Gari yangu ya kwanza nimenunua, Nissan Dualis

NUNEZ DIAZ

Member
Apr 15, 2015
85
108
Habari wana JF,

Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nimenunua na kumiliki gari yangu ya kwanza nissan dualis, kusema ukweli sijui vitu vingu kuhusu magari nafahamu vitu vichache sana.

Naombeni msaada jinsi ya kuitunza hii gari angalau idumu napokea maoni na ushauri jamani, gari nimeipokea juzi tu
 
habari wana jf
kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nimenunua na kumiliki gari yangu ya kwanza nissan dualis,,kusema ukweli sijui vitu vingu kuhusu magari nafahamu vitu vichache sana naombeni msaada jinsi ya kuitunza hii gari angalau idumu napokea maoni na ushauri jamani,,gari nimeipokea juzi tu
Dnt drink and drive, zingatia service, kama bado ni kijana, achana na mambo ya kijanga ya kushindana nani anamaliza kisahani.
 
Habari wana JF,

Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu nimenunua na kumiliki gari yangu ya kwanza nissan dualis, kusema ukweli sijui vitu vingu kuhusu magari nafahamu vitu vichache sana.

Naombeni msaada jinsi ya kuitunza hii gari angalau idumu napokea maoni na ushauri jamani, gari nimeipokea juzi tu
1.Kumbuka kubadilisha Oil kwa wakati, ni muhimu sana. Hii inaambatana na aina sahihi ya Oil inayopendekezwa na watengenezaji wa gari lako. Fanya service kwa wakati.

2. Zingatia uendeshaji wako. Speed za kipuuzi, brake za kujidai na uendeshaji wowote wa kihuni achana nayo.

3. Chukulia serious mabadiliko ya gari. Ukishaizoea gari lako, likianza kubadilika utajua tu kuwa kuna mahali. Chukua serious na tafuta suluhisho mapema.

4. Marafiki ni wazuri. Lakini epuka sana kuazimisha azimisha gari lako kwa marafiki.
 
ahsante sana kwa ushauri
 
1. Epuka kuoshea gari Lako maji ya Chumvi. Utaliharibu na litapauka Sana.

2. Kuwa mbahili WA kuasimisha gari Lako. Epuka Sana kuasimisha watu gari. Gari ni lako peke yako.

3. Fanya service Kwa wakati. Kama oil inabidi ubadiri baada ya kilomita 5000 zingatia Hilo.

4. Tafuta fundi wako mmoja anaejua KAZI. Acha kumpa kila fundi gari lako awe analigusa utakuja kuharibiwa gari Lako.

5. Jifunze hata namna ya kufungua tairi na baadhi ya parts za gari sio unachojua ni kuingiza ufunguo na kukunja usukani.

6. Unapokwenda Kufanya service. Oil na vifaa vingine mwambie fundi akuandikie anavyovihitaji ukanunue kwenye maduka Genuine yeye fundi KAZI yake aje kuweka kwenye gari. Kumeibuka mafundi Wasio waaminifu unawapa hela wakufanyie service wanaweka Oil na vifaa vingine feki mwisho WA siku injin ya gari inakufa.

7. Zingatia alama za barabarani ipasavyo achana na mihemko.
 
Hakika umemaliza kazi na gari unalo
 
1.Kumbuka kubadilisha Oil kwa wakati, ni muhimu sana. Hii inaambatana na aina sahihi ya Oil inayopendekezwa na watengenezaji wa gari lako. Fanya service kwa wakati.

2. Zingatia uendeshaji wako. Speed za kipuuzi, brake za kujidai na uendeshaji wowote wa kihuni achana nayo.

3. Chukulia serious mabadiliko ya gari. Ukishaizoea gari lako, likianza kubadilika utajua tu kuwa kuna mahali. Chukua serious na tafuta suluhisho mapema.

4. Marafiki ni wazuri. Lakini epuka sana kuazimisha azimisha gari lako kwa marafiki.
Umemaliza kila kitu mkuu
 
Kuna jamaa yangu nesi alichukuaga mkopo akalichukua hilo dude Dualis, ikawa mda wote maspeed tu.. Umbali mdogo tu anataka amalize sahani.. Alikuja kulibwaga, bahati nzuri alipata tu michubuko.

Kuna mwamba mwingine alikua daktari, nae Dualis ilikua gari yake ya kwanza.. Sijui lilimkuta jambo gani maana tuliishia kuambiwa amesha-R.I.P na alikua ktk barabara iliyonyooka ila gari ilitoka nyang'a nyang'a hakuna kilichopona!

Ushauri wangu jitahidi kua na nidhamu road.
 
Jambo la kwanza kwenye oil ya gear box. Fanya ubahiri wote ila sio hilo eneo. Usije ukaweka brand ya oil nje ya ile ya Nissan au ipo moja ya mobil ila sidhani kama inapatikana sana hapa Bongo. Ukiweka nje ya hiyo utakuja hapa kulia lia kuwa gari hizi ni mbovu kumbe ni wewe unashida.

Oil ya engine pia tumia yenyewe ya Nissan zinajulikana maana zipo za gear box na za engine. Asije akatokea fundi akakuchanganyia hiyo taarifa na kusema oil ni oil unaweza mix HAPANA. Kataaa. Tumia hizo oil za Nissan tuuu.

Gear box ya hiyo gari ni CVT so haitumii gear box oil (hydraulic) nyingine nje ya recommended ambayo ni zake na brand ya mobil. Utakutana na CVT oil (hydraulic) za brand zingine na mafundi wanaweza kushawishi kutia tu kwa sababu yoyote kataaaaaaaaa weka only ya Nissan.

Kingine, zingatia kutunza movements zako. Ni bora upite njia ndefu ya lami ukaingia gharama isiyozidi elfu 5 au 10 ya mafuta kuliko kufosi kupita njia fupi yenye mashimo makubwa na rough ambayo itaweza kukuchakazia gari yako na kuja kununua spare isivyo lazima. Ukiheshimu unapoipitisha ina uimara wa kutokukusumbua spare hata kwa miaka 2 bila shida yoyote.

Mengine nitakushauri kulingana na wachangiaji wanavyochangia. Karibu kwenye familia ya Nissan Dualis. For anything unaweza uliza tu bila shaka.
 
Back
Top Bottom