Gavana Luoga akitoa takwimu za mchango wa kanda ya ziwa kwenye uchumi wa Tanzania

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Gavana Luoga ametoa takwimu za mchango wa kanda ya Ziwa kwenye uchaguzi wa Tanzania.

Mwaka 2019, kanda ya ziwa ilichangia Trilioni 34 kwenye uchumi wa Tanzania sawa na 25.9% ya pato la Taifa.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 90% ya dhahabu Tanzania.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 50% ya pamba na kahawa inayouzwa nje ya nchi.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 95% ya mauzo ya samaki ndani na nje ya nchi.

Kanda ya ziwa inavutia zaidi ya 80% ya watalii ama mapato ya utalii Tanzania. Kwa maana kwamba Serengeti national park hutembelewa na zaidi ya 80% ya watalii wanaokuja Tanzania. Bila Serengeti utalii Tanzania ni kama haupo. Bila Serengeti wazungu tutaishia kuwaona kwenye tv.

Mwisho na kwa umuhimu wa wanasiasa, kanda ya ziwa ina wapiga kura wengi kuliko kanda yoyote ile Tanzania. Kanda ya ziwa ina determine urais wa nchi hii hivyo wanasiasa chagueni maneno na kauli zenu kuhusu watu wa kanda ya ziwa.

Tuwe makini na kauli zetu japo ukweli unabaki Kanda ya Ziwa ndio nguzo ya Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi nchini japo kimaendeleo hailingani na Kanda ya Kaskazini. Nachelea kueleza kwa vipi nguvu ya awali ya upinzani ilikuwa Kanda ya Ziwa
 
Prof Luoga anatosha BoT ? Maana alikuwa bingwa kupika data za urongo ....tumpe muda atupe majibu....muda mwalimu mzuri
 
Gawana Luoga ametoa takwimu za mchango wa kanda ya Ziwa kwenye uchaguzi wa Tanzania.

Mwaka 2019, kanda ya ziwa ilichangia Trilioni 34 kwenye uchumi wa Tanzania sawa na 25.9% ya pato la Taifa.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 90% ya dhahabu Tanzania.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 50% ya pamba na kahawa inayouzwa nje ya nchi.

Kanda ya ziwa inazalisha zaidi ya 95% ya mauzo ya samaki ndani na nje ya nchi.

Kanda ya ziwa inavutia zaidi ya 80% ya watalii ama mapato ya utalii Tanzania. Kwa maana kwamba Serengeti national park hutembelewa na zaidi ya 80% ya watalii wanaokuja Tanzania. Bila Serengeti utalii Tanzania ni kama haupo. Bila Serengeti wazungu tutaishia kuwaona kwenye tv.

Mwisho na kwa umuhimu wa wanasiasa, kanda ya ziwa ina wapiga kura wengi kuliko kanda yoyote ile Tanzania. Kanda ya ziwa ina determine urais wa nchi hii hivyo wanasiasa chagueni maneno na kauli zenu kuhusu watu wa kanda ya ziwa.

Kamanda imhotep huu ndio ukweli.
 
Kama wanawapiga kura wengi imekuwaje miaka yote wagombea hawatoki kwao?
Unataka kutisha watu kwa kigezo cha ukanda yaani kosa afanye mmoja uwahisishe kanda nzima?
Alifanya madudu na atapondwa kwa madudu yake.
Kua na wapigakura wengi sio necessarily mgombea lazima atoke kwao ila wao wanaweza kudetermine mshindi.

Na tunakoelekea tutaamza kutoa hata wagombea maana tukitoa mgombea na tukaungana kumpigia kura anashinda urais asubuhi na mapema.
 
Wakuu tunapozungumzia masuala ya ki kanda si mbaya ila inategemea tunayazungumzaje kimantiki.

Kwa ufaham wangu wa kawaida kanda kubwa kigeografia inaweza kuwa ni kanda ya ziwa na ndo kanda yenye mikoa nyingi. Kama vile Mara, simihu, Mwanza,kagera, shinyanga,Geita,..

Tukuzungumzia Rasilimali watu kanda yenye watu wengi vilivile ni kanda ya ziwa.

Kiuchumi bado ina rasilimali nyingi ku -compare na zone nyingine kwanza kuna Maziwa yakutosha, mapori yenye mashamba yenye mbolea za kutosha. Vile vle kuna kila aina ya madini ikiwemo dhahabu kwa asilimia kubwa.
Kwa ujumla ni kanda iliyo barikiwa sana.
Ila tukirudi kwenye umoja ni vyema tukautanguliza uzalendo wa nchi kwanza pasipo kuangalia ukanda upi ni bora kuliko upi.
 
Yaani mikoa yenye 16% ya population inachangia 26% tu ya GDP?

Hizi ni Takwimu za kuonesha umaskini uliotopea kwa watu wa huko badala ya kujisifia.

Hata ukiangalia Takwimu za mkoa mmja mmja kutoka NBS ,lake zone ni vichekesho yaani mikoa kibao inazidiwa na Mbeya na Njombe
 
Kama wanawapiga kura wengi imekuwaje miaka yote wagombea hawatoki kwao?
Unataka kutisha watu kwa kigezo cha ukanda yaani kosa afanye mmoja uwahisishe kanda nzima?
Alifanya madudu na atapondwa kwa madudu yake.
Yaani Wana watu 16% tuu kiasi kwamba hata wakijichagua hawawezi kutoa Rais kamwe kwa kura hizo
 
Tuwe makini na kauli zetu japo ukweli unabaki Kanda ya Ziwa ndio nguzo ya Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi nchini japo kimaendeleo hailingani na Kanda ya Kaskazini. Nachelea kueleza kwa vipi nguvu ya awali ya upinzani ilikuwa Kanda ya Ziwa
Usiwe mjinga wewe nguzo ipi? Yaani mikoa 6 inachangia only 26% ya GDP afu unasema nguzo? Una akili timamu kweli wewe
 
Back
Top Bottom