Gavana akerwa na uchafuzi wa mazingira

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
*~Aagiza kukamatwa mara moja kwa Mwanakijiji*

*~Ni baada ya kuanzisha dampo kienyeji kwenye makazi ya Watu*

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe, Gavana Emmanuel Shilatu ameagiza kukamatwa Mara moja kwa mkazi aliyekuwa ameanzisha dampo holela kinyume na utaratibu ili kuzuia uwepo wa magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu n.k.

Gavana Shilatu ametoa maamuzi hayo mara baada ya kusimamishwa na wakazi wa kijiji cha Miuta waliomweleza kero ya dampo hilo ambalo ni hatarishi kwa afya za wakazi hao.

*"Hakuna asiyejua umuhimu wa mazingira safi. Huyu aliyeanzisha dampo kienyeji kwenye makazi ya Watu na ni jeuri, naagiza akamatwe mara moja na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake."* - alisema Gavana Shilatu huku akishangiliwa na Wakazi hao waliokerwa na dampo hilo.

Gavana Shilatu pia aliwapongeza viongozi wa kata pamoja na wa kijiji cha Miuta kwa kushirikiana vyema na Wananchi wao na kusisitiza waendelee kuwafichua wavunja sheria sugu kwa maslahi mapana ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

*"Nawapongeza Viongozi wa Kata na wa Kijiji cha Miuta kwa ushirikiano na Wananchi. Endeleeni kufanya kazi pasipo kuangalia hadhi, rangi, dini, kabila wala itikadi ya Mtu na msisite kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wavunjifu wa Sheria, taratibu na kanuni za nchi"* alimalizia Gavana Shilatu.

Katika tukio hilo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kata Miuta, Afisa maendeleo kata, Mwenyekiti Kijiji cha Miuta pamoja na Mtendaji Kijiji cha Miuta.
IMG-20181128-WA0613.jpeg
 
Back
Top Bottom