Gazeti la Dira: Kashfa ya kuhongwa - Zitto, Ole Sendeka, Sarah Msafiri na Anne Kilango watajwa

Zitto hakuhusika isipokuwa kuna shinikizo la kumuweka kwenye list ili kukidhi matakwa ya kisiasa.

Kosa la Zitto kwenye hii saga ni kutoa kauli mapema mno watu waka-tafsiri kuwa na maslahi Tanesco. Na kwa bahati mbaya, watu ambao wamekuwa wanamtetea wamejikita sana kugeuza mambo ili yaonekane kuna msukumo wa ukabila na udini, badala ya kupambana na tuhuma zenyewe.
 
Tunataka kauli kama hizi. Na tutafuatilia kuona kama wanachukua hizo hatua za nidhamu.

"Kiongozi mkuu wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema:

“Nalaani kitendo cha wabunge kuhusishwa na ufisadi hasa ikizingatiwa kwamba Chadema tumekuwa tukiupinga vikali. Tumekuwa tukipinga rushwa kwa sababu ndiyo inayoielekeza nchi pabaya… Chadema hatufumbii macho rushwa.”

Alisema tangu kuanza Bunge la 10, Chadema kimekuwa kikiona baadhi ya mambo yanayoendelea katika mhimili huo muhimu wa dola yamejaa walakini...

“Ndiyo maana sisi Chadema tumekuwa tukisema Bunge limepoteza mwelekeo.”

Alisema akiwa mtendaji mkuu wa chama, anasubiri taarifa kamili kutoka katika kikao cha wabunge wa chama hicho ili kuweka wazi majina ya wahusika na kisha kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu (CC) ambacho kitakaa na kuchukua hatua kali.

“Tunahitaji tupate maelezo ya kina... chama chetu hakikurupuki… Nasubiri taarifa ya kokasi ya chama. Katiba ya Chadema inatambua uwapo wa kikao cha wabunge wetu na kwa bahati nzuri, kiongozi wake mkuu ni Mwenyekiti wa Chadema (Freeman Mbowe) na katibu (David) Silinde ni mbunge wetu. Tunasubiri taarifa yao.”

Alisema Chadema kina kanuni ya kudhibiti rushwa hivyo, mbunge wake akitajwa miongoni mwa wanaohusishwa na rushwa, atawajibishwa kupitia kikao cha CC ya chama hicho.
 
Kosa la Zitto kwenye hii saga ni kutoa kauli mapema mno watu waka-tafsiri kuwa na maslahi Tanesco. Na kwa bahati mbaya, watu ambao wamekuwa wanamtetea wamejikita sana kugeuza mambo ili yaonekane kuna msukumo wa ukabila na udini, badala ya kupambana na tuhuma zenyewe.

FJM huwa nakufagilia sana na comment zako.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
dah kama zitto anahusika kweli,atakuwa ametu disappoint sana. au ndo maana siku za karibuni amekuwa mpole na mkimya sana kukosoa serikali.kumbe anaogopa watamlipua!!! makamada mlo mstari wa mbele msikate tamaa kwa hili,
 
Msimamo wa Chama ukikiukwa sio kosa la jinai.....Rushwa ni kosa la Jinai...Kula rushwa na kukiuka msimamo wa chama ni vitu viwili tofauti!
Kama unatambua hivyo,kwa nini Zitto kutoa maoni yake kuhusu "Urais" ndio kumnanga kiasi hicho hapa jamvini na hata chamani?Au huoni kuwa huu ni mwendelezo wa kumpaka tope Zitto tangu alipotoa msimamo wake juu ya urais? au hili ni kosa la jinai. By the way,una ushahidi gani kuwa katenda kosa hili la jinai,au kutoa mtazamo kuhusu kusimamimishwa kazi Mkurugenzi wa Tanesco ndio kosa la jinai? Toa evidence kuwa katenda kosa,vinginevyo hakuna jipya zaidi ni siasa majitaka tu!
 
kweli nyerere aliona mbali kwa kuweka ktk katiba umri wa kugombea urais uwe zaidi ya miaka 40: maana vishawishi ni vingi hasa rushwa kwa kijana kuvishinda!!
 
Toa ushahidi wa Zitto kumiliki hivyo ulivyotaja. Tabia ya Mtu mzima kusubiri watu wengine wafikiri kwa niaba yako haifai. Hizi siasa majitaka zitawafikisha wapi? Na utafaidika na nini kwa hizi siasa majitaka!

Endelea hivyo hivyo kusubiria ushaidi tu wenzako wananeemeka ukija kustuka washakuamisha hadi hapo unapokaa,we unafikiri nao hawana akili wafanye mambo kiwaziwazi?
 
Kama unatambua hivyo,kwa nini Zitto kutoa maoni yake kuhusu "Urais" ndio kumnanga kiasi hicho hapa jamvini na hata chamani?Au huoni kuwa huu ni mwendelezo wa kumpaka tope Zitto tangu alipotoa msimamo wake juu ya urais? au hili ni kosa la jinai. By the way,una ushahidi gani kuwa katenda kosa hili la jinai,au kutoa mtazamo kuhusu kusimamimishwa kazi Mkurugenzi wa Tanesco ndio kosa la jinai? Toa evidence kuwa katenda kosa,vinginevyo hakuna jipya zaidi ni siasa majitaka tu!

Chadema wameshawahi kutoa tamko kuhusu Zitto kutangaza kugombea uRais...zaidi ya wenzake kukana kilichoandikwa kwenye gazeti? Chadema imesema kwamba Zitto amechukua rushwa (mpaka utake watoe ushahidi)? Walichosema Chadema ni kuwa kama kuna mBunge wao atakayegundulika amekula rushwa basi atahadhibiwa kutokana na taratibu za chama ie. CC itamuadhibu!

Sioni uhusiano wa Zitto kutangaza kugombea uRais na hili tukio la ulaji rushwa, halikuzuliwa na Chadema...ni Prof Muhongo, na zamani Mkullo waliosema/zusha...kwa nini unawananga Chadema na hili?!
 
:spy: siamini sijui kwa nini? naona kama cinema hivi tena drive in halafu nimesimama morocco????!!!! siwaelewi kabisa
ghafla naanza kufikiria hakuna dhambi tena katika kuua!
mbaya mno! ninahasira siwezi kuandika kitu cha maana. mnisamehe kwa kweli naumia mno!
 
Huwa nasema kila Siku, hakuna mwaminifu wote tumeoza. Watu wanafiki sana sana. Wanayoongea mdomoni na kuwaza au Kuamini moyoni tofa bin uti....
Alilalamika sana Lawino, politicians are hypocrites.
 
Funguka basi dada yangu nikusaidie, maana yule ni ndugu yangu kabisa. Na mimi niliishamkataza kwamba haya mambo ya kulaumiwa laumiwa kila mara sipendagi vile!
msalimie bwana au nipm no yake tafadhali
 
Chadema wameshawahi kutoa tamko kuhusu Zitto kutangaza kugombea uRais...zaidi ya wenzake kukana kilichoandikwa kwenye gazeti? Chadema imesema kwamba Zitto amechukua rushwa (mpaka utake watoe ushahidi)? Walichosema Chadema ni kuwa kama kuna mBunge wao atakayegundulika amekula rushwa basi atahadhibiwa kutokana na taratibu za chama ie. CC itamuadhibu!

Sioni uhusiano wa Zitto kutangaza kugombea uRais na hili tukio la ulaji rushwa, halikuzuliwa na Chadema...ni Prof Muhongo, na zamani Mkullo waliosema/zusha...kwa nini unawananga Chadema na hili?!

Kauli ya Zitto kasema hivi,"yeyote akionesha ushahidi, chembe tu ya ushahidi, kwamba nimekula rushwa, sitasubiri a minute, nitawajibika ".
Sijui mwenzangu wewe hao wabunge wa Chadema waliosema Zitto kachukua rushwa wamesemea wapi hayo na lini,na wametoa evidence gani! Tujuze
 
Habari kuwa kuna wabunge wa upinzani wanaohusika kuihujumu TANESCO zimepokelewa kwa masikitiko makubwa sana na imewafanya wananchi wengi kukata tamaa. Kwa ufupi wananchi tulikuwa tunawaunga mkono vyama vya upinzani tukijua wana dhamira ya kuleta mabadiliko na hatimaye kuboresha maisha ya watanzania. Kinachoonekana kutokana na taarifa za Waziri Sospether Muhongo ni kwamba hakuna tofauti kati ya CCM na vyama vya upinzani kwani lengo lao ni moja tu kutumia rasilimali za watanzania kunufaisha matumbo yao na familia zao in the expense ya maumivu na matatizo ya watanzania. Hii ni dhambi kubwa. Binafsi nimebaki njia panda kuhusu kwa nani watanzania tuweke matumaini yetu kuhusu mustakabali wa maisha bora kwa kila mtanzania. Watanzania tunasalitiwa na viongozi waroho ambao kwa wananchi wanajidai kondoo kumbe ndani ni Mbwa mwitu wabaya. Kwa viongozi wa namna hii tusitarajie tena mabadiliko hata kama CCM tutaiondoa kwani tunafanya yale yale yanayotufanye tupigane usiku na mchana kukiondoa chama dhalimu CCM madarakani. Si mambo ya kufumbia macho kwa sababu ya ushabiki wa kichama bali kutumia jicho la pili kuona upande mwingine wa shilingi na kufanya maamuzi yatakayo rudisha heshima ya vyama vinavyohusika na hatimaye kurudisha matumaini kwa waTZ. Viongozi hawa watajwe hadharani na wapewe adhabu inayostahili na wasipewe tena nafasi ya kuongoza kwani wamekosa adabu na credibility. Hii haina tofauti na kuku kula vifaranga wake.
Mtaani kwangu watu wamebaki na maswali mengi kuliko majibu na yanatakiwa yapate majibu kutoka kwa viongozi hawa hawa kwani doa lililosababishwa na wahusika ni kubwa sana.

Naona una jitahidi kumtetea huyo mnafiki mkubwa this time his true colour imefahamika
 
Haya ndio maneo, sio kuwekana gizani. Tupatieni majina haraka ili tuwapige mawe! Wa kwanza kupigwa awe yule aliyetuuzia misumari kwa pauni 50,000. Wa pili awe yule aliyeuzia Tanesco matairi mabovu.

NB: Lazima tuthibitishe kuwa wanahusika.

Wakati tukisubiri kudhibitisha wamehusika na wizi, ulaji rushwa, ufisi, sorry ufisadi basi ni vema wakawekwa benchi na vyama vyao husika then uchunguzi uendelee wasimamishwa uanachama kwa muda na ubunge pia!!!
 
Zitto!? Sikubaliani na msimamo wake sometimes lakini hili la kula mlungula ngumu kuamini!
unaona kasingiziwa au hawezi kula rushwa?? umemsikia wapi Zitto kwa uwazi na nguvu nyingi akishambulia mafisadi kama wanavofanya akina slaa, kiwia, msigwa, lema,n.k???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom