Liz Senior
JF-Expert Member
- Apr 19, 2007
- 483
- 53
Q, mimi pia nina tatizo hilo, Kabla sijajua ni nini nilifikiri nina kitu kinaota kooni...nipata shida sana. Nashukuru nilionana na Dr. mzuri sana alinieleza kwa mapana yake na umuhimu wa kufuata masharti. Usishindane nao, utaumia zaidi. In fact alinieleza zamani watu wenye tatizo hilo walitibiwa kama watu wenye matatizo ya akili kwa vile ilikuwa haieleweki ni nini. Wengi walipata depression, na walijitenga sana na wengine. Ni kwa vile ni kitu kinakera na huwezi kumweleza mtu akakuelewa.
Tangu wakati huo nimekuwa makini sana na vyakula na ni muhimu kuhakikisha unalala kichwa kimenyenyuka kidogo..mto mzuri. muhimu zaidi usiifikirie sana hiyo hali,
Q, sijapita huku muda mrefu sana. Ninaendelea vizuri na huwa hainisumbui kama pale mwanzoni maana nimeikubali na kuijitahidi sana kufuata maelekezo. ILA nikikosea kitu hasa ulaji, ikiwa si vitu sahihi au nisipokula kwa wakati (mf kula muda mfupi kabla ya kulala) basi najiandaa kwa kero hiyo