GATUSSO: mnipange ama niondoke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

GATUSSO: mnipange ama niondoke

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Gang Chomba, Nov 27, 2009.

 1. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Aliyepata kuwa dikteta wa kiungo barani europa kwa Miaka ya hivi karibuni Ivan Rhino Genarro Gatusso amefungua kinywa chake na kusema kuwa anataka kujua mustakabali wa kupata namba katika kikosi cha kwanza hapa Milan ama la basi atatimka klabuni hapa.
  kauli hiyo imetolewa kwa masikitiko makubwa na kiungo huyo nguli mwenye amsha amsha za kutosha awapo dimbani kufuatia kitendo cha kocha Leonaldo kuendelea kutomtumia kamanda huyo aliyepata kuwa pia kipenzi cha washabiki wa rossonelli.
  Hakuna taarifa rasmi zilizobainisha kuwa ni sababu gani haswa imepelekea Gattuso kuwa benchi kwa mechi nyingi.
  Lakini kuna habari zisizo za uhakika sinadokeza kuwa kocha Leonardo ameamua kutokumtumia kiungo huyo kutokana na kitendo chake cha utovu wa nidhamu alichokionyesha ktk mechi ya wapinzani wa jadi maarufu kama dela madoninna kati ya Rosonelli na Nerazurri ambapo Milan walifungwa goli 4-0 nyumbani kwake na Inter.
  Lakini pia duru za soka zinadokeza kuwa mfumo unaotumika sasa wa kuwasimamisha washambuliaji wawili mbele ndo kikwazo cha kupata namba kwa Rhino. Wachambuzi wa soka pia wametanabaisha kuwa tangu kocha Leo alipoanza kuutumia mfumo huu Milan imekuwa na mfululizo wa ushindi ama droo kitu ambacho ndio milan wanachokitaka kwa sasa.
  Najihisi kama ni kiongozi muasi kwa jinsi ninavyofanyiwa hapa Milan...hakika naumia sana pale ninapoona mashuka makuubwa yaliyoandikwa maneno ya kunisifu na kunitukuza toka kwa washabiki wenye imani nami lakini nayasoma hayo nikiwa nimekaa benchi...alikaririwa Gattuso kwa uchungu.
  Lakini kwa sisi tunaoijua Milan tunaona wazi kuwa Leonaldo atakutana na upinzani mkali toka kwa washabiki wa Milan kufuatia kitendo chake cha kumuweka benchi mshambuliaji anayeaminika kuwa ni hatari Suppa Pippo Fillipo Inzaghi.
  Hakuna uthibitisho mpk sasa unaoonyesha ni lini ama ni wapi Pippo aliwahi kumpiga chenga, ama tobo, ama kisigino beki kisha akafunga, lakini inaaminika kuwa Pippo ndiye mshambuliaji hatari na mabeki huwa makini kwa kipindi chote awapo uwanjani.
  Leonaldo ameonyesha imani kwa washambuliaji Alesandro Pato na marco Boriello na amekuwa akimtumia kwa nadra sana mshambuliaji huyo kipenzi cha watu wa milan aliyejiunga na klabu hiyo mwaka 2000 akitokea Bianconelli ama Juve.
  Akiongelea matukio haya hivi karibuni makamo wa rais wa klabu hiyo muheshimiwa Adriano Galliani amesema kuwa mambo yote haya yanatokea ni kwa sababu tu ya swala zima la wakati...
  Milan ilianzishwa tarehe 16/dec/1898 na tangu hapo imebeba kombe la ulaya mara 7 na ndio klabu iliyobeba vikombe vingi vya kimataifa kuliko klabu yoyote hapa ulimwenguni.
  'SFORZA MILAN'.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  uhasama na makocha una spoil sana viwango vya wachezaji.

  si mnakumbuka kilichomkumba rivaldo akiwa ac milan?
  kiwango alikuwa nacho kilikuwa ni cha juu sana,
  lakini kocha akasema hakumpeleka hapo klabuni,
  ila alikuwa amepelekwa na rais wa klabu,
  kwa hiyo rais wa club ndio ampange...
  dogo akakaa benchi,
  mwisho wa siku kiwango kikaporomoka na leo sijui hata aliko.
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  lakini jamaa anaonekana kweli mbabe sana uwanjani, rafu nyingi sana.
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Gatusso keshazeeka!
   
 5. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi na flamini nae vipi kama mtu mzima Gattuso hachezi yeye inakuwaje? Au ndo anacheza badala ya Gattusso?
   
 6. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Nimeifuatilia timu hii kwa muda sasa na ninachojaribu kukwambia ni kuwa Flamini nae hana namba ingawa mara kadhaa amekuwa anaingia kama sub.
  Gattuso alivimba sana kichwa, acha ashikishwe adabu.
  Kama timu inaweza kwenda el santiago bernabeu bila yeye na kupata ushindi ni wazi kuwa hana msaada kama yeye anaofikiria
   
 7. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Ili Gattuso apangwe basi ni wazi mmoja kati ya Boriello ana Pato anatakiwa akae benchi. Na hili haliwezekani kwa sababu wote hawa kwa sasa wako kwe fomu.
  jamaa alikosea ktk mechi waliyofungwa 4 dhidi ya Inter kwani alipewa kadi nyekundu ya kizembe kisha akaenda kumfokea leonardo na kuvua jezi na kuitupa chini.
  Kitendo hiki kilitafsiliwa tofauti na waandishi wa soka
   
 8. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh halafu mkuu gang chomba nahisi sasa watu watakuwa wamefahamu timu unayoishabikia.
  Teh teh tutaanza kuifuatilia sasa ili tuwe tunakupa maneno machafu kama unayoyatoaga kwa wenzako
   
 9. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Na wakati ligi ilipokuwa inaanza milan walikuwa na matokeo mabaya kutokana na kumsimamisha mshambuliaji mmoja mbele.
  Lakini toka alipoanza kusimamisha watu wawili timu imekuwa na matokeo mazuri mpk rrraha yani.
  Pirlo ni mtu muhimu sana ktk kikosi hivyo hawezi kukaa nje, na pia mtu kama Clarence nae
  Ni mtu hatari sana.
  So mtu anayetakiwa akae nje kwa ajili ya Gattuso ni Massimo ama tunaomjua tunamwita Ambro ambaye ndiye Nahodha wetu na pia ana uwezo mkubwa wa kunyang'anya mipira pasipo rafu. Pia ambro ana kipaji cha kupiga mipira mirefu na kumdondokea mshambuliaji nae akafunga...
  So Kaka Gattuso itakuwaje?
   
 10. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Maskini Flamini, anasubiri wazee wastaafu then aanze kucheza.
   
 11. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kwa kwa kwaaaaa
  Wakuzeheka ni nani?
  Seeldorf?
  Au Pirlo?
  Yaani hawa hawazeheki.
  Juzi seedorf kawajibu waandishi wa habari kuwa ni rahisi kwa waandishi kustaafu kuliko yeye kutundika daruga...so kama Flamini anasubiri atasubiri mpk kunakucha
   
 12. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Dah hili swala la Inzaghi hata mimi limeanza kunitia hofu.
  Ila mmmmh mie chimo.
   
 13. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  OFFICIAL NEWZ:
  Makamo mwenyekiti wa AC Milan msema hovyo Adriano Galianni muda wowote atakuwa na kikao cha faragha na Gattuso.

  Source: le gazzetto dello sport
   
 14. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,276
  Likes Received: 4,260
  Trophy Points: 280
  Flamini siku hizi anacheza beki wa kulia/kushoto na anaanzia bench
   
 15. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  flamini kafulia vibaya mno.
  We fikilia anacheza mtu kama Abate yeye amejikunyata tu nje.
  ana wakati mgumu kwa kweli. Wale jamaa wana tradition zao ktk soka
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kocha wa Milan Leonardo kawatoa hofu wana Milan kwa kuwaambia kuwa kibaba chao kikiwa fit 100% atakipanga tu hivyo msihofu
   
 17. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Halafu huyo gatuso mwenyewe anayezungumziwa basi utafikiri labda ni fabregas ama gerald ama lampard. Kumbe zee limeshachoka.
   
 18. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Flamini jana kaanza dimba la chini kuchukua nafasi ya Pirlo aliepumzishwa...final result catania 0-2 milan.
  Thanx to Hunter
   
Loading...