Mafisadi wote wanajulikana sehemu walipo,mmoja yupo Kenya,anaomba hifadhi,wengi waliobakia wapo hapa hapa Tanzania yetu,wengine walipotelea Marekani kwenda kusomea digrii ya ufisadi na wamerudi kusubiri zamu yao,wamekuwa kama Tai walioona mzoga hawachezi mbali na Tanzania yetu,maana haina mwenyewe.
Lakini huyu D BALLALI ambaye hatujui ukubwa wake kimadaraka mpaka hata Serikali ya CCM haiwezi kumrejesha kwa kuwa hajulikani alipo! Mimi nadhani tuwaulize wale wote ambao leo wanarudisha pesa kwa mlango wa nyuma na Serikali inakubali bila hata kuwaweka magereza, ili kupata ukweli namna walivyozipata hizo pesa. Kwanini tunakubali kuwa kimya kiasi hiki, tusimuulize huyu bwana sifa ni nini kinachosababisha Ballali kushindwa kumrejesha nchini kujibu kesi yake.
Watanzania wangapi wamekufa,wamerejeshwa na wengine hata kutolewa na kupelekwa nje ya nchi kushtakiwa, kwanini huyu Ballali mtanzania mwenzetu inakuwa ni kigeu geu kwa Serikali!.
Sasa naamini Ballali,Rais Mstaafu B W M na J M K NA C C M yao wana kesi ya kujibu, na shahidi namba moja ni Ballali.
Watanzania wa ndani na mliopo nje tushirikiane kumtafuta huyu Balali mwenye siri nzito tumrejeshe kwa njia ya umoja wa mataifa,la muhimu tujue yupo wapi, kama yupo Afghanistan tumuombe BUSH, KWA NI YEYE TU anayeweza kufika hapo,kweli nawaambia kama sisi wenyewe watanzania hatutakuwa tayari kuona umuhimu wa Balali kurejeshwa nchini ili aje kuwataja Mafisadi wenye kinga basi tumekwisha kwani ni kila baada ya miaka mitano wanazaliwa si chini ya watano na baada ya miaka kumi anazaliwa mmoja ambaye naye anakinga.
BALLALIIIIIII ole wako TUKIKUPATA
AHSANTE
SEFF
Jamani nauliza BALALI yuko wapi???. na serikari imechukua hatua gani?
Cha kushangaza ni kwanini modes wameiweka hii kwenye vibweka vya wakubwa!Wadau kuna mtu mwenye taarifa yoyote kuhusu gavana wetu wa Benki Kuu? Hivi bado anaumwa? Bado yuko US au kesharudi Dar? Ni muda mrefu, kumekuwa na umkimya sana kuhusu Mhe. Gavana ambaye ni mtu muhimu katika masuala ya fedha TZ.
Wadau ninaomba taarifa.
1. kafichwa au kajificha??
2. Bado mgonjwa mahututi au kidogo afadhali?? kama ndio, yu na hali gani? yu hospitali au nyumbani? Tunaomba kuelezwa yuko wapi tukamjulie hali.
Inabidi tuandamane ili kuleta dhana halisi ya nguvu ya Umma na vyombo vyote vya habari vishikie bango hili suala la kuishinikiza serikali imlete Balali aje ajibu shutuma zake
Ndugu zanguni mi nina imani kabisa hapa kuna kamchezo kachafu ka kuzugana ili mambo yapoe na wadanganyika ghadhabu zitulie. Balali anajulikana alipo ingekuwa JK ni mwenzetu kwenye kijiwe chetu angetutonya kidogo ingawa angejidai tusimwambie mtu...Si unajua mtu mzima akijamba huwezi kusema? utageuza lugha kuwa bomu limelia kumbe kachafua hali ya hewa. Siri ya urembo iko kwa balali na ndio maana wametulia iko siku atachomolewa huko aliko ndipo mchezo utakaponoga mwanawane!!!
Hata Big Ben nae huenda anazugazuga nadhani anatamani na Zimbabwe wafurushane ili ahamie huko kujifanya msuruhisi ili auwe sooo!!! lakini kitaeleweka tu. Tatizo Mzee wa Zengo la kupinda nae ameanza kutupotezea stimu za kazi anapodai kuwa mafisadi wana pesa sana kwa hiyo kuwashitaki inahitaji uangalifu sijui anawinda digidigi anaogopa atakurupuka au vipi anaturudisha enzi zile za kulala usingizi wa pono kuamshwa mpaka umwagiwe maji sikioni...Hatuko tayari kwa hilo.....Mi nawaambia historia itaandikwa mwaka huu eh!!