Gari ya kubeba mafuta yakamatwa na bangi

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
2446636.jpg


769149.jpg

1755006.jpg



Huko mkoani Mara, askari wamemtia nguvuni dereva pamoja, utingo pamoja na mmiliki wa gari moja lililosajiliwa kwa ajili ya kusafirisha mafuta ya gari, Scania yenye "plate" namba T263 BLL (pichani) lililokuwa limesheheni bangi iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam tokea eneo la Lamadi, Mara.

Eneo hilo linasadikika kuwa maarufu kwa biashara ya bangi kiasi cha kuzoeleka kwa wakazi wa eneo hilo.
 
Hivi hii mizigo ya madawa yya kulevya baada ya kukamatwa na polisi huwa inapelekwa wapi?
 
Hivi hii mizigo ya madawa yya kulevya baada ya kukamatwa na polisi huwa inapelekwa wapi?

kama kesi ikipelekwa mahakamani na baada ya ushahidi kutolewa na bhangi kutolewa km kielelzo huwa inateketezwa kwa kuchomwa mbele ya hakimu,mtuhumiwa na mwendesha mashitaka
 
si kilimo kama kilimo kingine? mlisema kilimo kwanza sasa wao zo muhimu kwao ndio hilo miltafutie soko , mbona hollandi inaruhusiwa? hivi kweli zao hili halifai duniani au kama lina ukali kiasi hiki haliwezi kufanyiwa utafiti kama vile mkonge kutoa umeme, miwa kutoa umeme
 
Nawasiwasi na polisi nao kuwa michezo hii wamo. Ile kazi polis asiyekuwa na Imani ya dhati anauona mzigo wa pipi huo hapo mshahara wake tena baada ya mbinde ndio kilo2 na ghafla bini vuu anaona pipi hizo hapo mtu katemeshwa na kila pipi akiipigigia hesabu na milioni kadhaa itamuwea ngumu sana kutokuficha zingine. Maana huwa ninaona wakitangaza wanasema idadi fulani kisha wanasema bado anaendelea kuzitoa.

Wadau kwa nini kila bangi inayokamatwa huonekana ilikuwa ikiletwa Dar? hapa Dar kuna mtandao gani wa wauza bangi ambao polis wanashindwa kuudhibit???? Itabidi magari yote yawe yanapigwa search ya nguvu
 
Back
Top Bottom