Gazeti la Habaril leo mnamnyanyapaa mtoto

pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
225
Ni kutokana na kichwa cha habari kuhusu mtoto aliyefingiwa ndani ya boksi huko Morogoro.

Katika harakati za kuifahamisha jamii kinachoendelea kwa sasa juu ya afya ya mtoto huyo, gazeti la habari leo wamempa jina kuwa ni 'Mtoto wa boksi' Je hii ni sawa?
=============================


Mtoto wa boksi' yupo Muhimbili


MTOTO mwenye umri wa miaka minne aliyefungiwa ndani ya boksi kwa zaidi na miaka mitatu mkoani Morogoro, amehamishiwa katika Hos- pitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi na tiba zaidi huku wataalamu wakikuna vichwa namna ya kumrudishia afya yake.

Imeelezwa jopo la madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ya binadamu wakiwemo wataalamu wa saikolojia, wanahitajika kwa ajili ya kumwezesha mtoto huyo mwenye ulemavu kuwa katika hali ya kawaida.

Aidha, pamoja na uhitaji wa jopo la wataalamu hao, mtoto huyo ambaye amelazwa katika wadi ya watoto, atahamishiwa katika wadi maalumu ya watoto wenye utapiamlo awe karibu na uangalizi wa lishe baada ya kubainika ana udhaifu mkubwa wa lishe.

Wakizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam kwa nyakati tofauti hospitalini hapo, Daktari Bingwa wa Watoto wa MNH, Dk Mwajuma Ah- mada alisema mtoto huyo hajazidiwa kuumwa.

Alisema walimpokea juzi usiku na hatua za awali zilizofanywa ni pamoja na kuchukua baadhi ya vipimo kwa ajili ya uchunguzi.

“Mtoto aliletwa hapa jana (juzi) usiku, baadhi ya vipimo vimechuku- liwa, vingine atafanyiwa leo (jana) ikiwa ni pamoja na kumfanyia huduma ya kum scan (kumwingiza kwenye mashine maalumu) mwili mzima ili tufahamu tatizo na tiba sahihi,” alisema Dk Ahmada.

Alisema huduma ya tiba kwa mtoto huyo siyo ya daktari bingwa mmoja bali inahitaji jopo la wataalamu waki- wemo wa mifupa, saikolojia, viungo na magonjwa mbalimbali ya binadamu kumsaidia mtoto huyo.

“Kwa sasa hatuwezi kusema lolote kubwa kuhusu mtoto huyo ndio kwanza kafika na ndiyo tuko kwenye hatua ya awali ya kuchukua vipimo, na leo atafanyiwa huduma ya kumulikwa mwili mzima ili tujue tunaanzia wapi”, alisema Dk Ahmada.

Alisema pamoja na kusubiri majibu ya vipimo, hatua wanayochukua ni ya kumhamishia kwenye wadi ya watoto wenye utapiamlo, ili kutibu maradhi hayo ambayo ndio yameonekana awali, kwani mtoto amekosa lishe na viru- tubisho muhimu vya awali.

Alifafanua, katika hatua hiyo ya awali, mtoto huyo atakuwa akipewa maziwa ya lishe na kuendelea na tiba ya dawa za kuua vijasumu kutokana na kusumbuliwa na vichomi.

Akizungumzia kwa ufupi ikiwa mtoto huyo anaweza kurejea katika hali ya kawaida kwa viungo kunyooka na kutembea, Dk Ahmada alisema pamoja na kusubiri majibu ya vipimo, lakini pia tiba ya mtoto inategemea zaidi historia ya mtoto mwenyewe.

Mlezi azungumza Kwa upande wake, mlezi wa mtoto huyo , Josephina Joel akizungumza na gazeti hili wadini hapo alisema mtoto anaendelea vizuri ingawa juzi alikuwa na homa.

Hata hivyo alisema imeshuka, na kwamba kadri siku zinavyosonga, anaona uchangamfu wa mtoto.

Mwandishi wa habari hizi, alizungumza na mtoto huyo katika mahojiano mafupi:

Mwandishi: Unaitwa nani mtoto mzuri?

Mtoto: Akataja jina lake

Mwandishi: Utakula nini?

Mtoto: Chipsi (viazi vya kukaanga)

Mwandishi: Njoo nikubebe

Mtoto: Sitaki naumia
 

Otorong'ong'o

JF-Expert Member
Aug 17, 2011
35,466
2,000
Inasikitisha sana...Nawapongeza Magic FM leo katika kipindi cha Magazeti hawakusoma kile kichwa cha Habari cha Gazeti la Habari leo...

Hivi kwanini CCM inapenda dhalilisha Watanzania...??
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,077
2,000
Wananyanyapaa wazazi wake, mbaya sana wanamnyanyapaa marehemu mama yake na huyo mtoto.Hii si busara habari leo walichokifanya.
 

pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
225
Ni kama ndiyo dasturi yetu watanzania; kutokujua madhara ya mambo mbalimbali.

Ndiyo sababu hata wananchi wengi kwa muda mrefu, tokea kuzuka kwa ugonjwa wa ukimwi, wamekuwa na uwoga wa kijitokeza kupima afya zao kwa kuogopa unyanyapaa, na wala sio kwa kuogopa kufa.

Ikiwa pia ni pamoja na wenje matatizo mbalimbali ya kimaumbile kutokuwekwa katika uwazi ili kuweza kupata msaada toka kwa jamii.

Huyu mtoto hadi anafariki jina lake mashuhuri lilikuwa ni 'Mtoto wa boksi'.

Ama angekuwa alifungiwa stoo, angeitwa 'Mtoto wa stoo'

ingekuwa kwenye gunia, ' Mtoto wa gunia'

ingekuwa kwenye choo, 'mtoto wa choo'.

Hivi ndivyo tulivyo wanaadamu kutokuthaminiana.

Home
Kauli ya mwisho ya ‘mtoto wa boksi’ - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Tanzania Daima


"Eeee Mwenyezi Mungu Uliye Mtukufu tunakuomba kama kuna kosa lolote alilifanya umsamehe na umpumzishe kwa amani kiumbe wako mtoto Nasra katika Pepo".
 

UNLOCK

JF-Expert Member
Mar 9, 2014
269
195
Ila kweli c kauli nzuri kabisa kumuita hivyo wange2mia jina lake 2 wa2 wangeelewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom