Waziri wa Kaskazini
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 6,981
- 14,749
Wadau Kuna Gari kama Inavyooneka Pichani no za Usajili ni T961 BZT lipo Katikati ya Ruaha-Mbuyuni-M tandika-A/B Sasa liko pale Takribani Miezi 6 toka limeharibika na Lilipo sio sehemu salama kwani Kuna Kona
Nilibahatika Kusimama na kuonana na Mlinzi analinda hilo Gari na Kunipa stori Fupi kuwa toka Lilipo Haribika Dereva alie mkabidhi alimwambia anaenda kuchukua spare Mjini toka siku hiyo hajawahi kumuoana Ila aliwasiliana nae
Kama baada ya Mwezi kupita akamwambia Anaumwa, na Baadae akawa hapokei simu akipokea anamwambia bado hajapata spear Duhumuni la kupost hizi picha kuwa yule Mlinzi anadai Anapata changamoto kubwa Sana hasa Usiku anadai Kuna Gari zina simama kwa lengo la Kutaka kuiba Spear, Wadau Kama yupo anaemjua Mmiliki wa hili Gari pichani Basi amfikishie Kilio cha Mlinzi .
===============================
Update...
Nilifanikiwa kufanya Mazungumzo na Moja ya
Askari Kituo cha Polisi Ruaha -Mbuyuni Anasema hata wao Walijitahidi Kufanya mawasiliano na mmliki wa Gari no T 961 BZT Scania ambayo ni Mali JOPEPRI INTERPRISES - MOSHI Bila mafanikio kupitia kwa Mkuu wa Kituo lakini hatua Wanayotaka Kuichukua kuwafahamisha Tanroad Iringa kwa hatua zaidi.