wanaume wa tanzania ni wanafiki kwa kila kitu....hii nchi haitokaa iendelee hadi wanaume wote watoke madarakani....yanajivalia tu suti kichwani wizi mtupuhii nchi! bora kusiwe na rais wala serikali, ingewezekana tukajiongoza wenyewe! naitema puuuuuu!
Wako sita........i have a lot of information but am waiting for wrong news first
Habari kuwa kuna wabunge wa upinzani wanaohusika kuihujumu TANESCO zimepokelewa kwa masikitiko makubwa sana na imewafanya wananchi wengi kukata tamaa. Kwa ufupi wananchi tulikuwa tunawaunga mkono vyama vya upinzani tukijua wana dhamira ya kuleta mabadiliko na hatimaye kuboresha maisha ya watanzania. Kinachoonekana kutokana na taarifa za Waziri Sospether Muhongo ni kwamba hakuna tofauti kati ya CCM na vyama vya upinzani kwani lengo lao ni moja tu kutumia rasilimali za watanzania kunufaisha matumbo yao na familia zao in the expense ya maumivu na matatizo ya watanzania. Hii ni dhambi kubwa. Binafsi nimebaki njia panda kuhusu kwa nani watanzania tuweke matumaini yetu kuhusu mustakabali wa maisha bora kwa kila mtanzania. Watanzania tunasalitiwa na viongozi waroho ambao kwa wananchi wanajidai kondoo kumbe ndani ni Mbwa mwitu wabaya. Kwa viongozi wa namna hii tusitarajie tena mabadiliko hata kama CCM tutaiondoa kwani tunafanya yale yale yanayotufanye tupigane usiku na mchana kukiondoa chama dhalimu CCM madarakani. Si mambo ya kufumbia macho kwa sababu ya ushabiki wa kichama bali kutumia jicho la pili kuona upande mwingine wa shilingi na kufanya maamuzi yatakayo rudisha heshima ya vyama vinavyohusika na hatimaye kurudisha matumaini kwa waTZ. Viongozi hawa watajwe hadharani na wapewe adhabu inayostahili na wasipewe tena nafasi ya kuongoza kwani wamekosa adabu na credibility. Hii haina tofauti na kuku kula vifaranga wake.
Mtaani kwangu watu wamebaki na maswali mengi kuliko majibu na yanatakiwa yapate majibu kutoka kwa viongozi hawa hawa kwani doa lililosababishwa na wahusika ni kubwa sana.
km wako sita basi mwaga mkuu unaogopa nini na kwa nini usubiri tupate wrong news?.....je, kwenye list yako waliotajwa hapa wapo pia?
Gazeti la Dira la leo limewataja wabunge wanasadikiwa kulamba mlungula ambapo kwa mujibu wa gazeti hilo wamo Zitto kabwe ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wakutisha ikiwapo nyumba kadhaa na magari ya kifahari, wengine waliotajwa ni Ole Sendeka na Mama Kilango Malecela ambao ndiyo wapiga kekele wakubwa wa ufisadi kumbe usanii tu.
Kwaupande mwingine Katibu mkuu wa CDM Dr. Slaa amesema ikiwa itabaunika wabunge wake watakutwa na hatia watachukuliwa hatua kali za kichama.
Magazeti mengie yamesuasua kuwataja live eti 'majina yamehifadhiwa' safi sana gazeti la dira.
Lazima naye yumo. Si ulisikia hotuba yake ya msemaji wa kambi ya upinnzani, Wizara ya Nshati na madini.Mnyika mbona anarukwa?
Kwanini slaa ndio akurupuke kutoa matamko na sio mnyika mwenye wadifa huo kichama? kuelekea 2015 tutaona mengi
ni bahati mbaya wengi humu hamfahamu kinachoendelea...na wakifanikiwa mtayumba sana.
Gazeti la Dira la leo limewataja wabunge wanasadikiwa kulamba mlungula ambapo kwa mujibu wa gazeti hilo wamo Zitto kabwe ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wakutisha ikiwapo nyumba kadhaa na magari ya kifahari, wengine waliotajwa ni Ole Sendeka na Mama Kilango Malecela ambao ndiyo wapiga kekele wakubwa wa ufisadi kumbe usanii tu.
Kwaupande mwingine Katibu mkuu wa CDM Dr. Slaa amesema ikiwa itabaunika wabunge wake watakutwa na hatia watachukuliwa hatua kali za kichama.
Zitto!? Sikubaliani na msimamo wake sometimes lakini hili la kula mlungula ngumu kuamini!
Why are you waiting the wrong news? Be open, we want clear news from you if have it.Wako sita........i have a lot of information but am waiting for wrong news first
kuchukua sitting allowance si kosa kwani ni haki ya kila mbunge.Wataje na wabunge wa Chadema wanaochukua sitting allowance,nao ni wezi pia.