Gazeti la 'HabariLeo' na taarifa ya kifo cha Mh. Mtema

Nimepitia taarifa za kidogo cha mh. Mbunge Mtema, katika gazeti la habari leo si taarifa iliyopewa kipaumbele jambo ambalo nadhani si Sawa na hasa nikilinganisha na taarifa iliyopewa kipaumbele, taarifa ambayo haikuwa na uharaka wowote Kwani
1. Ni habari ya kawaida pamoja na yaliyoandikwa kuipa uzito. hapa nawakumbuka wastaafu wote hata walio vijijini.
2. Ni ya uchunguzi, so ingeelea kutafitiwa japo kwa leo, na ikaambatanishiwa na nyaraka kadhaa za utumishi wa umma zinazopelekea hali ngumu ya maisha kwa watumishi wasifanya ufisadi.
Kwa maoni yangu nashauri
1. Habari leo wajisahishe katika hili Kwani pamoja na mwelekeo wao kisiasi wakumbuke like ni gazeti la umma wa tz, linaendeshwa kwa kodi zetu, Kwani hata wasipouza litaendelea kuchapwa tu.
2. R. Mtema, marehemu sasa, Alikuwa mtanzania, Lakini mbunge wa JMT, hivyo ni msiba kitaifa, ni uungwana tukalia wote,
3. Ajali ile imechukua maisha ya watz wengine, Kama mlivyowahi jurist kipaumbele katika taarifa nyingine za aina hii, basi mngefanya vivyohivyo
4. Kofi zetu zinauma pamoja na madhira mnayotutendea nyie mlokabidhiwa dhamana ya utumishi wa umma.
Inasikitisha, mnaimba uzalendo, kuipenda nchi, kuwa wamoja ilihali ninyi mmejitenga na jamii ya watz. Naomba kwa hili tuwakumbushe Habari leo kwamba wamechemka.

Mkuu kuna gazeti lingine nalo la Majira limeamua kuandika wanachoita vita ya madaraka ndani ya chadema
 
Tusifanye mambo na kujudge kila kitu kwa hisia wakuu,hivi ni kweli lazima kila gazeti liipe habari ambayo magazeti mengine yameipa nafasi ya upendeleo?
Katika kutafakari kwa umakini saana utajua kuwa Habari Leo wako ok.Tatizo jingine nikuchanganya events and our emotions then kinachotokea hapo ni lawama na kushindwa kuwa objective katika kulaum au kutoa judgement sahii.REGIA MUNGU AKULAZE MAHARA PEMA.AMINA
 
Nyie Vijana wa JF: Msipende kukomalia siasa changa. Kuna hoja nzito iliyoandikwa kwenye Habari Leo. Ningetaka kuzungumzia au kuuliza kilichoandikwa kwamba Dereva wa gari marehemu Regia Mtema alikuwa na ulemavu wa mguu! This is very serious nijuavyo mimi walemavu wa miguu hawapewi leseni ya kuendesha gari ila wakiwa na gari maalum hupewa leseni for a specific use to easy there movement narudia mfumo wetu umeoza tena vibaya. Kwani leseni anayopewa mlemavu ni specific kutumia mjini tu na sio on a highway na pia haruhusiwi kubeba abiria. Nataka mamlaka iliyompatia marehemu Regia leseni ikiwa ni pamoja na TRA wote wajiuzulu. Kwanza nani alimruhusu as an amateur driver kubeba abiria tena 8. Huu ni upuuzi kwanza analipwa pesa kila mwezi za kuajiri dereva. We have a lot of un answered questions huyo dereva alikuwa wapi? This looks like a suicide mission why one with disability is allowed to recklessly drive a vehicle without a proper licence! Fine she is dead kinachobaki let us soberly learn this lesson and authorities have to take measures sio kukimbilia rambi rambi tu hazitatupunguzia hii road carnage. While driving from Dar to Chalinze professionals know when to overtake kuanzia Vikindu mpaka Vigwaza never attempt to overtake unless you can see 200 metres ahead clear don't forget to check your rear mirror for crazy drivers coming from behind!:A S 465:
 
Unamtusi marehemu unapata faida gani wewe? Huna hata huruma? Unajionyesha wewe ni mtupu katika mawazo yako.Endelea kusherehekea msiba wa wengine kwa sababu hujui kesho yako.
 
Sishangai kwa habari leo kufanya hivyo. Kwakuwa siku zote limejipambanua kwetu kama gazet la ccm na si gazeti la umma.

Majira nalo limeacha kuandika habari za msiba likaona litumie siku ya leo kuandika kuna mgogoro mkubwa wa madaraka chadema.Shame on them
 
Hata Hao Habari Leo Wangeandika wasingebadilisha Ukweli!! Kwani Yameshatokea!! Ila tunawakumbusha kuwa watambue kuwa hii ni safari ya watu watu!! Watu wanajifanya kudharau wakati wanapoona wanapumua kama kawaida ila hii ni safari ya kila Mja!!!
 
Mkuu afadhali Habari leo kuliko kilichoandikwa na gazeti la Majira
 
Unamtusi marehemu unapata faida gani wewe? Huna hata huruma? Unajionyesha wewe ni mtupu katika mawazo yako.Endelea kusherehekea msiba wa wengine kwa sababu hujui kesho yako.

Heri wewe uliyeumbwa ukiwa mtimilivu kuliko mwanadamu yeyote aliyezaliwa na mwanamke Utaishi milele!!
R.I.P Mbunge wetu Regia!! Tunaomba Mungu atupe Nguvu Tuweze Kusonga Mbele!! Amen!!
 
Molemo!
Una uelewa mdogo hoja niliyotoa yahitaji mawazo pevu kuijibu. Gari linapoendeshwa na amateur that is one of the motokeo. Nahoji ni kweli alikuwa na ulemavu wa mguu au la ? Then dereva wake alikuwa wapi! Kutokana na kwamba marehemu alikuwa na umri wa miaka 32 she is still young by implication hakuwa narudia hakuwa na uzoefu wa kuendesha gari kwenye highway.Cha pili ni utata wa leseni yake? The rest is history unaweza ukanitukana the way you like but nawaasa vijana mjifunze kujenga na kuchangia / kuchambua hoja. Gari kupinduka mara tano she was flying? Zile kona na humps zilizopo you don't stand a chance Kama unakwenda over 80mph! Hakuna cha siasa hapa CUF ,CCM , CHADEMA or democratic party we should look into facts hakuna conspiracy theory it's pure accident soma vizuri maelezo ya majeruhi? Hoja ya magazeti yanavyoweka story just ask the editor nadhani haina mjadala!:A S 465:
 
Hata Hao Habari Leo Wangeandika wasingebadilisha Ukweli!! Kwani Yameshatokea!! Ila tunawakumbusha kuwa watambue kuwa hii ni safari ya watu watu!! Watu wanajifanya kudharau wakati wanapoona wanapumua kama kawaida ila hii ni safari ya kila Mja!!!
Mkuu.....Si kwamba Habari Leo hawajaiandika habari ya kifo cha Regia,habari imeandikwa sema tatizo(kwa mujibu wa muanzisha thread) haijawekwa katika kipaumbele,yenyewe imewekwa ya pili katika kipaumbele na imewekwa na picha ya gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha mpendwa wetu Regia Dotto Mtema....

Habari yenyewe ni hii hapa chini:

Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu

Na Oscar Mbuza, Ruvu.

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Regia Mtema amekufa katika ajali ya gari iliyotokea saa 5:15 asubuhi jana.

Katika tukio hilo, Mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Landcruiser VX
(V8) lenye namba za usajili T 296 BSM, alipasuka kichwa na ubongo wake kutapakaa katika eneo la ajali mita chache kabla ya kulifikia Daraja la Ruvu kutokea Dar es Salaam.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta na
alipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kubiringita mara saba.

Mbaga alisema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, polisi walifika na kumkuta Mbunge huyo akiwa tayari amekufa huku akibubujikwa na damu nyingi kutokana na kichwa kupasuka huku ubongo ukiwa umemwagika ardhini.

"Askari walipofika kwanza walianza kuwakimbiza majeruhi Hospitali ya Tumbi, waliwachukua
kwanza majeruhi watano halafu baadaye wakawachukua wengine wawili na baadaye ndio tukafanya mpango wa kuondoa mwili wa marehemu eneo la tukio kuupeleka Hospitali ya
Tumbi," alisema Mbaga.

Alisema hata hivyo ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Mbunge huyo kuwa na ulemavu wa mguu na hivyo kuwa na mguu mmoja tu wa kushoto ambao alisema inadhaniwa ulimpa tabu katika kufanya uamuzi baada ya kutokea kwa lori hilo la mafuta mbele
yake.

"Kama mnavyojua pedeli za gari zipo upande wa kulia lakini yeye alikuwa anatumia mguu wa kushoto kwa hiyo inawezekana kutokana na mshituko wa kutokea gari mbele, alibabaika katika kuutumia mguu huo wa kushoto kufanya uamuzi na hivyo kusababisha gari kumshinda na kupinduka," alisema Mbaga.

Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mlandizi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Bondo alisema
mbunge huyo alikuwa na abiria wengine saba ndani ya gari hilo ambao ni wa familia yake na walikuwa wakielekea katika kijiji cha Mperamumbi katika Tarafa ya Ruvu kukagua mashamba.

Alisema muda mfupi baada ya ajali hiyo, gari la Mbunge huyo liliondolewa kutoka eneo la ajali ili kuepusha msururu wa magari katika eneo hilo.

"Sasa hivi nasubiri kufika kwa Kamati ya Bunge ambayo nimeambiwa itafika mahali hapa wakati wowote ili kuja kutembelea eneo la tukio," alisema Mkuu huyo wa Kituo cha Polisi cha Mlandizi.

Naye Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alithibitisha kutokea kwa kifo cha Mtema aliyekuwa mmoja wa wabunge 48 wa chama hicho na akakiri kuwa Chadema imepata pigo kubwa kutokana na msiba wa ghafla wa mbunge huyo akisema kuwa, mchango wake ulikuwa ukihitajika kwa chama na taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa, mipango ya mazishi ya marehemu ilikuwa inapangwa nyumbani kwa baba wa
marehemu, Estelatus Mtema, Tabata Chang'ombe, katika Manispaa ya Ilala na kwamba ratiba ya maziko itatolewa baada ya kukamilika kwa taratibu zilizotarajiwa kupangwa na familia ya marehemu, Ofisi ya Bunge na chama.

Kutokana na kifo hicho, salamu za rambirambi zimemiminika kwa Chadema na familia ya marehemu, zikiwamo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.

Katika salamu zake za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Rais Kikwete alisema amesikitishwa na kuhuzunishwa na habari za kifo cha mbunge huyo ambaye amepoteza maisha akiwa bado kijana na kwamba
pigo hilo siyo la Chadema pekee, bali ni kwa taifa zima.

"Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi habari za kifo cha Mheshimiwa Mtema katika ajali ya gari. Siyo kwamba ajali hii imechukua maisha ya kijana bali imelinyang'anya taifa mbunge hodari na kwa hakika, kifo chake siyo tu ni pigo kwa chama chako cha Chadema bali ni pigo kwa sote na kwa taifa letu kwa jumla. Nakutumia wewe binafsi, chama chako na wanachama wake salamu za dhati za moyo wangu kuomboleza kifo na msiba huu mkubwa."

"Napenda ujue kuwa niko nanyi katika msiba huu. Napenda vilevile uniwasilishie salamu zangu za rambirambi za dhati kabisa kwa wana-familia, ndugu na jamaa wa marehemu
Mheshimiwa Mtema. Wajulishe kuwa nimepokea habari hizo kwa uchungu mwingi na kuwa moyo wangu uko nao katika wakati huu mgumu wa maombolezo, " amesema Mheshimiwa Rais na kuongeza.

"Aidha, wajulishe kuwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, awajalie uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake. Naungana nawe, Mheshimiwa Mwenyekiti, na wanafamilia wa marehemu kumwomba Mwenyezi
Mungu aiweke pema roho ya Mheshimiwa Regia Mtema. Amen."

Naye John Nditi anaripoti kutoka Kilombero kuwa, wananchi wa mjini Ifakara na vitongoji vyake wamepokea taarifa za msiba huo kwa mshtuko mkubwa kufuatia taarifa ya kifo cha mbunge huyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini Ifakara, kwa majonzi baadhi ya wananchi walisema kuwa wana-Kilombero wamempoteza mbunge kijana na mchapakazi aliyewatumikia wananchi wake bila kujali jinsia na itikadi ya vyama vya siasa.

Baba mkubwa wa marehemu Bartholomew Mtemanyenja alisema walipata taarifa za ajali hiyo, na baadaye baba mzazi wa marehemu, Estelatus Mtema alithibitisha akiwa njiani kwenda eneo la tukio akitokea Kilombero ambako juzi alishiriki katika maziko ya mmoja wa madaktari wa Hospitali ya St. Francis.

"Tulipata taarifa mchana wa saa saba na nusu saa baadaye, baba yake mzazi aliamua kuondoka kwa kupanda magari tofauti kwenda eneo la tukio, lakini akiwa njiani alituarifu kuwa Regia amefariki dunia," alisema baba mkubwa.

Awali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Abdul Mteketa alisema amesikitishwa na kifo hicho na
kumwelezea marehemu kuwa ni kijana mdogo, na mchango wake ulikuwa bado unahitajika kwa
wananchi wa Kilombero na Taifa kwa ujumla.

Naye Katibu wa Mbunge, Mashaka Manjoti alisema kuwa Wilaya ya Kilombero na Chama chao kimepoteza mpigania maendeleo ya wananchi wanyonge wakiwemo na watumishi wa nyanja mbalimbali.

Historia ya marehemu ambaye mwaka 2006 alihitimu Shahada ya Sayansi ya Uchumi na Lishe katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Alizaliwa miaka 31 iliyopita na Aprili 21 mwaka huu angetimiza miaka 32. Alipata elimu ya Msingi katika Shule ya Msingi Mchikichini, Ilala kuanzia mwaka 1989 hadi 1995, huku elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne aliipata katika Shule ya Sekondari ya Forodhani kuanzia mwaka 1996 hadi 1999 zote za Dar es Salaam.

Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa katika Mchepuo wa Kemia, Biolojia na Lishe (CBN) mwaka 2000, lakini aliomba uhamisho ili kwenda Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bweni Machame, Moshi mkoani Kilimanjaro.
 
Bora habari leo! Channel ten ndio hawana mpango kabisa na hii habari ya kifo cha dada yetu! Wao wanonyesha habari nyingine kabisa! Kuna shida kubwa sana kwenye hivi vyombo vyetu vya habari!

Hivi hawaoni aibu? Watanzania wote wanasikitika wao wako kimya, hivi huko mtaani wanako ishi, wanakakijiji kao?
 
Nyie Vijana wa JF: Msipende kukomalia siasa changa. Kuna hoja nzito iliyoandikwa kwenye Habari Leo. Ningetaka kuzungumzia au kuuliza kilichoandikwa kwamba Dereva wa gari marehemu Regia Mtema alikuwa na ulemavu wa mguu! This is very serious nijuavyo mimi walemavu wa miguu hawapewi leseni ya kuendesha gari ila wakiwa na gari maalum hupewa leseni for a specific use to easy there movement narudia mfumo wetu umeoza tena vibaya. Kwani leseni anayopewa mlemavu ni specific kutumia mjini tu na sio on a highway na pia haruhusiwi kubeba abiria. Nataka mamlaka iliyompatia marehemu Regia leseni ikiwa ni pamoja na TRA wote wajiuzulu. Kwanza nani alimruhusu as an amateur driver kubeba abiria tena 8. Huu ni upuuzi kwanza analipwa pesa kila mwezi za kuajiri dereva. We have a lot of un answered questions huyo dereva alikuwa wapi? This looks like a suicide mission why one with disability is allowed to recklessly drive a vehicle without a proper licence! Fine she is dead kinachobaki let us soberly learn this lesson and authorities have to take measures sio kukimbilia rambi rambi tu hazitatupunguzia hii road carnage. While driving from Dar to Chalinze professionals know when to overtake kuanzia Vikindu mpaka Vigwaza never attempt to overtake unless you can see 200 metres ahead clear don't forget to check your rear mirror for crazy drivers coming from behind!:A S 465:

Uko sahihi mkuu umeona mbali sana.Naunga mkono hoja kwa aslimia 100
 
Molemo!
Una uelewa mdogo hoja niliyotoa yahitaji mawazo pevu kuijibu. Gari linapoendeshwa na amateur that is one of the motokeo. Nahoji ni kweli alikuwa na ulemavu wa mguu au la ? Then dereva wake alikuwa wapi! Kutokana na kwamba marehemu alikuwa na umri wa miaka 32 she is still young by implication hakuwa narudia hakuwa na uzoefu wa kuendesha gari kwenye highway.Cha pili ni utata wa leseni yake? The rest is history unaweza ukanitukana the way you like but nawaasa vijana mjifunze kujenga na kuchangia / kuchambua hoja. Gari kupinduka mara tano she was flying? Zile kona na humps zilizopo you don't stand a chance Kama unakwenda over 80mph! Hakuna cha siasa hapa CUF ,CCM , CHADEMA or democratic party we should look into facts hakuna conspiracy theory it's pure accident soma vizuri maelezo ya majeruhi? Hoja ya magazeti yanavyoweka story just ask the editor nadhani haina mjadala!:A S 465:

Post yako ya mwanzo umemtukana Marehemu.Kaa kimya kama huna cha kusema.Kuwa kwako CCM haina maana kumkashifu marehemu eti kwa nini aliendesha gari? Narudia tena wewe endelea lakini huijui kesho yako
 
Inasikitisha kwa gazeti hili hasa kwa tukio hili,lakini haishangazi kwa imekua kawaida ya gazeti hili kudharau na kutozipa umuhimu au kuzipindisha hoja za upinzani hasa CHADEMA hata kama zina uzito,ukweli na umuhimu katika taifa inasikitisha gazeti hili ambalo linaendeshwa na kodi zetu linatumika kama gazeti la CCM.Naimani kama gazeti hili lingefutiwa ruzuku mawili yanaweza kutokea 1.Kufa baada ya matoleo mawili na 2.Kujirekebisha na kuanza kuandika habari balanced kutokana na umuhimu wake na nafasi yake katika taifa na pia kufanya kazi kwa ushindani na ufanisi zaidi kama yalivyo magazeti mengi ambayo yamejipatia sifa na yanauzika kwa umakini wake,kama vile Rai Mwema, Mwananchi,Tanzania Daima,Nipashe,Majira kuyataja machache.Tatizo hili liko kwa vyombo vyote vya habari vinavyoendeshwa na serikali.Na hii inatokana na chama tawala mbali na mabadiliko ya mfumo wa vyama vingi vya kisiasa bado inashindwa kufahamu kua CCM na serikali ni vitu tofauti.CCMni chama cha kisiasa kama vilivyo vyama vingine wakati serikali na nchi ni yaWATANZANIA WOTE.
 
Nyie Vijana wa JF: Msipende kukomalia siasa changa. Kuna hoja nzito iliyoandikwa kwenye Habari Leo. Ningetaka kuzungumzia au kuuliza kilichoandikwa kwamba Dereva wa gari marehemu Regia Mtema alikuwa na ulemavu wa mguu! This is very serious nijuavyo mimi walemavu wa miguu hawapewi leseni ya kuendesha gari ila wakiwa na gari maalum hupewa leseni for a specific use to easy there movement narudia mfumo wetu umeoza tena vibaya. Kwani leseni anayopewa mlemavu ni specific kutumia mjini tu na sio on a highway na pia haruhusiwi kubeba abiria. Nataka mamlaka iliyompatia marehemu Regia leseni ikiwa ni pamoja na TRA wote wajiuzulu. Kwanza nani alimruhusu as an amateur driver kubeba abiria tena 8. Huu ni upuuzi kwanza analipwa pesa kila mwezi za kuajiri dereva. We have a lot of un answered questions huyo dereva alikuwa wapi? This looks like a suicide mission why one with disability is allowed to recklessly drive a vehicle without a proper licence! Fine she is dead kinachobaki let us soberly learn this lesson and authorities have to take measures sio kukimbilia rambi rambi tu hazitatupunguzia hii road carnage. While driving from Dar to Chalinze professionals know when to overtake kuanzia Vikindu mpaka Vigwaza never attempt to overtake unless you can see 200 metres ahead clear don't forget to check your rear mirror for crazy drivers coming from behind!:A S 465:

Haya ni maajabu, yaani watu wanafurahia kamanda kuondoka? Lugha ya kejeri kwenye msiba Haifai.
 
Back
Top Bottom