Gavana BoT: Baada ya Arusha sasa ni Dar, hakuna haja ya kuwa na Bureau de change zaidi ya 100

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
UDHIBITI WA BIASHARA YA FEDHA ZA KIGENI- Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema hakuna haja ya jiji la Dar es Salaam kuwa na maduka 100 ya kubadilisha fedha (Bureau de Change) na badala yake kuwa na maduka hayo mipakani na kwenye hoteli za kitalii.

--------
Mwezi uliopita, Benki kuu ya Tanzania (BoT) iliyafunga zaidi ya maduka 100 ya kubadili fedha jijini Arusha kwa kutokukidhi masharti ikiwemo kutokuwa na leseni halali za biashara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa BoT Profesa Florens Luoga amesema operesheni hiyo haitakoma, na huenda mji mkuu wa kibiashara Dar es Salaam ukafuata baada ya Arusha.

"Hatuhitaji maduka 100 ya kubadilisha fedha Dar es Salaam, kwani kuna benki za kutosha. Tunahitaji maduka ya fedha kwenye sehemu muhimu kama kwenye mahoteli ya kitalii na mipakani," amesema Luoga kwenye mkutano wa Rais John Magufuli na Wakuu wa Mikoa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

"Udhibiti utaendelea kuwa mkali. Hii ni moja ya hatua zitakazoendelea, kanuni ambazo zilikuwepo ziliongeza udanganyifu na maduka yakazidi kuongezeka kiholela," ameongeza Luoga.

Katika operesheni iliyofanyika Arusha mwezi uliopita BoT ilitumia askari kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kutumika kwa askari wa JWTZ kwenye msako huo kulishtua watu wengi na ikamlazimu Luoga kutoa ufafanuzi baadaye.

Kwa mujibu wa Luoga BoT ilitumia wanajeshi "kufuatia askari wengi wa Jeshi la Polisi kuwa katika usimamizi wa mitihani ya kidato cha pili," na taasisi yake ilihusisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wasio na silaha ili kuongeza nguvu katika kufanikisha zoezi hilo.

Kabla ya operesheni hiyo ya kushtukiza, kulishafanyika operesheni nyengine mbili za awali na maofisa wa BoT ambazo hazikuzaa matunda.

Wakati msako wa Arusha ukifanyika, thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ilikuwa imeshuka maradufu na kufikia Sh2,300 kwa dola moja. Mara ya mwisho kwa kiwango hicho kufikiwa ilikuwa Julai 2015 na BoT ililazimika kuchukua hatua mahususi kukabiliana na anguko hilo.

Kwa mujibu wa tovuti ya BoT dola moja ya Marekani kwa hii leo Sesemba kumi imekuwa ikibadilishwa kwa shilingi 2,290.

Wiki mbili zilizopita, BoT ilizipiga marufuku benki tano kuendesha biashara ya sarafu za kigeni kwa muda wa mwezi mmoja kwa kukiuka sharia.

Benki ya Barclays Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank zote zilipigwa marufuku ya kuendesha biashara hiyo Novemba 23 kwa kukiuka sheria za biashara, kwa mujibu wa Alexander Ng'winamila, mkurugenzi wa masoko ya fedha katika benki kuu.

"Benki zilizopigwa marufuku aidha zilifanya biashara nje ya viwango vya masoko au hazikuwasilisha kwa Benki Kuu rrekodi za biashara zao, suala ambalo ni kinyume na sheria," Ng'winamila aliliambia shirika la Reuters.

Chanzo: BBC
 
Huyu Gavana ni wa ajabu kabisa Bureau de Change haziwezi kuliongezea Taifa fedha za kigeni wala kuimarisha shilingi kulingana na dola, euro. Bureau de Change kazi yao ni kutoa huduma kwa customers.
Hata iweje haitakaa itokee ukafahamu mambo ya uchumi kuliko gavana wa bank.wewe jikite kwenye utalaam wako na stadi nyingine mambo ya uchumi waachie wenyewe.wakati mwingine Sio lazima kuongea unaweza kukaa kimya
 
Viongozi wasiwe waoga wamwambie Rais ukweli kwanini uchumi wa nchi awamu hii ya 5 ya uongozi wa CCM unadumaa /kongoloka na sekta ya kifedha kuyumba
"Hatuhitaji maduka 100 ya kubadilisha fedha Dar es Salaam, kwani kuna benki za kutosha. Tunahitaji maduka ya fedha kwenye sehemu muhimu kama kwenye mahoteli ya kitalii na mipakani," amesema Luoga kwenye mkutano wa Rais John Magufuli na Wakuu wa Mikoa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wengine waandamizi wa serikali.
 
Hata iweje haitakaa itokee ukafahamu mambo ya uchumi kuliko gavana wa bank.wewe jikite kwenye utalaam wako na stadi nyingine mambo ya uchumi waachie wenyewe.wakati mwingine Sio lazima kuongea unaweza kukaa kimya
huyo gavana mwenyewe ni lawyer, hana utaalamu wowote aliunga unga akapiga tax, hapo palifaa awekwe mbobezi wa monetary policy na awe huru asiingiliwe na jiwe
 
Huyu Gavana ni wa ajabu kabisa, kupunguza Bureau de Change haiwezi kuliongezea Taifa fedha za kigeni wala kuimarisha uchumi kwa kuongeza uzalishaji ,kuuza bidhaa /mazao nje ya nchi au nguvu ya shilingi kulingana na dola, euro. Bureau de Change kazi yao ni kutoa huduma kwa customers.
hivi unafahamu malengo ya kuanzisha maduka ya kubadili fedha ilikua ni nini au ulikua shule?
Sababu hiyo haipo tena
Nendeni mkabadili pesa zenu benki na mkiweza fungueni kabisa akaunti za kigeni
Unakuta mtu ana akiba mpaka milioni 30 kwenye akaunti yake,lakini hana mawazo afungue akaunti ya kigeni aweke walau dola elfu mbili
 
Ccm mgejitahidi kujifunza sio kila kitu mnabisha haya ila tu singeri wote tuta/tunaicheza.
 
Huyu Gavana ni wa ajabu kabisa, kupunguza Bureau de Change haiwezi kuliongezea Taifa fedha za kigeni wala kuimarisha uchumi kwa kuongeza uzalishaji ,kuuza bidhaa /mazao nje ya nchi au nguvu ya shilingi kulingana na dola, euro. Bureau de Change kazi yao ni kutoa huduma kwa customers.
Isitoshe ni serikali ya jamhuri ya muungano ndio iliyotoa Leseni kwa hawa wadau wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni.
 
Huyu Gavana ni wa ajabu kabisa, kupunguza Bureau de Change haiwezi kuliongezea Taifa fedha za kigeni wala kuimarisha uchumi kwa kuongeza uzalishaji ,kuuza bidhaa /mazao nje ya nchi au nguvu ya shilingi kulingana na dola, euro. Bureau de Change kazi yao ni kutoa huduma kwa customers.
Kwa hiyo ww unaelewa sana kuliko governor
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom