Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Florens Luoga abadilishwe haraka

Nasikitika sana kwa kushidwa kazi aliyopewa gavana wetu wa bank kuu Florens Luoga. Huyu gavana ni chaguo baya sana ambalo limewahi kutokea. Tujue tu kwamba huyu professor ni mwanasheria na sio mwana uchumi au mhasibu. Nashauri apewe Prof Mussa Assad kwa muda wa mpito.

Sababu moja ni kwamba bank kuu imepunguza riba za t-bills mpaka 7% kwa lengo la kupunguza mikopo ya bank za biashara ili ziwe 10%. Mara nyingi bank zina weka 2%-3% zaidi ya rate za bank kuu. Cha ajabu bank karibu zote zinatangaza riba za mikopo kuanzia 16% na utoaji wa mikopo ni riba za 21% kwa wenye hati za nyumba na mikopo mingine inaenda hadi 24%. Tusishangae banks zinaonyesha zinapata faida za ajabu wakati wakopaji wamepungua kutoka 24% mpaka chini ya 10%. Je hii ina maana gani

1. Ameshidwa kuongoza hizi bank au hajui kuziongoza. Hizi bank zime hakikisha zina marafiki serikalini na wakurugenzi wamekuwa na nguvu kuliko gavana wa bank kuu. Raisi alienda uingereza na mkurugenzi wa CRDB na sio gavana wa bank kuu. Hivyo imekuwa kama vile Professor hawezi hata kusimamia hizi bank .
2. Kuna miradi ya serikali wanachukuwa mikopo bank na ni wizi wa ajabu kama mradi wa serikali unachukuwa mkopo wa zaidi ya 10% kwa mwaka

Nitoe tu mfano nchi nyingine bank wanafanyaje US mfano bank kuu yao ina riba ya 2% na bank za biashara zinatoa mikopo kwa sasa ya 3%-5% yaani wanaongeza si zaidi ya 3% lakini tanzania bank ya biashara inaongeza kutoka 7% mpaka 21% ambayo ni ongezeko la 14%!!!. Hii maana yake ni kwamba biashara zisikotumia mikopo pesa nyingi ambazo zingetumia kuajiri wafanyakazi wapya, ununuzi na upanuaji wa biashara unasimama au unachukuwa muda mrefu. Hii inapunguza pesa kwenye mzunguko, inapunguza ajira na inakuwa vigumu kampuni zetu kushindana bila kuwa na pesa za mitaji.

Nchi zinazoendelea zina vitu vitatu vikubwa (1) Watu wanaojua kufanya kazi (2) Teknologia inayowezesha uzalishaji wa viwango na ufanisi (3) Upatikanaji wa mikopo nafuu. USA wasingekuwa na uchumi mkubwa kama mikopo ingekuwa 16%, 21% na 24%. Uchumi wa nchi hizi ungekuwa matatani sana sana. Sasa cha ajabu bank zinatoa mikopo ya 16%, 21% na 24% wa gavana kanyamaza tu!, waziri naye kanyamaza, Raisi naye kanyamaza!. Lakini vilevile Makamu wa Raisi Mpango anajua hili naye kanyamaza. Kwenye vitu muhimu kama hizi Rais, waziri na gavana waweke siasa na urafiki pembeni. Ni wafanya biashara wachache sana wanaweza kwenda kukopa nchi nyingine. Mo mfano ilibidi aende mpaka south Africa kukopa lakini wafanyabiashara wadogowadogo hawataweza kukuza biashara zao kwa riba hizi.

Lakini hata tukiacha yote hayo kwa kitendo cha Gavana wa bank kuu kushidwa kupunguza mikopo mpaka 10% kwa wafanyabiashara inatosha sana kumfukuza kazi. Waziri naye akishidwa kuongelea hili inabidi naye apishe wengine. Mwigulu ni mwana Ilboru mwenzangu lakini kama hili swala la riba halitapata ufumbuzi mapema inabidi aondolewe.

Zitto , Mwigulu Nchemba
Wivu tu unakusumbua.......
ukiona kuna mapungufu toa ushauri.....
unaposema atolewe manake nini!!?
si wivu wa kike huu!
 
Mtoa mada Pooote umepatia, lkn ulipomtaja ASSAD tu ndio umeteleza. Yule Bw.Mropokaji, Mtatata, Asiye siri, Ana Visasi na Vinyongo kibao. Kwa kifupi msiba wa Jiwe umefanya tuuujue Wasifu wa Viongozi wetu wengi akiwemo Assad. Huyu Bw.kazi pekee inamfaa akawe Mwalimu wa Madrassa au akarithi mikoba ya Maaalim Seif kule Zenjiber
Huyo jamaa ana hasira na Magu!!?
unfortunately Magu keshatangulia mbele za haki......
so amekosa mtu wa kuleteana nae mabifu
ameshikwa na 'mhaho'
 
Uzi mzuri sana nashangaa baadhi ya vilaza hapo juu wanataka kuharibu uzi.
Mjadala zaidi unahitajika kwny hii ishu ya riba za mabank hapa Tanzania.
Riba zikiongezwa manake serekali inataka ku control inflation/money supply kwenye uchumi.
ku discourage wakopaji wengi
 
BOT Kuna wachumi wameajiriwa hapo na ndio wanafanya briefing kwenye Board unless huelewi kwamba BOT ni Corporate body. Tafadhali tusibishane sana elewa unavyoelewa kama hujaelewa.

Gavana anakuwa kama governing person wa management tu, kazi zote za uchambuzi hufanyika kwenye idara husika mzee. That's how corporate world runs.

Na kwenye Board Kuna governing committees ambazo hupitia then humshauri Mwenyekiti wa Board. Hapo Gavana anakuwa ameshapewa briefing na management na huwepo kujibu kama issues zitaibuka na wao hurudi kuandaa majibu kupitia idara husika.

Gavana is just the same as CEO ajue management na lawyers they fit into that position worldwide accepted.
Umeeleza vizuri sana sasa kwa kichwa chenye akili ndogo kama cha mleta mada kinadhani Gavana anafanya kila kitu
 
Nasikitika sana kwa kushidwa kazi aliyopewa gavana wetu wa bank kuu Florens Luoga. Huyu gavana ni chaguo baya sana ambalo limewahi kutokea. Tujue tu kwamba huyu professor ni mwanasheria na sio mwana uchumi au mhasibu. Nashauri apewe Prof Mussa Assad kwa muda wa mpito.

Sababu moja ni kwamba bank kuu imepunguza riba za t-bills mpaka 7% kwa lengo la kupunguza mikopo ya bank za biashara ili ziwe 10%. Mara nyingi bank zina weka 2%-3% zaidi ya rate za bank kuu. Cha ajabu bank karibu zote zinatangaza riba za mikopo kuanzia 16% na utoaji wa mikopo ni riba za 21% kwa wenye hati za nyumba na mikopo mingine inaenda hadi 24%. Tusishangae banks zinaonyesha zinapata faida za ajabu wakati wakopaji wamepungua kutoka 24% mpaka chini ya 10%. Je hii ina maana gani

1. Ameshidwa kuongoza hizi bank au hajui kuziongoza. Hizi bank zime hakikisha zina marafiki serikalini na wakurugenzi wamekuwa na nguvu kuliko gavana wa bank kuu. Raisi alienda uingereza na mkurugenzi wa CRDB na sio gavana wa bank kuu. Hivyo imekuwa kama vile Professor hawezi hata kusimamia hizi bank .
2. Kuna miradi ya serikali wanachukuwa mikopo bank na ni wizi wa ajabu kama mradi wa serikali unachukuwa mkopo wa zaidi ya 10% kwa mwaka

Nitoe tu mfano nchi nyingine bank wanafanyaje US mfano bank kuu yao ina riba ya 2% na bank za biashara zinatoa mikopo kwa sasa ya 3%-5% yaani wanaongeza si zaidi ya 3% lakini tanzania bank ya biashara inaongeza kutoka 7% mpaka 21% ambayo ni ongezeko la 14%!!!. Hii maana yake ni kwamba biashara zisikotumia mikopo pesa nyingi ambazo zingetumia kuajiri wafanyakazi wapya, ununuzi na upanuaji wa biashara unasimama au unachukuwa muda mrefu. Hii inapunguza pesa kwenye mzunguko, inapunguza ajira na inakuwa vigumu kampuni zetu kushindana bila kuwa na pesa za mitaji.

Nchi zinazoendelea zina vitu vitatu vikubwa (1) Watu wanaojua kufanya kazi (2) Teknologia inayowezesha uzalishaji wa viwango na ufanisi (3) Upatikanaji wa mikopo nafuu. USA wasingekuwa na uchumi mkubwa kama mikopo ingekuwa 16%, 21% na 24%. Uchumi wa nchi hizi ungekuwa matatani sana sana. Sasa cha ajabu bank zinatoa mikopo ya 16%, 21% na 24% wa gavana kanyamaza tu!, waziri naye kanyamaza, Raisi naye kanyamaza!. Lakini vilevile Makamu wa Raisi Mpango anajua hili naye kanyamaza. Kwenye vitu muhimu kama hizi Rais, waziri na gavana waweke siasa na urafiki pembeni. Ni wafanya biashara wachache sana wanaweza kwenda kukopa nchi nyingine. Mo mfano ilibidi aende mpaka south Africa kukopa lakini wafanyabiashara wadogowadogo hawataweza kukuza biashara zao kwa riba hizi.

Lakini hata tukiacha yote hayo kwa kitendo cha Gavana wa bank kuu kushidwa kupunguza mikopo mpaka 10% kwa wafanyabiashara inatosha sana kumfukuza kazi. Waziri naye akishidwa kuongelea hili inabidi naye apishe wengine. Mwigulu ni mwana Ilboru mwenzangu lakini kama hili swala la riba halitapata ufumbuzi mapema inabidi aondolewe.

Zitto , Mwigulu Nchemba

Wewe mwanauchumi gani ambaye analinganisha nchi mbili zinazotofautina mbingu na ardhi kwenye vigezo vyote vya uchumi na mifumo ya kitaasisi. Yaani katika nchi zooote una draw examples from US..
 
Nimeona ametoa waraka kuwashugulikia maafisa wa benki wenye mikopo chechefu.

Huyu jamaa sasa naelewa ni kwa nini kipindi cha uteuzi wake waungwana walipinga sana.

Kama anashundwa kuelewa tu sababu zinazosababisha mikopo chechefu atawezaje kusimamia mustakabali wa uchumi wa nchi yetu.
 
Jamani huyo proffessor atolewe ni incompetent kuongoza benki kuu. Halafu ana dharau na roho mbaya sana anatesa saana wanafunzi wake wa research wakienda anawatupia karatasi usoni. Huyu prof ni mlevi mnooo duh hivi taarifa zake hawa viongozi wetu hawazipati jamani mbona tabia zake zinajulikana kila mahali.

kwenye ulevi hapo muache naye ale bata ndio starehe yake hiyo inayompa burudani..

Kwenye kutumia makaratasi usoni wanafunzi wake hapo sikubaliani naye ila hao wanafunzi nao mafala, siku mmoja naye wamtie vitasa tu na ukiulizwa unasema alikuwa ananipapasa anashika shika machine eti nimgonge....
 
Asante kwa uzi mzuri. Namkaribisha mtaalamu mwingine Naantombe Mushi atie nyama
Ngoja nichambue.. ntamwaga madini hapa

Mkuu nimesoma uzi na comments ila naona kuna falacies nyingi. Kuna hoja za msingi ndio ila kuna hoja nyingine inaonekana hazipo sahihi.. Itabidi kutulia niandike uzi kabisa lakini lazima nita address issues za mtoa mada
 
Ulevi gani wa kulewa kwa aibu wewe ukiwa kiongozi?
kwenye ulevi hapo muache naye ale bata ndio starehe yake hiyo inayompa burudani..

Kwenye kutumia makaratasi usoni wanafunzi wake hapo sikubaliani naye ila hao wanafunzi nao mafala, siku mmoja naye wamtie vitasa tu na ukiulizwa unasema alikuwa ananipapasa anashika shika machine eti nimgonge....
 
Kama ndo hivyo mmeifanya bot kuwa chombo kinachoweza kuendeshwa na yeyote hata na housegirl maana anakaa tuu kazi inafanywa na mgt na committes za bodi.
Sasa wewe naona unaongea vitu usivyovijua, Gavana ni mtu wa utawala tu. Na sehemu hiyo kwa taaluma yake, ni anastahili. Hizo kazi unazompa ahusiki nazo kabisa, kama ulikutana na magumu huko kwenye kukopa basi ilaumu serikali na sera zake na si yeye.

Hizo benki kunufaika ingekuwa ni kinyemela, basi hatua kubwa ingeshachukuliwa. Ila kama kumekaliwa kimya basi elewa serikali ina baraka zake huko, pia inanufaika kupitia kodi wanazozitoza kwa taasisi hizo. Kimaana nyingine nao ni wanufaika kwenye mafaidiko hayo. Jambo jingine la kujiongeza ni kuangalia na hizo benki zinatozwa vipi hivi sasa, ndiyo uje kuhitimisha na kusema wananufaika wao. Na si kukandamizwa ukimbilie kutoa uzi ukiishia kulaumu.

Hebu jaribu kutumia akili yako pia, unawezaje kujua hili wewe wa huku chini na wao wasifahamu lolote lile. Umelionea kwenye ramli?
Haiwezekani hii, wana data za kutosha kuliko wewe. Ukiona hivyo ujiongeze tu, usilaumu asiyehusika na kumpendekeza mtu kisa mtazamo wa kisiasa.

B.O.T haijiendeshi kihuni hadi ifikie kujiwekea tu taratibu zake, bali ni kwa sera maalum za serikali. Gavana hawezi kuhusika hapo kwani hapangi yeye hayo mambo, ni kiongozi pekee kulingana na taaluma yake ya sheria ndiyo anafaa kuwa kiongozi. Watu wa uchumi sehemu hizi za uongozi si wazuri sana, labda watu wa waliyobobea kwenye Business administration.
 
Hujielewi wewe governor ni mwenyekiti wa vikao vikao vikubwa vinavyofanya maamuzi mfano mgt na bodi. Sasa propasal fulani ya sera za uchumi inaletwa kikao cha mgt yeye kama chair na ulewa wake mdogo wa uchumi hawezi kupinga au kuwarekebisha kwa chochote kazi yake kuangalia tuu upepo unaendaje halafu maamuzi yanafanywa kirahisi hivyo. Proposal inaenda bodi yeye ni chair kunakuwa hajuna mabadiliko. Mnaona hii ni sawa tuùuu lol!
Now you are coming to my premise, CEO hajui hata business trend yeye pia ana washauri (consultants) ukiacha waajiriwa wa kwenye management ambao nao ni wataalamu.

You don't have to be a professional wa uchumi kuweza kuongoza bank as long unajua banking business au umekulia kwenye any business. You can manage a business as long una utaalamu wa management ya biashara so inategemea ni aina gani una utaalamu nayo hata kama sio mtaalamu that's why wasomi wote na utaalamu wa business administration au management au any other na wengine hawana hata elimu Ila wanakuwa CEO wazuri sana .

Nakupa mfano wa matajiri wa malori na mabasi au mahoteli, unamjua marehemu mzee Mfugale alikuwa owner na CEO wa Peacock Hotels? Yule mzee ni standard seven Ila aliweza kujenga Mali kutoka kwenye umoja wake akaingia kwenye mabasi ya Kwacha na baadae akaondoka akahamia kwenye biashara ya leisure na akafanikiwa sana mpaka kifo chake . Alimuajiri mwanae ambae alikuwa anafanya UN bwana Vitus Mfugale kama mkurugenzi mkuu na akamlipa same amount ya mshahara wa UN Ila ni mwanae na akawatosa wanae wengine but simply hakutaka waingie kwenye biashara yake lakini walibaki kwenye supply na Mambo mengine wakisubiri urithi tu. Alikuwa anatumia utaalamu wa Vitus tena lately sio wakati anachuma hela.

So haihitaji kuwa mtaalamu wa hiyo sekta ili uweze kuongoza uongozi ni kitu kingine otherwise hata Rais angekuwa anasomea Urais
 
Hujielewi utendalo kama huyo prof
Sio kazi yake hiyo.. CEO wa Toyota amezaliwa ukoo wa Toyota ila hajui hata engine inatengenezwaje na wala balance sheet inatengenezwaje ila ndie bosi wa Toyota dunia nzima. Gavana wa Bot sio kazi yake.. idara husika itazisoma hizo balance sheet na kumwelekeza
 
Wanasheria naona imewauma sana lakini gavana kawa angusha sana bank kuu sio siasa. Huyu mzee amepwaya sana kama mikopo isikofika 10% akapumzike tu . Hata kimei kasema riba zinatakiwa kuwa chini sasa haina ubishi. Isiposhuka tutahakikisha anatoka kwa manufaa ya nchi.
 
Kama ni rahisi hivyo pelekeni hata std 7 akawe governor. Hivi huelewi kuwa governor kazi yake kubwa ni ni ku- govern bot sasa anagovern nini ikiwa hana uelewa na abc za fedha na uchumi?
Now you are coming to my premise, CEO hajui hata business trend yeye pia ana washauri (consultants) ukiacha waajiriwa wa kwenye management ambao nao ni wataalamu.

You don't have to be a professional wa uchumi kuweza kuongoza bank as long unajua banking business au umekulia kwenye any business. You can manage a business as long una utaalamu wa management ya biashara so inategemea ni aina gani una utaalamu nayo hata kama sio mtaalamu that's why wasomi wote na utaalamu wa business administration au management au any other na wengine hawana hata elimu Ila wanakuwa CEO wazuri sana .

Nakupa mfano wa matajiri wa malori na mabasi au mahoteli, unamjua marehemu mzee Mfugale alikuwa owner na CEO wa Peacock Hotels? Yule mzee ni standard seven Ila aliweza kujenga Mali kutoka kwenye umoja wake akaingia kwenye mabasi ya Kwacha na baadae akaondoka akahamia kwenye biashara ya leisure na akafanikiwa sana mpaka kifo chake . Alimuajiri mwanae ambae alikuwa anafanya UN bwana Vitus Mfugale kama mkurugenzi mkuu na akamlipa same amount ya mshahara wa UN Ila ni mwanae na akawatosa wanae wengine but simply hakutaka waingie kwenye biashara yake lakini walibaki kwenye supply na Mambo mengine wakisubiri urithi tu. Alikuwa anatumia utaalamu wa Vitus tena lately sio wakati anachuma hela.

So haihitaji kuwa mtaalamu wa hiyo sekta ili uweze kuongoza uongozi ni kitu kingine otherwise hata Rais angekuwa anasomea Urais
 
Ww jamaa inaonesha umeshikwa pabaya na huyu gavana na unatetea mkate wako usichukuliwe!!!
 
Hapa ndo naona umuhimu wa kiongozi dikiteta........maana ni kutangaza tu BOT imepunguza riba kwa mabanki, Serikali inatangaza kuanzia sasa riba za mabalenki kwa wananchi izisidi 10&.
Benki itakayokaidi itaongezewa riba na BOT.
Au nasema uongo ndugu zangu!!!
 
Back
Top Bottom