Gazeti la An-nuur lamuadhimisha Kleist Abdulwahid Sykes (1950 - 2017)

Huyu Niliyemquote kasema Marehemu ndie alikuwa mpigania uhuru asiyejulikana full stop i don't want more marumbano yasiyohitajika... ulitakiwa umuelekeze yeye. kuwa kazaliwa 1950 so hawezi kuwa mpigania uhuru au awe makini na anavyoandika visipotoshe watu ndio maana nakataa.

Mlaleo,
''Malumbano,'' si ''marumbano.''

Siku hizi R na L zinawapa shida watu wengi.
Wakati wetu walimu walikuwa wakali sana katika matamshi yote Kiswahili na Kiingereza.

Labda hilo gazeti na picha zinaweza likatufanya tukaelewana.

Hii picha ya juu kulia ni Kleist Sykes, mwandishi, Balozi Abbas Sykes, Sheikh Abdallah
Awadh
na Hussein Shebe.

Mwandishi ndiyo mwenye umri mdogo kupita wote na mwenye umri mkubwa zaidi ni Sheikh
Abdallah Awadh.

24296373_2551122764914071_9012549259415078798_n.jpg
 
Mzee wangu Mohamed Said, shikamoo. Naomba maoni yako huru kabisa kuhusu serikali yetu ya sasa, ni miaka 56 baada ya uhuru. Mchapakazi mpya tuliye naye ikulu ameshughulikiaje suala la ubaguzi uliokuwa ukilalamikiwa wa kidini tangu uhuru, hali ikoje sasa?
 
Historia ya Tanganyika itabaki kwamba Nyerere ndiye aliyetupatia uhuru maana kuna wengine walikua wanacheza bao pale jirani Lumumba nao wanajiita wapigania Uhuru
 
Historia ya Tanganyika itabaki kwamba Nyerere ndiye aliyetupatia uhuru maana kuna wengine walikua wanacheza bao pale jirani Lumumba nao wanajiita wapigania Uhuru
Mtochoro,
Angalia hapo chini:

KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
Mohamed Said January 24, 2015 0

DSCN1129.JPG

DSCN1159.JPG

Jengo Hili la African Asociation Lilijengwa kwa Kujitolea Kiongozi Akiwa Kleist Sykes
Hapa Ndipo Palipokuja Kuzaliwa TANU Mwaka 1954

DSCN1154.JPG

Msomaji nakuwekea hapa vipande kutoka Dictionary of African Biography (DAB) ambao ni mkusanyo kwa njia ya maandishi historia ya Waafrika walioacha alama katika maendeleo ya bara hili.

Huu ulikuwa mradi wa Oxford University Press (OUP) na Chuo Cha Harvard na ulichukua miaka kadhaa kukamilika.

Nilikuwa mmoja wa waandishi waliotakiwa kuwaandika baadhi ya Watanzania na Watanganyika waliofanya makubwa katika historia ya nchi yao. Mradi huu ulikuwa chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong wa Harvard na ulikusanya wanahistoria 500 kutoka Afrika na kwengineko.

Nilimshauri Prof. Akyeampong akate baadhi ya majina aliyoniletea ya Watanzania kwa kuwa kwa hakika hawakuwa na mchango wowote wa maana isipokuwa labda baadhi walipata kuwa na vyeo katika serikali uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961. Nilifanya hivi kwa makusudi kabisa kwa kujua kuwa waliokuwa madarakani hawakutaka hata kidogo historia ya kweli ya waliopogania uhuru wa Tanganyika ifahamike na kuthaminiwa. Hii sasa ikawa nafasi yangu ambayo lau kwa uchache ningeliweza kuiweka sawa historia ya kweli ya Tanganyika.

Mimi nilisahau kabisa kuhusu kazi hii na hata ilipochapwa mwaka 2011 ilinichukua miaka minne kuja kukumbuka na kuanza kufuatilia nini ilikuwa hatima ya ule mradi na hapo ndipo nilipoona hii Dictionary of African Biography katika mtandao.
OUP wametoa volume sita za kazi hii mwaka 2011.

Volume hizi sita zinauzwa USD 1300 na vilevile zinapatikana kwenye mtandao kwa ''subscribers.'' Nimeletewa kutoka School of African Studies, London ukurasa ulio na makala niliyoandika kuhusu maisha ya Kleist Sykes (1894 - 1949) nami nimeona itakuwa vyema kama nitaweka hapa vipande vipande ili wasomaji wasome kwa faida ya kuhifadhi kumbukumbu za wazee wetu.

Labda msomaji utataka kujua kwa nini nilichagua kuandika maisha ya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography.

Nimemchagua Kleist Sykes kwa sababu hizi kubwa:
  1. Kwanza alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Asociation mwaka 1929 na muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 akiwa katibu vilevile na kwa jinsi siasa za kiloloni zilivyokuwa wakati ule za ''wagawe uwatawale,'' yeye aliunganisha vyama hivi katika uongozi mmoja lau kama Al Jamiatul Islamiyya kilikuwa chama cha Waislam na wakati huo huo akaweza kuweka misingi ya kuwashirikisha Wakristo katika kupigania haki za Mwafrika wa Tanganyika katika African Association.
  2. Pili Kleist alifungua mlango wa Waislam wawe na shule zao wenyewe ili kukabiliana na shule za Wamishionari ambazo zilikuwa zikiwabatiza watoto wa Kiislam katika shule zao na hili liliwafanya wazazi wa Kiiislam kusita kuwapeleka watoto wao shule.
  3. Tatu katika kutimiza hili alianzisha shule ya Kiislam - Al Jamiatul Islamiyya Muslim School ambayo ilisomesha masomo ya kisekula na Qur'an. Inasemekana ilikuwa ndoto ya Kleist kuona Qur'an inasomeshwa kwanye madarasa juu ya madawati na wanafunzi wamekaa katika viti kama shule badala ya zile madras za asili ambazo watoto wanakaa chini katika majamvi. Nia yake ikiwa kuwa katika shule mtoto atapata yote mawili - elimu ya dini yake na masomo ya kisekula. Ndoto hii ya Kleist sasa si ndoto tena kwani shule za Kiislam nyingi zimeanzishwa nchini pote miaka mingi baada ya yeye kutangulia mbele ya haki zikisomesha Qur'an na masomo ya kisekula kwenye darasa moja na mwalimu akiwa kasimama mbele ya ubao.
  4. Jambo la nne ni lile la kuuweka wazi mlango wa TANU kwa Wakristo ambao wakati wa vuguvugu la kuanzisha African Association mwaka 1929 serikali iliwatisha wasijiunge na chama hicho. Hii inatokana na yeye kuwa na akina Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts katika uongozi wa African Association na kwa njia hii kujenga msingi wa umoja na ushirikiano kwa Waafrika wote bila kujali dini zao. TANU ilipokuja asisiwa na wanae Abdulwahid na Ally pamoja na wazalendo wengine mwaka 1954, hali ilikuwa haijabadilika lakini uongozi wa Waislam ndani ya TANU uliweka mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa TANU haivurugwi na hisia za Uislam kiasi cha kuwaweka pembeni ndugu zao Wakristo.
Hii ndiyo sababu ikawezekana Nyerere kuchaguliwa kuongoza TAA mwaka 1953 na TANU ilipokuja asisiwa mwaka 1954 watoto wake wawili, Abdulwahid na Ally wakiwa kati ya waasisi 17 kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika haikuwa tabu kwake yeye kukabidhiwa jukumu la kuwaunganisha Waafrika chini ya bendera moja ya kudai uhuru.

Itoshe tu safari ya kwanza ya TANU kujitangaza nje ya Dar es Salaam Nyerere aliifanya 1954 Morogoro akifuatana na Zuberi Mtemvu na nyingine ilikuwa 1955 Lindi akifuatana na Rajab Diwani na Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hizi ndizo sababu nne zilizonipelekea kuandika maisha ya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography.

Mtochoro,
Yako mengi tusimame hapa kwa sasa.
 
Mzee wangu Mohamed Said, shikamoo. Naomba maoni yako huru kabisa kuhusu serikali yetu ya sasa, ni miaka 56 baada ya uhuru. Mchapakazi mpya tuliye naye ikulu ameshughulikiaje suala la ubaguzi uliokuwa ukilalamikiwa wa kidini tangu uhuru, hali ikoje sasa?

Ralph,
Mimi ningependa nami nisome mawazo yako.
Kisha nami nikupe yangu,
 
Ralph,
Mimi ningeoenda nami nisome mawazo yako.
Kisha nami nikupe yangu,
Mimi siku zote nilipinga kuwa Nyerere hakuendeleza udini ulioachwa na wakoloni, na nilisapoti hoja zangu kwa ushahidi wa kitendo cha Nyerere kutaifisha shule za misheni ili wote wasome huko kwa uhuru bila kujali dini zao. Pia niliona kama Nyerere alijitahidi kuepuka udini, na hata tuhuma za udini zilipomfikia alijitahidi kuzifanyia kazi. Marais waliofuata hali kadhalika walifanya jitihada hiyo, Mzee Mwinyi japo mwenyewe mwislamu aliwarudishia wakristo baadhi ya shule zao zilizotaifishwa na Nyerere. Mzee Mkapa ndiye aliyewapa waislamu chuo cha Tanesco Morogoro kikawa chuo kikuu chao. Na wote, awamu ya kwanza hadi ya nne walijitahidi kuwa na serikali shirikishi isiyokuwa na sura ya udini, kwa mtazamo wangu. Lakini, kwa mshangao wangu pia, manung'uniko ya udini bado yalikuwepo katika awamu zote hizo.
Kilichonisababisha kutaka maoni yako ni kuwa, katika awamu hii, sijayasikia malalamiko yale ya udini tena. Je ni kwamba yamekwisha au hayasemwi? Kama yamekwisha tumpongeze mchapakazi wetu.
 
Tyler...
Sasa tatizo liko wapi?
Nani anakuzuia kutoa pongezi?
 
Mlaleo,
''Malumbano,'' si ''marumbano.''

Siku hizi R na L zinawapa shida watu wengi.
Wakati wetu walimu walikuwa wakali sana katika matamshi yote Kiswahili na Kiingereza.

Labda hilo gazeti na picha zinaweza likatufanya tukaelewana.

Hii picha ya juu kulia ni Kleist Sykes, mwandishi, Balozi Abbas Sykes, Sheikh Abdallah
Awadh
na Hussein Shebe.

Mwandishi ndiyo mwenye umri mdogo kupita wote na mwenye umri mkubwa zaidi ni Sheikh
Abdallah Awadh.

24296373_2551122764914071_9012549259415078798_n.jpg
Wewe wajifanya unajua lakini huna lolote kuna siku umeandika matusi humu leo unajifanya ati mtaalam wa R na L
 
Acha kuzuga umeona umeumbuliwa na ujuha wako ndio unajifanya kuchange gia angani,bwege tu wewe
Mimi huwa sikosei na wala siyumbshwi na hoja zangu sababu huwa zipo sawia... kusanya hoja ya kwanza hadi ya mwisho kisha mspmeshe mwenye akili ataelewa nimesimamia nini... niondolee viroja vyako hapa.
 
Wewe wajifanya unajua lakini huna lolote kuna siku umeandika matusi humu leo unajifanya ati mtaalam wa R na L
Mlaleo,
Mimi najua sijifanyi kujua.
Naweza nikakuthibitishia kuwa najua ikiwa utapenda.

R na L nazijua kwani nilipata Merit Pass First Class English Oral
Cambridge.

Sina sababu ya kumtukana mto yeyote hapa.
 
Mzee, nimesoma Kitabu chako chote cha Maisha na Nyakati za Abduwahid Sykes sijaona mahali ambapo wazee wako wa Kariakoo wanapigania Uhuru, wakiwa peke yao, ndio maana TAA iliitwa "Chama cha Starehe!"
Kazi ya "kupigania" uhuru hasa ilifanywa kwa uongozi shupavu wa baba yetu wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere (RIP), japokuwa wewe unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuwa sio wa dini yako!
Du kwenye udini tena, kweli...
 
Mlaleo,
Mimi najua sijifanyi kujua.
Naweza nikakuthibitishia kuwa najua ikiwa utapenda.

R na L nazijua kwani nilipata Merit Pass First Class English Oral
Cambridge.

Sina sababu ya kumtukana mto yeyote hapa.
Na kwenye kiswahili ulipataje maana umekimbilia Cambridge
 
Ninachoshangaa ni kuwa kipindi hiki ambako kuna ubaguzi wa wazi kabisa hakuna anayelalamika.
Ralph...
Popote panapo dhulma malalamiko yatakuwepo.
Huenda wewe huyaoni wala kuyahisi lakini hii haina maana kuwa hakuna malalamiko.
 
Back
Top Bottom