Gari lingine analodaiwa kutapeli katibu CCM lakamatwa na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari lingine analodaiwa kutapeli katibu CCM lakamatwa na polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Jan 29, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Idadi ya magari yanayoshikiliwa na polisi katika kituo cha Magomeni, ambayo Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara (Pichani) anadaiwa kutapeli, yamefikia matano.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, alisema jana kuwa idadi ya magari hayo,imeongezeka baada ya gari lingine kukamatwa jana.
  Wakati gari hilo likikamatwa, tuhuma za utapeli zinazomkabili Manara, zimekitikisa chama hicho na sasa viongozi wake wameanza kukutana kwa lengo la kujadili kuhusu hatua za kumchukulia kada huyo ndani ya chama.
  Katibu wa CCM Mkoa huo, Kirumbe Ng’enda, alisema jana kuwa hawawezi kuzinyamazia tuhuma hizo, kwa vile zimechafua taswira nzuri ya chama hicho.
  “Tumelipokea, vikao vinakutana kujadili. Tunakwenda hatua kwa hatua. Hatuwezi kunyamazia jambo hili. Lazima tuchukue hatua. Hiki chama si cha kuvumilia, ni chama cha kusimamia maadili,” alisema.
  Hata hivyo, alisema hatua zitakazochukuliwa na vikao vya chama dhidi ya mwanasiasa huyo kijana kulingana na matokeo ya uchunguzi unaoendelea kufanywa na vyombo vya dola.
  Alisema pamoja na chama kuzipokea tuhuma hizo na kuamua kuzishughulikia, wanasikitishwa na mwelekeo wa taarifa zinazoihusisha CCM na kashfa hiyo.
  Manara alikamatwa Jumanne kwa tuhuma za kutapeli magari 18 yenye thamani ya mamilioni ya fedha kwa kutumia chama hicho.
  Magari, ambayoanadaiwa kutapeli, baadhi yanamilikiwa na watu binafsi na mengine yanamilikiwa na makampuni ya kuuza magari.
  Alimakatwa na kushikiliwa katika kituo cha polisi Magomeni hadi jana juzi mchana.
  Kalinga, alithibitisha kukamatwa kwa Manara na kwambakati ya magari, ambayo Manara anatuhumiwa kutapeli, 11 yanamilikiwa na mtu mmoja, sita mtu mmoja na moja linamilikiwa na mtu mmoja.

Loading...