Gari lipi linafaa zaidi? Naombeni ushauri wenu

Opa inateleza mkuu gari yangu ya 2 kumiliki, ila gari ile nyepesi sana but kwa mbio ni balaa
kwa wepesi nakubaliana na wewe kabisa maana hata kulisukuma huwa sihitaji msaada. Nalisukuma mwenyewe tu ikitokea limegoma kuwaka.

Kwa mbio ndio usiseme, linatembea kinoma af liko stable likiwa na suspension parts nzima.
 
Alphard kwanza ni tamu sijui kama anaijua, asije kuwa anafananisha body lake na Noah!!

Nilishawahi safiri na Alphard Arusha to Dar, gari iko stable muonekano mzuri labda aseme haipendi sabb iko juu sana na pia mlango wa nyuma ndio vile yan kama tunafungua hiace.
Uko vizuri
 
Habari.

Nimeombwa ushauri, na mie nikaona busara kupata mawazo chanya zaidi kutoka hapa JF.

Ninaye jirani yangu ambaye anataka kununua gari jingine (naweza sema ku-upgrade) na kuliuza hili alilonalo kwa sasa.

Kwa sasa anamiliki IST ambayo anaiona ndogo kwa sababu familia imekua kubwa. Mara nyingi gari hii hutumiwa na mkewe (mwalimu) kwendea shule na church na pia issue za hapa na pale.

Alisema budget yake ni 15 to 20M, hivyo mie nilimshauri anunue Harrier Tako la Nyani...akasema zimekuwa common sana then nikamwambia aagize Toyota Alphard...nayo akasema ndefu sana eti kama unapaki lory lol.

Katika pita zangu JF nikaona post za Nissan Duallis ndo nafikiria nimwambie khs hiyo

Je, wana JF, kulingana na haya mahitaji yake... tumshauri gari lipi hasa litakalotimiza mahitaji yake kwa sasa? Anataka gari liwe;
  • Confortable and good looking
  • Liwe na nguvu but si zaidi ya 2000 CC
  • Lenye security features nzuri
  • Analoweza tumia kwa safari za 1000km+
  • Liwe lenye mwendo pia
Natanguliza shukrani za dhati kwa mchango wa mawazo mtakaouleta.
Suzuki grand Vitara, mistubish outlander
 
Kwa budget ya 20M Fari family mtu wa umri 60yrs. Walau iende na shamba. Sio matanuzi tu mjini. Isafiri songea -il sirari. Haya wenye kindakindaki ma machuma toeni ushauri. Kuna mtu kaniambia Nissan X trail. Je kuna option ingine?
 
1672389031888.png
 
Back
Top Bottom