Gavana BoT: Nchi haiweki rehani Watu wake inapochukua Mikopo

Kuna vitu ni vigumu. kujibu moja kwa moja, kwenye umma.... ethics lazima hizingatiwe,
ila hangetakiwa kujibu kwa mfano inayoendana na ualisia wa swali.....masharti yapo. Ila hayana impact kwenye Rasilimali tulizo nazo nchini...
Mfano kuna miradi ambayo ni white elephant. Kimsingi hata wawezeshaji wanazikodolea macho kwambo usipo zimalza mkopaji hamekwisha ni lazima wazibinafishe.. .
 
miluzi mingi sana...kila mtu anajua, kila mtu ni serikali, kila mtu waziri, kila mtu Rais, kila mtu mbunge, kila mtu PM...kila mtu mwanasiasa...
 
Hawawezi kujibu..mana hao nao wapo wananufaika na mfumo wa wizi na ufisadi wa mali za wananchi wa lipa kodi wa nchi hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
"Unapokopa mkopo hukopi kwa ajili ya kula unakopa kwa ajili ya kufanya project ambazo zitaendelea kuzalisha na kwasababu unaendelea kuzalisha uhimilivu wako wa deni unaendelea kuwa mzuri sio kwamba deni linapanda" Gavana Benki Kuu Tanzania, Profesa Florens Luoga

"Katika kamati mnaangalia madeni yenu yasiuze nchi ndio maana nchi haiwezi ikaweka rehani watu au rasilimali zake na itahakikisha inazitumia ili kuhakikisha Serikali inaendelea kupata kipato" Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga

"Ukitumia pesa za ndani peke yake utapandisha kodi, utawafanya wananchi wachangie kwa njia nyingine ambayo ni gharama na itachukua muda mrefu. Badala ya kutengeneza mradi kwa miaka 3/4 utautekeleza kwa miaka 20 kwa sababu unategemea uchukue pesa za ndani" - Profesa Florens Luoga


PowerBreakFast
Masharti ya mikopo ya WB na IMF yanajulikana.
Mara nyingi ni structural changes ambazo lazima zilenge mashirika makubwa ya serikali, utumishi katika sekta ya umma, pension na hisa za serikali katika mashirika makubwa yenye hisa za serikali.
Mfano; Unaweza ukaambiwa binafsisha bandari, serikali iwe regulator tu.
Binafsisha shirika lote la umeme, serikali ibaki regulator tu.
Binafsisha Posta, Reli, Shirika la ndege, hospitali na hata vyuo vikuu.
Kuandika katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, kuanzisha aina fulani ya wizara kwa ajili ya NGOs labda, haki za binadamu etc.
Utaambiwa punguza kuajiri, ongeza umri wa mtu kustaafu ili kupunguza pension,
Maswala ya uzazi wa mpango ishupaliwe na serikali.
Acha kununua silaha kwa wingi. Punguza personel katika Jeshi la Wananchi, polisi , uhamiaji na magereza. Watakuambia watu wote hawa wa nini? Kwani kuna vita?
Watakuambia badilisha mitaala na kuondoa baadhi ya masomo ili kuipunguzia serikali mzigo.
Watakuambia mfumo wa mikopo elimu ya juu sio effective.badilisha na iwe kwa wanafunzi wachache. Watakuambia kuna watoto wenye uwezo mnawapa mikopo.
Watakuambia non academic personel ni wengi katika mfumo wako wa elimu. Wapunguze.
Watakuambia achana na umeme wa maji. Funga mabwawa ya kuzalisha umeme.
Watakuambia, why GoT is running from two capitals? Chagua moja.
Watakuambia mfumo wako wa umiliki ardhi umekaa kijamaa sana. Badilisha.
And so and so and soooo!
 
Huyu mzee asitaafu sasa
Sawa kuwa bila kukopa Itabidi serikali iwakamue wananchi kulipa tozo za kila aina!! Ukikopa wananchi wanategemea wapate afueni ya hizo tozo lakini hilo sivyo kwa nchi yetu; wananchi wanakamuliwa kwa mlundiko wa tozo na Samia na Madelu wake wanazidi kukopa tu!! Mbadilisheni huyo waziri sio mchumi mbobezi.
Huyu mzee inabidi astaafu na mchumi aliyebobea akachukue nafasi yake ; yeye akaendeleze kampuni yake ya uwakili.
 
Back
Top Bottom