Gari za FFU zimemwagwa Ubungo hadi Kimara

Pole sana OC - CID sio officer, wanazurura na madeffender usiku kukamata wacheza pool, kutoka kila kichwa 10,000/- kukamata wauza gongo ambao hawajatoa posho ya kila wiki 5,000/-, mnaweka check point za kukusanyia return, kichekesho mnasimamisha maroli tu, na madereva wanavyowadharau wanawatupia 500/- kila check point, magendo yanapita. POLIBUSINESS LTD, Ukipangiwa patrol na Pikipiki, return 10,000/- Golf return 50,000/- Deffender return 100,000/-, check point return 100,000/-, Trafic return 20,000/- kona mbovu, kwenye ulaji 50,000/-. Hao FFU ni njaa kali ndio maana wana mihasira. Mnakula na mafisadi wa CCM, ndo maana mko tayari kuwafia. Wasaliti wakubwa nyie.

ushapeleka malalamiko kwenye ngazi yoyote!? Ni kinyume ya utaratibu kwa askari yoyote kufanya hvyo!
 
Hayo ni matumizi mabaya ya lasilimali, Nguvu inayotumika kudhibiti maandamano ingetumika kudhibiti wahamiaji haramu ingekuwa bora zaidi.
 
Salaam wakuu,
Nimetokea Kibamba. Nimefika maeneo ya Kimara nimekuta Difenda za FFU kama sita hivi zikirandaranda huku zikiwa zimesheheni askari waliojikoki kana kwamba wanajiandaa kuingia kwenye msitu wenye wanyama wakali; wamebeba maguruneti na zana za kutisha. Pamoja nao wamo askari kanzu kibao nao wanarandaranda katika maeneo hayo.

Karibu njia nzima kutoka Kimara hadi Ubungo imesheheni magari ya FFU. Mengine yamepaki maeneo ya Rombo, Baruti, Kibo na Ubungo yenyewe.

Nilijaribu kudodosa kulikoni, ndipo nilipoambiwa kuwa hayo ni maandalizi ya kuwatawanya wafuasi wa chama fulani ambao walijiapiza kuandamana leo. Maandamano hayo yalipangwa kuanzia eneo la Kimara, ndio maana Polisi wamejizatiti kudhibiti eneo hilo.

Njiani pia nilikutana na Mwenyekiti wa Bavicha Bw. John Heche akiwa kwenye gari yake Nissan Patrol nyekundu akielekea maeneo hayo. Ndio anakwenda kuongoza maandamano....!!? Tusubiri tuone!

Je unajuwa kazi za polisi ni nini?

na kwanini uwaogope polisi kama wewe si muhalifu?
 
Viongozi wengi nchini wapo madarakani kwa nguvu ya rushwa, kuiba kura/kuchakachua kura, kutegemea waganga, udanganyifu/ahadi za uongo, undugu/udini. Hii imeleteza tumekuwa na viongozi wasiowajibika, wapenda starehe, wasiojituma na kufikiri kwa kina juu ya utatuzi wa matatizo ya watu, viongozi wasiona-vision, bali wenyekutawala kwa kutemea POLICE na JESHI. Sababu ni viongozi wabovu wanazani wata-control nguvu ya mabadiliko katika jamii kwa kutumia police!!

Police wetu wanakosa akili na hivyo kutumiwa kulinda maslahi ya wachache
 
Unaongelea kwenye button za cm!! Unajifanya shujaa kumbe kunguru la zenji
 
na ndio maana ikija kwenye suala la uhalisia wa maisha wanakuwa waoga sana maana wanashika responsible positions kwa kutumia 'artificial profiles'
Viongozi wengi nchini wapo madarakani kwa nguvu ya rushwa, kuiba kura/kuchakachua kura, kutegemea waganga, udanganyifu/ahadi za uongo, undugu/udini. Hii imeleteza tumekuwa na viongozi wasiowajibika, wapenda starehe, wasiojituma na kufikiri kwa kina juu ya utatuzi wa matatizo ya watu, viongozi wasiona-vision, bali wenyekutawala kwa kutemea POLICE na JESHI. Sababu ni viongozi wabovu wanazani wata-control nguvu ya mabadiliko katika jamii kwa kutumia police!!

Police wetu wanakosa akili na hivyo kutumiwa kulinda maslahi ya wachache
 
hivi kwa akili yako unadhani polisi wote ni form 4? Am young and energetic and a graduate frm a respected university with a CPA..nina cheo na maisha safi na mshahara wangu ni mkubwa,fanyeni maandamano 2NAWANYUKA.

Hii akili haiwezekani ikawa ya Graduate, ni ya FISADI au MTOTO wa FISADI!! Graduate ambaye anaipenda nchi yake hawezi kubaka democracy!! Inaelekea ninyi ndiyo mnaokula pesa za askari wetu ndiyo maana wako frustrated na wanafanya kazi bila kufikiria!!
 
Si mnapelekwa pelekwa bila kujua mnachokitaka, sasa andamana wakati bwana zenu wamejifungia ndani wanapiga chabo kwenye runinga. Jiulize wale waliokufa Arusha na kuzikwa na maelfu ya watu, nini kimeendelea kwa familia zilizokuwa zinawategemea? ama kuzikwa kwa stlye ile ndo sifa za kwenda kwenye maandamano!! Mi nadhani kama una shughuli ya kufanya na kujua wajibu wako kwa familia yako huwezi kwenda kwenye maandamano ambayo unajua yamekatazwa na madhara yake yanajulikana. FANYA KAZI ACHA DOMO.
 
Serikali ya mabavu ya CCM ina uwezo wa kununua vifaa vya kisasa vya kuumiza watu,lakini inashindwa kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watu yanapotokea maafa kama vile ajali ya meli iliyotokea hivi majuzi. Kweli nimeamini CCM ni Chama Cha Mashetani,kazi ya shetani ni kuiba ,kuua na kuharibu.

Hawanunui magari ya zimamoto wala magari ya wagonjwa wanatumia rasilimali za nchi kununua magari ya kuwalinda wasitolewe madarakani.
 
Pole sana OC - CID sio officer, wanazurura na madeffender usiku kukamata wacheza pool, kutoka kila kichwa 10,000/- kukamata wauza gongo ambao hawajatoa posho ya kila wiki 5,000/-, mnaweka check point za kukusanyia return, kichekesho mnasimamisha maroli tu, na madereva wanavyowadharau wanawatupia 500/- kila check point, magendo yanapita. POLIBUSINESS LTD, Ukipangiwa patrol na Pikipiki, return 10,000/- Golf return 50,000/- Deffender return 100,000/-, check point return 100,000/-, Trafic return 20,000/- kona mbovu, kwenye ulaji 50,000/-. Hao FFU ni njaa kali ndio maana wana mihasira. Mnakula na mafisadi wa CCM, ndo maana mko tayari kuwafia. Wasaliti wakubwa nyie.

Nilipo RED.

Fanya homework yako vizuri. Cheo kikubwa sana hicho yaani Afisa upelelezi wa Wilaya yaani asiwe ofisa. Je unajuwa kuwa huyo ni wa pili kimadaraka katika mpangilio wa Polisi katika wilaya. No 1 ni OCD.

Lakini vile vile tuhuma ulizotoa ni nzito sana na cha kufurahisha sasa hivi Tz mpo katika mpango wa Polisi Jamii. Kila namba ya mkuu wa polisi ipo wazi na hadharani.

Pitia web site yao www. policetz.go.tz kisha peleka tuhuma zako ili zifanyiwe kazi.

Ipende nchi yako kwa kuibua maovu yote na kuyapeleka panapo husika.
 
Nguvu ya umma ipo wapi wewe? nguvu ya umma na wabunge 23...

Hizo gari 6 ni chambo tu jitokezeni muone mizigo yenyewe imepaki Lugalo inasubiri amri tu..

Ndio mtajua nidhamu ya Jeshi la polisi Tanzania ni kubwa kiasi gani

Siku hizi Polisi wana kambi Lugalo?
 
hivi kwa akili yako unadhani polisi wote ni form 4? Am young and energetic and a graduate frm a respected university with a CPA..nina cheo na maisha safi na mshahara wangu ni mkubwa,fanyeni maandamano 2NAWANYUKA.

Ndugu ebu usiwadharirishe polisi wasomi. Hawaongei ujinga na upuuzi unaochangia hapa.
 
Tatizo sio wao tatizo kiapo walichoapa cha kuwa watiifu kwa mkuu hata kama anamchukua wife inabidi atii tu.leo cha kati kimetoka hvyo wamesahau shida.(Cha kati ni posho)kwa wale mlioishi kota mnafaham
 
Wao wanadhani tunaogopa hayo magari yao?tena wakaandae makaburi na wapanue keko na segerea ili tutakaokamatwa tupate pa kwenda

Ndugu zangu Watanzania sisi tunayo silaha kubwa ya kupambana na askari hawa wanaopewa amri na kuitekeleza bila kutumia common sense. Wanatumia nguvu nyingi ldhidi ya raia asiyekuwa na ahatia na kuwaacha vibaka, wezi, wavuta bangi na mafisadi papa wakaitanua. Hii leo ukiibiwa kitu nenda polisi. Utaambiwa kamkamate mwizi wako uje, mara tupe hela ya mafuta gari halina mafuta, mara lete kianzio na mambo kibao. Sasa tumewachoka polisi.Tunatakiwa kuwapa somo la vitendo "actions speak louder than words" Ni wepesi wa kutaka vya bure.Tuwanyime lifti kwenye magari yetu, kwenye daladala kuanzia leo walipishwe nauli, kwenye magenge na maduka wasikopeshwe na wapandishiwe bei, mtaani tusiwape ofa ya bia wala soda au chochote, kwenye magazeti tuwachafue, kwenye sherehe tuwaalike na wakitualike tusiende, wakipita njiani tuwazomee tuseme "hao wauaji, watesaji,mawakala wa ccm" na kila aina ya zomeazomea ali mradi somo limefika.

Uwezo tunao na tuwaonyeshe kuanzia sasa ili waweze kuitambua nguvu ya umma. They should come back to senses and be reasonable in the thinking and actions. Gone are days of robotic mode of response and operations. On the contrary these are days of resonableness and proactiveness
 
Fanyani maandamano 2wanyuke! 2nawasubiri.

Hivi kwa akili ya kawaida tu, unadhani unawanyuka kina nani? wewe ni polisi eeh? sawa! Wazazi wako na ndugu zako wengine wanaishi wapi, wanaishije huko? kwanini wanaishi vile? pengine ndugu na jamaa zako wanaishi raha msstarehe, lakini waTanzania wengine wanaishije, kwanini? Matumizi mabaya ya rasilimali za taifa wewe yanakufurahisha?
sawa utafyatua risasi kuwaua waTanzania kwani wewe hao ni adui zako? wana silaha na wanafyatua pia? Badirika ewe Mtanzania.
 
Back
Top Bottom