga hela kupitia hiyo e-passport. inawezekana mamlaka imejithibitisha kuhusu rushwa waliyopokea. Badala ya kupongeza unaanza kuwatetea mafisadi.
Au unajinadi kwao ili uwe wakili wao watimuliwa
 
Kama wamefukuzwa kazi kwa nini umma usijulishwe? Au unataka waende mitaani na kuendelea kuwaibia watu kwa kigezo cha uhafisa uamiaji wakati wametimuliwa kazi? Hizi kazi zinagusa maisha ya watu ukiona hatua hii imefikiwa jua wahusika walishakili juu ya tuhuma zao kwa vinywa vyao.
 
kwa upo upande wa wala rushwa? gazeti la Jamhuri ilitoa taarifa jinsi majamaa walivyopiga hela kupitia hiyo e-passport. inawezekana mamlaka imejithibitisha kuhusu rushwa waliyopokea. Badala ya kupongeza unaanza kuwatetea mafisadi.
Au unajinadi kwao ili uwe wakili wao watimuliwa
Nadhani hujaelewa mada! Hao waliofukuzwa ni wafanyakazi wa chini tu, so huenda wamefukuzwa kwa kuhisiwa kuwa wao ndio wamewapa dondoo waandishi wa Jamhuri juu ya ufisadi huo!
 
kwa upo upande wa wala rushwa? gazeti la Jamhuri ilitoa taarifa jinsi majamaa walivyopiga hela kupitia hiyo e-passport. inawezekana mamlaka imejithibitisha kuhusu rushwa waliyopokea. Badala ya kupongeza unaanza kuwatetea mafisadi.
Au unajinadi kwao ili uwe wakili wao watimuliwa

Mkuu msome paskal vizur kauliza sababu ni nini za kuwekwa hadharani picha zao kama ni wala rushwa kwenye hilo gazeti zilipochapishwa hizo picha hiyo point ya wala rushwa wakihusishwa nayo ipo?
 
Back
Top Bottom