Gazeti la Amani na habari hizi za mzee wa upako zina ukweli

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,249
21,345
Nimepitia magazeti yote lakini nimeshangazwa na habari zilizopo kwenye gazeti hili leo 03 Nov 2016 kama zina ukweli wowote! Mwenye taarifa kamili atujuze; wasiwe wanatuchafulia mzee wetu bure; watu naimani zetu! Nimechoka kusikia Habari za kusemwa mzee wetu, mara mzee Wa upako amimina risasi hewani, mara mzee yule kafanya hivi; jamani huyu mzee muacheni atuhudumie waumini wake Tunaimani naye; kwenu kama anaonekana mbaya; lakini kwetu huyu mzee ni maraika; Mbali na neno tunajifunza sana ushauri wake. Muacheni atuhudumie!
WATASHINDANA LAKINI HAWATASHINDA
Screenshot_2016-11-03-06-14-13.png
 
Hilo ni gazeti la udaku we hujui. Mimi sijawahi kuamini chochote kutoka kwenye magazeti ya namna hiyo
 
Hilo ni gazeti la udaku we hujui. Mimi sijawahi kuamini chochote kutoka kwenye magazeti ya namna hiyo
Kwahiyo udaku umehalalishwa wapi kusema uongo? Kuna Katiba au sheria yoyote inayoruhusu gazeti la udaku kuongea kitu ambacho hakipo? Sheria ya makosa ya kimtandao na Habari inashughulikia makosa yepi na yepi haihusiki?
 
Sasa kama miaka yote wanaandika uongo na wanaachwa huoni kama wamehalalishwa kama si kuendekezwa
 
ni bora ukawauliza hao AMANI kuliko kuendelea na wewe kumtangaza huyo m w u.

mimi nilikuwa sijui ila nimejua baada ya wewe kupost hivyo na wewe hauko tofauti na AMANI.

jifunze kunyamaza
 
kaka hao waandishi ni hatari, wanajua kucheza na maneno, kama ukilisoma hilo gazeti ndani wanastail yao ambayo huwezi kumfungulia mashtaka wanacheza na maneno...ni vigumu sana kumpata ktk sheria maana kwanza ni gazeti la udaku, jiulize je udaku ni nini? udaku ni umbeya/ ama habari ambayo haijitosherezi/ taarifa isiyo rasmi na vitu kama hivyo, hapo mwandishi anaweza kusema tulipomtafuta muhusika kumuuziliza madai hapo kama ni kweli simuyake iliita bila kupokelewa/ ama alipopokea alishindwa kikataa ama kukubali, ama alikata simu baada ya kuulizwa, ama gazeti flani bado linamtafuta muhusika ajibu tuhuma hizo, sasa kukisha kuwa na vitu kama hivyo hapo tayari mwandishi kisha kubana na kama ulitafutwa kweli basi imekula kwako huwezi kushtaki popote, wajanja sana hawa jamaa, udaku ni tetesi tuu, ila kama ingekuwa ni yale magazeti makini sasa hapo kuna aina nyingine ya uandishi mjomba...sina taaluma ya habari ila hawa jamaa wanacheza na maneno.
 
Hii ni ukweli, ila sio jana wala juzi ni muda mrefu sana. Alisimulia mwenyewe katika mahubiri yake kama kuna mtu aliangalia katika Channel Ten wiki iliyopita, aliongea kuhusu hili
 
Hii habari hao watu wameitoa kwenye mahubiri yake yaliyorushwa wiki moja iliyopita channel ten, japo hakusema ubongo ulimwagika maana jamaa alipona. Pamoja na hayo siku akisimulia alisema HUYO JAMAA ALITOLEWA RIVER HADI MUHIMBILI NDANI YA DK 5 KWA GARI SIKU YA JUMA TATU TENA ASUBUHI SAA MOJA. Japo ninaamini miujiza ipo ila huo muujiza ilinipiga na butwaa kama kweli utoke River side ushike morogoro road, ukunjie fire au pale jangwani kwenda muhimbili ufike ndani ya dk tano siku ya juma tatu tena saa moja asubuhi. Je hiyo gari iliendeshwa kwa spidi gani? na je ni kweli kwa mazingira ya hizo barabara mbili hii inawezekana? Sijasema mzee wa upako alidanganya ila kwa akili zangu nimeshindwa kuitafuna.
 
Nimepitia magazeti yote lakini nimeshangazwa na habari zilizopo kwenye gazeti hili leo 03 Nov 2016 kama zina ukweli wowote! Mwenye taarifa kamili atujuze; wasiwe wanatuchafulia mzee wetu bure; watu naimani zetu! Nimechoka kusikia Habari za kusemwa mzee wetu, mara mzee Wa upako amimina risasi hewani, mara mzee yule kafanya hivi; jamani huyu mzee muacheni atuhudumie waumini wake Tunaimani naye; kwenu kama anaonekana mbaya; lakini kwetu huyu mzee ni maraika; Mbali na neno tunajifunza sana ushauri wake. Muacheni atuhudumie!
WATASHINDANA LAKINI HAWATASHINDA
View attachment 428510
mzee mi nimependa kujuaa tu aina ya simu yako manake hiyo miaplication hapo juu ni shida mpaka cnn,startimes we hatareee
 
Hiyo habari watakuwa wameitoa kwenye mahubiri yake,alisema mwenyewe Mzee wa Upako kuwa alimgonga mtu na alimuomba Mungu mtu huyo asife.
 
Ukitaka gazeti la Udaku lishtakiwe au kufungiwa na serikali basi liandike tu Habari mbaya dhidi ya Magufuli.
 
Ni kweli. Alisimulia mwenyewe na ni siku nyingi tu. Kipindi chake kilirudiwa kurushwa na Channel 10 saa 3.30 jana ucku. Kama huelewi bora kunyamaza kuliko kkurupuka!
 
Kweli Hilo Ni Udaku!! Sasa sifa ya uandishi Wa Habari Iko Wapi? UhAlisia Ni Kwamba Mze, Wa Upako Alikuwa Anatoa Ushuhuda Juu ya Matendo Makuu ya Mungu Jinsi ambavyo amekuwa Mtetezi Wake Maishani, akawa anashuhudia Jambo hilo Kipindi Kilefu Kilichopita Kwamba iliwahi nitokea Ajali, nikamgonga boda boda, yaani Ni Jambo LA Zamani, sio Leo, Hivyo ndivyo Tulivyomsikia Mtumishi Akishuhudia, Tena Jamaa mwenyewe Hakufa!! Sasa hawa wana jiha ribia Tu, Sifa ya Uandishi Wa Hbari.
Lakini Kuringana Na jina Lenyewe La Gazeti Huenda wakawa hawaoni Tatizo Kuwa wamekosea.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom