Gazeti la habari leo hacheni kufanya ugaidi wa habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la habari leo hacheni kufanya ugaidi wa habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lifeofmshaba, Apr 6, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MBUNGE mwingine wa Chadema, Tundu Lissu ameingia matatani baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kumtaka kuwasilisha uthibitisho wa madai kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema uongo, wakati alipojibu swali bungeni mjini Dodoma jana.

  Mbunge huyo wa Singida Mashariki alidai kuwa, Ngeleja ni muongo baada ya Waziri huyo kujibu swali la nyongeza lililogusa wananchi wa jimbo hilo ambako Kampuni ya Shanta Mining ina leseni ya utafiti wa dhahabu.

  Mbunge huyu akitumia Kanuni ya 63 (3) na 63 (4) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007 ya kutaka majibu, alidai kwamba, Waziri hakusema ukweli kuhusiana na sakata zima la wananchi wa Sambaru kuporwa maeneo yao na kujengwa uwanja wa ndege kwa nguvu bila kulipwa fidia.

  Kutokana na hali hiyo, Spika Makinda alimtaka Mbunge huyo kupeleka uthibitisho kwa sababu hawezi kuruhusu muda wa kipindi cha Maswali na Majibu kutumika kwa malumbano na kwamba, yeye ataamua.

  Katika kuhimiza hilo, alitolea mfano wa suala la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ambalo alisema sasa ndiyo litatolewa maamuzi.

  Lema alidai katika Mkutano wa Pili wa Bunge la 10, kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa ametoa kauli ya uongo bungeni kuhusu vurugu za kisiasa mkoani Arusha.

  Wakati mzozo huo ukiendelea bungeni, Spika Makinda wakati wa Mwongozo wake ili kuokoa muda wa maswali na majibu, aliwataka wabunge wanapokuwa na matatizo ya aina hiyo kutumia Kanuni za Kudumu za Bunge hasa ya 50 (1) inayompa nafasi mbunge kutoa wahaka wake kwa kumwandikia spika.

  Kifungu hicho kinampatia nafasi Mbunge kusema jambo lolote linalomhusu na lililofikia jamii na Mbunge anayetaka kusema atawasilisha kwa Spika na kupewa muda wa dakika 10 kuzungumza.

  Kutokana hali ilivyokuwa na hasa baada ya Lisu kutumia kifungu kinachotaka mambo kumalizika bungeni, Spika Makinda alimwagiza mbunge huyo kuwasilisha uthibitisho wake ifikapo Ijumaa ambapo kamati husika zitakaa na kujadili na yeye kutolea maamuzi kwa kutumia kifungu cha 63, kifungu kidogo cha 6.

  Spika alisema hakuna muda wa kulumbana katika kipindi cha maswali na majibu na hivyo kutaka mbunge athibitishe hoja yake hiyo na kuwasilisha Ofisi ya Spika kwa hatua zaidi.

  Katika majibu yake, Ngeleja alisema alishatembelea eneo hilo mwaka 2007 na si kweli kuwa limechukuliwa kwa nguvu.

  Alisema Sambaru ni eneo linalotamkwa kwa ajili ya kupata uelekeo wa eneo na kwamba kampuni hiyo inatekeleza kazi zake katika maeneo ambayo wamepewa kisheria na leseni.

  Lissu alidai kampuni hiyo imeshatwaa ardhi zinazomilikiwa na wananchi kwenye maeneo ya Kinyamberu, Taru na Sambaru na haijalipa fidia, wakati Ngeleja alisema kampuni husika kwa sasa inafanya upembuzi yakinifu ili kubaini idadi ya waathirika, kiwango cha athari na baadaye Serikali itatoa majibu.

  SOURCE HABARI LEO

  MY TAKE: wanaposema mbunge mwingine wa chadema yuko matatani ni kufanya ugaidi wa makusudi kwenye hii taaluma ya habari, habari leo wanajua kwamba LEMA alishawasisha ushahidi na spika kaukali maana, anajua yaliyoandika humo ni ya moto, tunajua nyie vi vipenzi wa ccm kila habari mnatafuta negetive ya chadema lakini hii mmechemsha na ninashauri chadema wawachukulia hatua kwa kukipaka matope chama maana hakuna mbunge aliyopo matatani
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Jembe na nyundo wako kazini
   
 3. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kweli kabisa wako kazini lakini sio jembe na nyundo hawajabadilisha tu ni knife and fork ndizo alama sitaili kwa hiki chama chetu mafisadi
   
 4. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Umejitakia mwenyewe nani kasema ulisome?, mimi niliacha kulisoma mda mrefu sasa hivyo kichwa changu kimepumzika kusoma upupu.
   
 5. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hata mimi niko kama wewe ndugu lakini mimi hizi habari nimeletewa na wenzetu ambao bado macho hayajaona nuru, hivi unajisikia je kama ndugu zako wanalishwa sumu na wewe huko pembeni umekaa kimya, hawa ni watu wa kupigiwa yowe ya mwizi ili wajue hatuwataki katika jamii, na kama tutahacha kusoma na kuwanyamazi, kunawenzetu wanamezwa na huu mto wa habari leo, ni busara kama umejua kitu kuwapa wenzio weledi, mimi nilipokuwa uk, walikuwa wanapiga vita wapotoshaji kama hawa kuliko kushabikia mambo mazuri ya gazeti la mwananchi,
  kuna kila sababu vita yetu uwamalize watu kama hao na sio kuwakimbia.
  la sivyo tutakwenda na kenge kwenye huu msafara wetu wa ukombozi wa nchi
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Tuko wengi sana tusiosoma huu upupu wa the so called mkumbwa sijuwi. Hivi mlishawahi kuuliza wanauza copies ngapi kwa toleo hawa jamaa? Ni aibu kwa kweli sitaki hata kuiweka hapa hiyo figure. Ila jamaa wana roho ngumu kweli walipaswa kuwa wamekwishaacha siku nyingi kuprint hiki kituko anyway ni kwa sababu linaendeshwa kwa ruzuku ya kodi zetu. I'm sure hata ccm ambao zimebaki kidogo kichwani hawasomi huu udaku otherwise copies za mauzo zingeongezeka japo kidogo.
   
 7. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sawa wewe hausomi lakini kuna watanzania wangapi wanapotezwa na haya magazeti?
  dawa ni kutosoma au kuwapiga vita kabisa watoke kwenye medani ya uandishi wa habari,
  mimi ninashokwambia ni hakika maana ndio sababu ya kuandika hapa kwa wana jamvi
  kuna asilimi kubwa ya watu bado wanasadiki haya magazeti, mengine tunajidanganya na ikifika wakati
  wa uchaguzi yaandika pumba na kuwa kikwazo kwa wagombea safi,
  kwa nini wazalendo tunapenda kutumia njia za kususa?
  anyway mimi sito wahacha na wala sito ogopa kujua pumba zao
  uwezi kupigana na adui unaye mdharau ndio maana wanashinda kila siku hawa kwa kukologa watu
  huu ni muda wa kukaba mpaka kivuli
   
Loading...