Gavana BoT: Baada ya Arusha sasa ni Dar, hakuna haja ya kuwa na Bureau de change zaidi ya 100

Ila ni kweli, Bureau De Change ni kama duka la kawaida tu la kuuza na kununua hela za kigeni, ni kazi inayowezwa kufanywa na mabenki, kama ni siku za jmosi au j2 jioni au usiku, waweza kwenda kwenye mahoteli ya nyota tano ukauza na kununua unazohitaji....
Hakuna tatizo hapo...
 
G
Hata iweje haitakaa itokee ukafahamu mambo ya uchumi kuliko gavana wa bank.wewe jikite kwenye utalaam wako na stadi nyingine mambo ya uchumi waachie wenyewe.wakati mwingine Sio lazima kuongea unaweza kukaa kimya
Angalizo Governor anashauriwa na wachumi yeye ajui chochote kwenye uchumi ni mwanasheria by professional
 
Wewe ni kilaza kweli yaani unataka kutwambia kuwa ukipata kazi basi wewe ndiye msomi kuliko wengine?hujui kuwa kuna watu wamesoma haswa lkn wanafanya shughuli zao?
Wabongo we wateme ngeli,kuwa na maneno mengi Utawaskia wanasema jamaa ni very smart

Ova
 
Kumbe hata Arusha, issue ilikua sio kuna na vibari halali vya biashara, issue ni kuyapungza maduka, sijui lengo ni nini? KWanini basi asipunguze hata idadi ya mabenki!? Yaani unapunguza tax payers? Nchi hi buana, sasa raisi hapo hapo kwenye mkutano kasema wazi kabisa kwamba walipa kodi nchi ni wachache, wapo 2.2 milioni, TRA waongeze wazidi hapo, BOT yenyewe inapunguza, sielewi!
 
Huyu Gavana ni wa ajabu kabisa, kupunguza Bureau de Change haiwezi kuliongezea Taifa fedha za kigeni wala kuimarisha uchumi kwa kuongeza uzalishaji ,kuuza bidhaa /mazao nje ya nchi au nguvu ya shilingi kulingana na dola, euro. Bureau de Change kazi yao ni kutoa huduma kwa customers.
Nchi yoyote iliyo makini Bureau de Change zinadhibitiwa na hazifanyi kazi holela kama Tanzania. Unajuta viduka vingine vimekaa kiaina aina mpaka mtu unashindwa kuelewa biashara yao wanaendeshaje.
 
Enhee waendelee hivihivi na sera zao za hovyohvyo,ili biashara ya magendo ishike hatamu wajuvi tutumie fursa.
 
Mkuu huyo unaye muelekeza ni kati ya vijana waaliyomezeshwa CD ya kusifia serikali ya ccm kwa kila jambo hata kama ni baya
Hivi bado kuna walanguzu wa USD? Unafikiri kufunga Beauro de Change kutasaidia? Siku hizi kuna miamala kibao ya forex kwa mfano world remit na kadhalika na iko kimataifa sasa sijui itakuwaje
 
Ukiona hivyo ujue kuwa maji yamezidi unga na kimbilio pekee kwa jiwe ni jeshini
gavana anapaswa kuwa na weledi zaidi ya wataalamu wake, kupokea ushauri na kuchuja inahitaji uwe mbobezi kweli kweli wa mambo ya uchumi na sera za kifedha. Nakiri udhaifu mkubwa bado unajithidhirisha kwenye chombo kikubwa kama hiki, toka enzi za Nyerere walipambana na issue hizi ili hamna mwananchi aliewahi kuona wajeda wakizunguka nje ya maduka ya kuuza fedha ni ulimbukeni tu.
 
Bila mikopo hatuwezi kuishi hata kwa mwezi
Bnafc naona ni kukosa wapi tunakosea coz kinachoshusha dola sio dola kuna sabubu nyingi ikiwemo import and export, nafikili tungejikita katika vitu tunavyozalisha kuoeleka nje viende na value ya kushindana kimataifa alafu kupunguza kuagiza vitu nje kuliko unavyosindika nje, pia kitu kingine kupunguza mikopo hiyo ndo kabisa inatuua c Tz tu hata nchi zote km mnamikopo mikubwa uchumi hauwezi shindana kimataifa! Ni hayo tu
 
Hii ni hatari. Tunaanzaje kubana watu kufanya biashara? Itafika siku sasa tutasema hakuna haja ya kuwa na "show rooms' za magari kila baada ya mitaa miwili. Au Kariakoo tupunguze Hardwares maana zimekuwa nyingi mno. Hizo "BANK ZA KUTOSHA" acha zipambane tu na Bureau de Changes.
 
Jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe
Tatizo lenu ndio hili kufikiri hao wateuliwa wenu wanajua kila kitu.. Huyo Gavana wenu ambae ni mwanasheria atajulia wapi monetary policy and flow? Yani tutaendelea kudorora siku baada ya siku kwa style hizi za kupeleka lecturers kwenda kusimamia uchumi..Uchumi sio Lecture theatre au Dissertation nyie!
 
Ccm ni janga la taifa
Jamani kasema hao hawakuwa na leseni.kuwa gavana si lazima uwe mchumi rejeeni sheria.wachumi wengi wametumislead sana au nataka tutoe mifano ya wachumi waliotupeleka pabaya?wengine mpaka watueleza tulenyasi ili ndege zinunuliwe na zikanunuliwa mbovu.hivyo swala la elimu ya uchumi si material ktk issue hii ya bureau de change ni utashi tu wa kiakili.kwani waziri wa afya ni daktari,wa ardhi ni mtaalamu wa ardhi,tamisemi ni mtaalamu wa local gvt.jadilini mambo yenye mantiki na si ushabiki wa kisiasa.acheni siasa twendeni kwenye uhaliasia.siasa zinatupotezea muda sana tunatakia kuchukua hatua kama tunaona mambo hayaendi sawa.Learn from french.a last change in fuel price has brought a big difference.
 
Ccm imetufikisha pabaya
Kwanza hakuna haja ya kuwa na bureau de change kwenye miji ambako kuna matawi ya benki za biashara. Benki zifungue madirisha ya kubadilisha fedha tu ili kuwahudumia wateja. Wageni watumie ATM kwa kutumia kadi zao za VISA, MATERCARD, AMERICAN EXPRESS? UNION PAY nk. Mambo utakatishaji wa pesa yatakuwa historia.
 
Hata iweje haitakaa itokee ukafahamu mambo ya uchumi kuliko gavana wa bank.wewe jikite kwenye utalaam wako na stadi nyingine mambo ya uchumi waachie wenyewe.wakati mwingine Sio lazima kuongea unaweza kukaa kimya

Kwa hiyo tukimteua hata kinyozi kuwa Gavana wa BOT automatically atakuwa na ufahamu wa mambo ya uchumi?
 
Back
Top Bottom