Gari yangu ikifika speed kuanzia 100kph inakua nyepesi, inataka kutoka barabarani, ii imekaaje!

Mkuu Mlolongo sikuzote babywalker ndivyo zilivyo zikishafika speed 100 zinakuwa hazina stability barabaran hiyo inatokana na namna hizo gari zilivyotengenezwa...
Pia hizo gari ni hatari Sana kama itatembea Kwenye speed hiyo, angalau Toyota IST kidogo iko poa barabaran unaweza kupiga speed Hadi 140 na bado inakuwa iko poa,lkn kama unaendesha Passo,bits, swift na honda fit usitegemee kuwa na utulivu barabaran.
jitahidi siku ambayo utasafiri Safar ndefu kuepuka speed kubwa Kwenye hiyo gari ni hatari kubwa
 
Kwanza umetuletea mada zaidi ya tatu kwa mpigo..

1..Umetueleza unavyospend na demu wako gheto...

2..Umetueleza kwa shemeji yako kunapikwa chakula kitamu sana, na unakula huko ukirudi gheto unalala tu...take care.

3..Unafanya ligi sometimes, na siku nyingime umefanya ligi na Murano...good kwa kutest mapafu ya gari lako...

4..Mada halisi umesema gaei linahama barabarani ukiwa high speed....
Tatizo langari kuhama barabarani huwa mara nyingi linasababishwa na wheel alignment ambayo haiko vizuri, pia kama umelinyanyua gari lako sana unaweza kuhisi hali hiyo..

Lakini pia ungekuwa vyema ungekuwa specific kuwa gari lako ni aina gani....mano IST...kwa sababu kwa uzoefu wa mafundi wangekuambia tatizo hilo ni kawaida kwa aina ya gari ulilonalo au ni shida nyingine..

Watu tuna baby walker na tunabonyeza 140kph na hazihami barabarani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bebe Walker bhan sjui Yan kinajiondoa barabarani chenyewe mnavinunua vya nini yani Kuna gari Kama Ford ranger kulitoa barabarani mpka uliombe (Sasa baba nilikuwa naomba nikutoe barabarani nikanywe bia wewe uoge)
 
IST/Vitz/Swift/Honda Fit

Ninamiliki moja kati ya hizo babywoka.

Nachotaka kujua ni je: Gari yangu itakua na matatizo sehemu ama ndio kawaida ya hizi babywoka.

Siku za weekend demu wangu huwa anakuja kunitembelea getto (mitaa ya Ubungo Riverside).

Jioni namrudisha kwao, anaishi Bunju na dada yake. Nikifika kule tena tunakaa weeee, wanapika chakula kitamu, nakula kisha usiku ukiwa mwingi naaga narudi zangu Ubungo.

Sasa kwa kuwa muda huo wa usiku traffic jams Bagamoyo Road zinakua zimepungua, gari chache, fujo za daladala zimefifia basi huwa natembea speed sana.

Naomba niseme tu huwa naamua kuanzisha ligi ndogondogo za magari mengine. Nayapita shaaaa nafurahi kinoma.

Tatizo nikifika speed kuanzia 80 mpaka 100 naona gari inakua nyepesi kinoma, inakua kama inataka kutoka barabarani. Yaani hata kutulia kwenye lane yangu inakua kazi.

Jana kuna Nissan Murano ilinipita pale Kibo Complex. Namie nikaamua kukimbizana nayo. Fyaaaaa fyaaaa fyuuuu... Gari ikawa inataka sijui kupaaa... Aaah mwisho nikaamua nirudi tu kwenye 60 kph. Jamaa huyooo nikaenda kumkuta mataa ya mwenge.

Sasa wakuu, hii tabia ya babywoka yangu kuwa nyepesi kama karatasi, kupoteza stability na kushindwa kutulia on the road during high speed ni kwamba gari ina tatizo ama ndio wekaness ya hizi gari ndogo.

Kama ndio zilivo niambieni nijue kabisaaa kuwa natakiwa kukaza my 'a$$' nivute Subaru Forester at the helm of next year.
Nunua Passo hutojuta.
 
Hii kamwe haitojuta
download-1.jpg
 
Ndugu nunua gari basi achha kupata shida kama hizo, kanunue gari ndugu yangu narudia tena kanunue gari hiyo sio gari
ila kwa ushauri weka viroba vya mchanga hata viwili au vitatu vya kilo 100 kwa kila kiroba hapo gari itakuwa nzito
lakini pia ndugu mwendo mkali unaua haina maana kuwa mwendo mdogo hauwezi kuuwa ila kuna tofauti sana ya mtu anayetembea nje usiku wa manane maeneo ya vibaka na anayecheza ndani kwake na mke wake usiku wa manane
 
Hiyo baby walker ina shinda ya handling...... Sasa kwasababu haujataka kutuambia gari yako ni aina gani na sisi hatuwezi kwambia inashida gani!
 
Gari yako ni nyepesi sana sababu imetengenezwa na mabati malaini.
Ushauri wangu uwe unaweka mawe ndani ya gari kabla hujaanza safari! Weka mawe au tofali za kutosha ndani ya gari ili kuepuka hatari inayoweza kutokea.
sasa hapa mkuu, ajali ikitokea si ndo kugongaana na hayo mawe na matofali ndani ya gari........mimi naona asindikizwe na baby pamoja na dada yake kurudi hom....
 
Unanikumbusha miaka ya 80 niliugua nikawa mwepesi kama karatasi, ilinibidi niweke make mfukoni ili upepo usinipeperushe. Chukua viroba jaza mchanga uweke kwenye gari.

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Hadi gari inajitahidi kukuokoa na kifo halafu wewe unajiuliza JF tena . Siku zako za kuishi ni nyingi bado inawezekana wewe ni mtu mwema na tegemeo la wengi . Mungu anakuokoa hadi gari lako limegundua . Acha mchezo mkuu hayo mambo ya kuokolewa na mkono wa Mungu hayanaga physics shauri lako 😂😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom