Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Hivi gari sita(6) na polisi zinaweza kuzuia nguvu ya Umma!!!!!!, polisi wasijidanganye katika hilo nijuavyo mimi ni kwamba Sisi Wananchi bado ni majoga sana, labda tutafanya hivyo mpaka itakapofikia mahala CCM wakaamua kwenda mbali zaidi na kutupapasa sehemu zetu za kukalia.Salaam wakuu,
Nimetokea Kibamba. Nimefika maeneo ya Kimara nimekuta Difenda za FFU kama sita hivi zikirandaranda huku zikiwa zimesheheni askari waliojikoki kana kwamba wanajiandaa kuingia kwenye msitu wenye wanyama wakali; wamebeba maguruneti na zana za kutisha. Pamoja nao wamo askari kanzu kibao nao wanarandaranda katika maeneo hayo.
Karibu njia nzima kutoka Kimara hadi Ubungo imesheheni magari ya FFU. Mengine yamepaki maeneo ya Rombo, Baruti, Kibo na Ubungo yenyewe.
Nilijaribu kudodosa kulikoni, ndipo nilipoambiwa kuwa hayo ni maandalizi ya kuwatawanya wafuasi wa chama fulani ambao walijiapiza kuandamana leo. Maandamano hayo yalipangwa kuanzia eneo la Kimara, ndio maana Polisi wamejizatiti kudhibiti eneo hilo.
Njiani pia nilikutana na Mwenyekiti wa Bavicha Bw. John Heche akiwa kwenye gari yake Nissan Patrol nyekundu akielekea maeneo hayo. Ndio anakwenda kuongoza maandamano....!!? Tusubiri tuone!