Gazeti la Dira: Kashfa ya kuhongwa - Zitto, Ole Sendeka, Sarah Msafiri na Anne Kilango watajwa

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,271
9,900
Gazeti la Dira la leo limewataja wabunge wanasadikiwa kulamba mlungula ambapo kwa mujibu wa gazeti hilo wamo Zitto kabwe ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wakutisha ikiwapo nyumba kadhaa na magari ya kifahari, wengine waliotajwa ni Ole Sendeka na Mama Kilango Malecela ambao ndiyo wapiga kekele wakubwa wa ufisadi kumbe usanii mtupu.

Kwaupande mwingine Katibu mkuu wa CDM Dr. Slaa amesema ikiwa itabainika wabunge wake walipokea rushwa hutua kali za kichama zitachukuliwa dhidi yao.

UPDATE
Baadaya Tindu Lisu kuongea na wanahabari jana na kutaja Wajumbe wa kamati za bunge waliohusika na kuchukuwa rushwa na kufanya biashara na Tanesco, Olesendeka amemtaka kwa kuomba muongozo kwa spika amruhusu amshitaki Lisu ali athibitishie mahakama ushiriki wakwe wa kuchukuwa shushwa,

Hata hivyo Spika amesema jambo hilo linafanyiwa kazi na kamati ya maadili hivyo Lisu ataitwa kuleta ushahidi wake kwa wale aliyowataja.
 
Magazeti mengie yamesuasua kuwataja live eti 'majina yamehifadhiwa' safi sana gazeti la dira.
 
Mimi nataka kuona mwisho wa hii saga maana hata Bunge lenyewe kuna wanafiki wengi hivyo itaathiri hatua kali za kuchukuliwa kwa wabunge waliochukua mlungula.
 
hizi taarifa zinazid kunifanya niikinai hii nchi...mungu tuokoe!!
 
kwanini tusianze na yule aliyewateua?
Haya ndio maneo, sio kuwekana gizani. Tupatieni majina haraka ili tuwapige mawe! Wa kwanza kupigwa awe yule aliyetuuzia misumari kwa pauni 50,000. Wa pili awe yule aliyeuzia Tanesco matairi mabovu.

NB: Lazima tuthibitishe kuwa wanahusika.
 
Habari kuwa kuna wabunge wa upinzani wanaohusika kuihujumu TANESCO zimepokelewa kwa masikitiko makubwa sana na imewafanya wananchi wengi kukata tamaa. Kwa ufupi wananchi tulikuwa tunawaunga mkono vyama vya upinzani tukijua wana dhamira ya kuleta mabadiliko na hatimaye kuboresha maisha ya watanzania. Kinachoonekana kutokana na taarifa za Waziri Sospether Muhongo ni kwamba hakuna tofauti kati ya CCM na vyama vya upinzani kwani lengo lao ni moja tu kutumia rasilimali za watanzania kunufaisha matumbo yao na familia zao in the expense ya maumivu na matatizo ya watanzania. Hii ni dhambi kubwa. Binafsi nimebaki njia panda kuhusu kwa nani watanzania tuweke matumaini yetu kuhusu mustakabali wa maisha bora kwa kila mtanzania. Watanzania tunasalitiwa na viongozi waroho ambao kwa wananchi wanajidai kondoo kumbe ndani ni Mbwa mwitu wabaya. Kwa viongozi wa namna hii tusitarajie tena mabadiliko hata kama CCM tutaiondoa kwani tunafanya yale yale yanayotufanye tupigane usiku na mchana kukiondoa chama dhalimu CCM madarakani. Si mambo ya kufumbia macho kwa sababu ya ushabiki wa kichama bali kutumia jicho la pili kuona upande mwingine wa shilingi na kufanya maamuzi yatakayo rudisha heshima ya vyama vinavyohusika na hatimaye kurudisha matumaini kwa waTZ. Viongozi hawa watajwe hadharani na wapewe adhabu inayostahili na wasipewe tena nafasi ya kuongoza kwani wamekosa adabu na credibility. Hii haina tofauti na kuku kula vifaranga wake.
Mtaani kwangu watu wamebaki na maswali mengi kuliko majibu na yanatakiwa yapate majibu kutoka kwa viongozi hawa hawa kwani doa lililosababishwa na wahusika ni kubwa sana.
 
wako sita........i have a lot of information but am waiting for wrong news first

km wako sita basi mwaga mkuu unaogopa nini na kwa nini usubiri tupate wrong news?.....je, kwenye list yako waliotajwa hapa wapo pia?
 
Haya ndio maneo, sio kuwekana gizani. Tupatieni majina haraka ili tuwapige mawe! Wa kwanza kupigwa awe yule aliyetuuzia misumari kwa pauni 50,000. Wa pili awe yule aliyeuzia Tanesco matairi mabovu.

NB: Lazima tuthibitishe kuwa wanahusika.

Wa tatu awe yule aliyesema wameagiza nguzo south africa wakacharge tanesco maelf ya madollar kumbe nguzo wamezitoa mufindi... Watu kama hawa hawana tofauti na jambazi anayevunja nyumba za watu
 
Nipo kwa hamu kumjua nani anapeleka nguzo za umeme za mbeya na iringa huko kenya halafu anazirudisha tena tanzania na kusema zimetoka south afrika...yaani huy akanunue risasi mwenyewe, mi nitakuja kumaliza!!

Wewe unanakitu cha kuongezea katika ufahamu wa rushwa hapa TZ. Hebu funguka vizuri mkuu.
 
hii nchi! bora kusiwe na rais wala serikali, ingewezekana tukajiongoza wenyewe! naitema puuuuuu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom