Gaza: Mashambulizi ya makombora yaendelea, Idadi ya vifo vya Wapalestina yafikia 122

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Mashambulizi ya maroketi yameendelea siku ya Ijumaa kati ya Israel na Palestina, huku idadi ya vifo na majeruhi pamoja na uharibifu wa mali vikiongezeka.

Israel imeendelea kufanya mashambulio katika ukanda wa Gaza ikipuuzia wito wa Jamii ya Kimataifa wa kusitisha mashambulizi, ikisababisha vifo vya jumla ya Wapalestina 122 wakiwamo watoto 31, huku wengine zaidi ya 900 wakijeruhiwa.

Waisraeli 6 na raia mmoja wa India wameripotiwa kuuawa katika mashambulio ya makombora kutoka upande wa Gaza, huku kukitajwa pia kuwapo kwa mzozo baina ya wakazi wa Kiyahudi na wale wa Kipalestina katika miji kadhaa ndani ya Israel.

Kundi la Hamas limetoa wito kwa Wapalestina kuandamana siku ya Ijumaa, wakati Shirika la Habari la Safa likiripoti kutokea kwa mvutano baina ya Wapalestina na Maafisa wa Polisi wa Israel katika mji wa Al-Bireh uliopo Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Maandamano yameripotiwa katika maeneo mengine pia ndani ya Israel.

1621006552543.png

Viongozi mbalimbali wameendelea kutoa wito wa pande zote kusitisha mashambulizi, akiwamo Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, anayezitaka pande zote “kukaa meza moja na kuyajadili.”

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ameelezwa kukasirishwa kwake na mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina na kutaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuleta suluhu.

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Fatou Bensuda ameliambia Shirika la Habari la Ruters kuwa wahusika wa pande zote mbili za mzozo wanaweza kukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita.

Amesema yupo tayari kuendelea na uchunguzi wake wa Uhalifu dhidi ya Binadamu hata bila ushirikiano wa Israel ambayo inaituhumu ofisi yake kwa ubaguzi dhidi ya Wayahudi na kukataa kusaini mkataba unaoipa mamlaka ofisi yake juu ya taifa hilo.

Chanzo: Al Jazeera
 
View attachment 1784732

Ukiangalia hivi vita ni wazi Wapalestina wanapitia wakati mgumu. Hamas ndio inawapa Israel uhalali wa kufanya uharibifu huu. Recep Ordegan katoa wito wa vita kusimama kwa sababu ni waislam wenzake wako taabani. Angekuwa ni mpenda amani asingeisaidia Azbeijan kupigana na Armenia.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom