Gavana BoT: Baada ya Arusha sasa ni Dar, hakuna haja ya kuwa na Bureau de change zaidi ya 100

Hata iweje haitakaa itokee ukafahamu mambo ya uchumi kuliko gavana wa bank.wewe jikite kwenye utalaam wako na stadi nyingine mambo ya uchumi waachie wenyewe.wakati mwingine Sio lazima kuongea unaweza kukaa kimya
Wewe ni kilaza kweli yaani unataka kutwambia kuwa ukipata kazi basi wewe ndiye msomi kuliko wengine?hujui kuwa kuna watu wamesoma haswa lkn wanafanya shughuli zao?
 
Viongozi wasiwe waoga wamwambie Rais ukweli kwanini uchumi wa nchi awamu hii ya 5 ya uongozi wa CCM unadumaa /kongoloka na sekta ya kifedha kuyumba
Hawawezi kumwambia ukweli kwakuwa wanajipendekeza na kuendelea kufanya hivyo ndiyo kuliangamiza taifa na sasa tunarudi enzi za miaka ya 80
 
hivi unafahamu malengo ya kuanzisha maduka ya kubadili fedha ilikua ni nini au ulikua shule?
Sababu hiyo haipo tena
Nendeni mkabadili pesa zenu benki na mkiweza fungueni kabisa akaunti za kigeni
Unakuta mtu ana akiba mpaka milioni 30 kwenye akaunti yake,lakini hana mawazo afungue akaunti ya kigeni aweke walau dola elfu mbili
Bwege wewe
 
Walanguzi wa usd wamepanic
Hivi bado kuna walanguzu wa USD? Unafikiri kufunga Beauro de Change kutasaidia? Siku hizi kuna miamala kibao ya forex kwa mfano world remit na kadhalika na iko kimataifa sasa sijui itakuwaje
 
Tatizo la Benki kwenye kubadili fedha za kigeni lipo hivi ukiwa na Dola wao watanunua dola yako kwa $1 = 2234 ila ukiwa na shillingi unataka dola wao watakuuzia $1= 2350 sasa mfanyabiashara gani atakubali huo ujinga wakati huo ukienda kwenye bureau de change ukitaka dola watakuuzia $ 1 = 2320 na ukiwa nazo dola wao watakuubadilishia kwa 2300 sasa nani mjinga akabadili fedha benki kwenye rates ndogo
Kwa mfanyabiashara una 1500$ na kuendelea ukienda bank unaomba special rate, ni utaratibu wa kawaida, mara nyingi inakua nzuri zaidi hata ya rates za bureau de change.
 
Kwa hiyo kwa mawazo yako pale ofisini kwa gavana maamuzi yote anafanya kwa akili yake
gavana anapaswa kuwa na weledi zaidi ya wataalamu wake, kupokea ushauri na kuchuja inahitaji uwe mbobezi kweli kweli wa mambo ya uchumi na sera za kifedha. Nakiri udhaifu mkubwa bado unajithidhirisha kwenye chombo kikubwa kama hiki, toka enzi za Nyerere walipambana na issue hizi ili hamna mwananchi aliewahi kuona wajeda wakizunguka nje ya maduka ya kuuza fedha ni ulimbukeni tu.
 
Bnafc naona ni kukosa wapi tunakosea coz kinachoshusha dola sio dola kuna sabubu nyingi ikiwemo import and export, nafikili tungejikita katika vitu tunavyozalisha kuoeleka nje viende na value ya kushindana kimataifa alafu kupunguza kuagiza vitu nje kuliko unavyosindika nje, pia kitu kingine kupunguza mikopo hiyo ndo kabisa inatuua c Tz tu hata nchi zote km mnamikopo mikubwa uchumi hauwezi shindana kimataifa! Ni hayo tu
 
Hata iweje haitakaa itokee ukafahamu mambo ya uchumi kuliko gavana wa bank.wewe jikite kwenye utalaam wako na stadi nyingine mambo ya uchumi waachie wenyewe.wakati mwingine Sio lazima kuongea unaweza kukaa kimya
Tatizo lenu ndio hili kufikiri hao wateuliwa wenu wanajua kila kitu.. Huyo Gavana wenu ambae ni mwanasheria atajulia wapi monetary policy and flow? Yani tutaendelea kudorora siku baada ya siku kwa style hizi za kupeleka lecturers kwenda kusimamia uchumi..Uchumi sio Lecture theatre au Dissertation nyie!
 
Isitoshe ni serikali ya jamhuri ya muungano ndio iliyotoa Leseni kwa hawa wadau wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni.

Jamani kasema hao hawakuwa na leseni.kuwa gavana si lazima uwe mchumi rejeeni sheria.wachumi wengi wametumislead sana au nataka tutoe mifano ya wachumi waliotupeleka pabaya?wengine mpaka watueleza tulenyasi ili ndege zinunuliwe na zikanunuliwa mbovu.hivyo swala la elimu ya uchumi si material ktk issue hii ya bureau de change ni utashi tu wa kiakili.kwani waziri wa afya ni daktari,wa ardhi ni mtaalamu wa ardhi,tamisemi ni mtaalamu wa local gvt.jadilini mambo yenye mantiki na si ushabiki wa kisiasa.acheni siasa twendeni kwenye uhaliasia.siasa zinatupotezea muda sana tunatakia kuchukua hatua kama tunaona mambo hayaendi sawa.Learn from french.a last change in fuel price has brought a big difference.
 
UDHIBITI WA BIASHARA YA FEDHA ZA KIGENI- Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema hakuna haja ya jiji la Dar es Salaam kuwa na maduka 100 ya kubadilisha fedha (Bureau de Change) na badala yake kuwa na maduka hayo mipakani na kwenye hoteli za kitalii.

--------
Mwezi uliopita, Benki kuu ya Tanzania (BoT) iliyafunga zaidi ya maduka 100 ya kubadili fedha jijini Arusha kwa kutokukidhi masharti ikiwemo kutokuwa na leseni halali za biashara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa BoT Profesa Florens Luoga amesema operesheni hiyo haitakoma, na huenda mji mkuu wa kibiashara Dar es Salaam ukafuata baada ya Arusha.

"Hatuhitaji maduka 100 ya kubadilisha fedha Dar es Salaam, kwani kuna benki za kutosha. Tunahitaji maduka ya fedha kwenye sehemu muhimu kama kwenye mahoteli ya kitalii na mipakani," amesema Luoga kwenye mkutano wa Rais John Magufuli na Wakuu wa Mikoa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

"Udhibiti utaendelea kuwa mkali. Hii ni moja ya hatua zitakazoendelea, kanuni ambazo zilikuwepo ziliongeza udanganyifu na maduka yakazidi kuongezeka kiholela," ameongeza Luoga.

Katika operesheni iliyofanyika Arusha mwezi uliopita BoT ilitumia askari kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kutumika kwa askari wa JWTZ kwenye msako huo kulishtua watu wengi na ikamlazimu Luoga kutoa ufafanuzi baadaye.

Kwa mujibu wa Luoga BoT ilitumia wanajeshi "kufuatia askari wengi wa Jeshi la Polisi kuwa katika usimamizi wa mitihani ya kidato cha pili," na taasisi yake ilihusisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wasio na silaha ili kuongeza nguvu katika kufanikisha zoezi hilo.

Kabla ya operesheni hiyo ya kushtukiza, kulishafanyika operesheni nyengine mbili za awali na maofisa wa BoT ambazo hazikuzaa matunda.

Wakati msako wa Arusha ukifanyika, thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ilikuwa imeshuka maradufu na kufikia Sh2,300 kwa dola moja. Mara ya mwisho kwa kiwango hicho kufikiwa ilikuwa Julai 2015 na BoT ililazimika kuchukua hatua mahususi kukabiliana na anguko hilo.

Kwa mujibu wa tovuti ya BoT dola moja ya Marekani kwa hii leo Sesemba kumi imekuwa ikibadilishwa kwa shilingi 2,290.

Wiki mbili zilizopita, BoT ilizipiga marufuku benki tano kuendesha biashara ya sarafu za kigeni kwa muda wa mwezi mmoja kwa kukiuka sharia.

Benki ya Barclays Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank zote zilipigwa marufuku ya kuendesha biashara hiyo Novemba 23 kwa kukiuka sheria za biashara, kwa mujibu wa Alexander Ng'winamila, mkurugenzi wa masoko ya fedha katika benki kuu.

"Benki zilizopigwa marufuku aidha zilifanya biashara nje ya viwango vya masoko au hazikuwasilisha kwa Benki Kuu rrekodi za biashara zao, suala ambalo ni kinyume na sheria," Ng'winamila aliliambia shirika la Reuters.

Chanzo: BBC

niko ulaya MADUKA ya pesa za kigeni MACHACHE SANA.. lakini bongo kama mama ntilie
 
Kwanza hakuna haja ya kuwa na bureau de change kwenye miji ambako kuna matawi ya benki za biashara. Benki zifungue madirisha ya kubadilisha fedha tu ili kuwahudumia wateja. Wageni watumie ATM kwa kutumia kadi zao za VISA, MATERCARD, AMERICAN EXPRESS? UNION PAY nk. Mambo utakatishaji wa pesa yatakuwa historia.
 
Back
Top Bottom