Gavana Luoga akitoa takwimu za mchango wa kanda ya ziwa kwenye uchumi wa Tanzania

Tanzania bhana ni vituko tu.Sasa hivi mheshimiwa magu kaondoka hata viongozi wengine wameanza kupumuapumua sa sijui hawakuwepo kipindi hicho!!
 
Gawana Luoga ametoa takwimu za mchango wa kanda ya Ziwa kwenye uchaguzi wa Tanzania.

Mwaka 2019, kanda ya ziwa ilichangia Trilioni 34 kwenye uchumi wa Tanzania sawa na 25.9% ya pato la Taifa.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 90% ya dhahabu Tanzania.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 50% ya pamba na kahawa inayouzwa nje ya nchi.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 95% ya mauzo ya samaki ndani na nje ya nchi.

Kanda ya ziwa inavutia zaidi ya 80% ya watalii ama mapato ya utalii Tanzania. Kwa maana kwamba Serengeti national park hutembelewa na zaidi ya 80% ya watalii wanaokuja Tanzania. Bila Serengeti utalii Tanzania ni kama haupo. Bila Serengeti wazungu tutaishia kuwaona kwenye tv.

Mwisho na kwa umuhimu wa wanasiasa, kanda ya ziwa ina wapiga kura wengi kuliko kanda yoyote ile Tanzania. Kanda ya ziwa ina determine urais wa nchi hii hivyo wanasiasa chagueni maneno na kauli zenu kuhusu watu wa kanda ya ziwa.


Kwa bahati mbaya sana umeamua kuifanya mada yako iwe ya kisiasa zaidi, tena ya kufarakanisha waTanzania kwa mistari yako hiyo ya mwisho.

Gavana wa Benki Kuu hawezi kuweka maneno kama hayo uliyoweka wewe.

Kwa hiyo wewe ni mtu wa Kanda ya Ziwa zaidi, kuliko ulivyo mTanzania, au siyo!

Kesho na keshokutwa utatuhimiza watu wa kanda hii tujiondoe Tanzania kwa vile mchango wetu ni mkubwa?

Mada yako inabomoa, kwa nini usihimize kujenga zaidi!
 
wachaga buana!
Bangi na ushamba vinakusumbua msukuma mwenzangu!

Ulifanikiwa kuona majina yaliyopo kwenye phonebook ya Samsung yako unapotumiwa SMS?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ujinga kuamini wingi wa watu utawasaidia kushinda uchaguzi wakati ukweli ni kwamba hali ya maisha ya watu ndio itakayoamua nani mshindi.
Hata mkiwa kabila moja kama hali ya Maisha ni ya kimasikini hakuna mtu ataendelea kukubeba kisa kabila moja.
Ccm waangalie wananchi wa chini wawawezeshe watoke kwenye umasikini wa miaka sitini ya uhuru waache kutegemea wingi wa kanda ya ziwa wakidhan watawabeba Kila siku.
 
Kua na wapigakura wengi sio necessarily mgombea lazima atoke kwao ila wao wanaweza kudetermine mshindi.

Na tunakoelekea tutaamza kutoa hata wagombea maana tukitoa mgombea na tukaungana kumpigia kura anashinda urais asubuhi na mapema.
Hivi 16% inaweza kumtoa mshindi? Tatizo hamuelewa hata kinachomaanishwa. Kanda ya Ziwa ina wapiga kura wengi zaidi kuliko kanda nyingine, lakini pekee yao, kura zao zote, hazitoshi kumtoa mshindi.
 
Mleta mada anapaswa kutambua tu, kufanikiwa kisiasa kunategemea namna gani unavyoweza kuja na hoja zenye ushawishi kwa watanzania wengi pasipo kuwagawa kikabila au kikanda.

Magufuli na genge lake chafu lililazimisha hoja za kuwagawa watanzania kama nguzo ya kuendelea kuwatawala watanzania.
 
Mbowe alitakiwa kukaa kimya inawezakana maendeleo ya kaskazini yametoka kanda ya ziwa halafu na wao kanda ya ziwa waamke patakalika kweli?
 
Usiwe mjinga wewe nguzo ipi? Yaani mikoa 6 inachangia only 26% ya GDP afu unasema nguzo? Una akili timamu kweli wewe
Soma hoja yangu kwa umakini. Ni kweli Akili zangu kamwe haziwezi kulingana na zako kwa lugha uliyotumia. Rudi kijiweni ulikozoea.
 
Kua na wapigakura wengi sio necessarily mgombea lazima atoke kwao ila wao wanaweza kudetermine mshindi.

Na tunakoelekea tutaamza kutoa hata wagombea maana tukitoa mgombea na tukaungana kumpigia kura anashinda urais asubuhi na mapema.
Mawazo ya ajabu sana mnavyofanya hivyo na ubaguzi wenu na MEKO kanda zingine zitakuwa dhidi yenu kwa pamoja hamtaweza huo ujinga wenu mnaojidanganya
 
Bangi na ushamba zinakusumbua msukuma mwenzangu!

Ulifanikiwa kuona majina yaliyopo kwenye phonebook ya Samsung yako unapotumiwa SMS?


Sent using Jamii Forums mobile app
Mie ni wa shamba kweli, mbona hata huko Kilimanjaro ni mashamba tupu!
 
Hakika nchi hii watu akili hazifikiri inavyotakiwa. Sehemu kuwa na idadi kubwa ya watu ni hatari kubwa.

Iangalieni hiyo kanda ya ziwa mnayoisema, oneni maisha ya watu wake, na tazameni takwimu za umasukini Tanzania.

Halafu mtu anakuja anasema, eti kanda ya ziwa ina watu wengi wa kuamua kiongozi wa nchi, akili gani hii!

Nani alikuambia watu masikini wanaweza kuamua nani awe kiongozi?

Licha ya kuwa kanda ya ziwa ina rasilimali zote muhimu, nini kimefanyika kubadili maisha ya watu?

Au wingi wa watu kanda ya ziwa umeleta mabadiliko gani katika kuamua huo mnaouita uongozi wa nchi?

Tuielimishe jamii ya kanda ya ziwa kuna ujinga mkubwa, ili tuokoe na tulete ustawi wa watu. Sio hizo ngonjela zenu zinazoangamiza watu.
 
Kua na wapigakura wengi sio necessarily mgombea lazima atoke kwao ila wao wanaweza kudetermine mshindi.

Na tunakoelekea tutaamza kutoa hata wagombea maana tukitoa mgombea na tukaungana kumpigia kura anashinda urais asubuhi na mapema.

Unadhani wote wanaakili ya kijinga kama yako ya kuchagua mtu ki kabila?
 
Uwe unasoma machapisho ya serikali kuongeza ufahamu. Mambo ya uchumi hayalinganishwi kwa jinsi unavyofikiri wewe, yanalinganishwa kwa facts and figures.

Kanda ya pwani ama Dar es Salaam inachangia 40% ya uchumi, kanda ya Ziwa 26%, nyingine zilizobaki fanya hesabu mwenyewe kisha uone kama una akili ama huna.
Opportunity Cost soma hiyo, una lingine?!
Naona ulibadili ID tu lakini akili iko vilevile.
 
Mbowe alitakiwa kukaa kimya inawezakana maendeleo ya kaskazini yametoka kanda ya ziwa halafu na wao kanda ya ziwa waamke patakalika kweli?

Mikoa yenu ina eneo kubwa na watu wengi lakini inaongoza kwa umaskini na uvivu. Mtamchangia nani maendeleo. Angalia ni mikoa gani ina shule nyingi na nani waliozijenga. Ndo utajua wenzenu wamewekeza wapi. Halafu angalia mikoa gani ina mambo ya kishirikina sana, wanaua albino na vikongwe.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom