Garissa Kenya: Polisi watatu wauawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ardhini

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Maafisa watatu wa polisi wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulio Jumatano alfajiri eneo la Liboi Kaskazini Mashariki mwa Kenya karibu na mpaka wa Somalia.

Duru za usalama zinaarifu kuwa gari la kijeshi lililokuwa limewabeba maafisa wa usalama wa Kenya lilikanyaga bomu la kutegwa ardhini

Taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari Kenya zinasema kuwa maafisa hao walikuwa wanapiga doria katika eneo la Kulan wakati gari lao lilipokanyaga mlipuko huo.

Maafisa wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo na inaarifiwa wamesafirisha hadi mjini Nairobi kupokea matibabu maalumu.

Katika mtandao wa kijamii wa Twitter, Shirika la msalaba mwekundu linasema ; gari limekanyaga bomu la ardhini na kuwajeruhi watu 8 baina ya Liboi na Kulan, Kaunti ya Garissa." Liliendelea kusema kwamba linashughulikia tukio hilo.

Gazeti la Daily Nation linaripoti kuwa maafisa hao walikuwa wanasafiri kwa gari la kituo cha polisi cha Kulan katika barabara ya Liboi - Milan wakati gari hilo lilipokanyaga bomu la kutegwa ardhini

Inaarifiwa gari hilo liliharibika vibaya.

Makamu wa Rais William Ruto ametuma ujumbe katika Twitter akisema, Waathiriwa wa shambulio la Liboi kaunti ya Garissa wamo mawazoni mwangu. Ni lazima tuujenge ukuta mpakani.

Serikali ya Kenya iliidhinisha ujenzi wa ukuta katika mpaka baina ya Kenya na Somalia kuzuia uharifu baada ya shambulio la kigaidi dhidi ya chuo kikuu cha Garissa mnamo mwaka 2015.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom