Gari la wizi lanaswa likiwa na mabango ya picha za Masha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la wizi lanaswa likiwa na mabango ya picha za Masha

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 6, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]

  Jeshi la Polisi la Polisi Mkoani Mwanza limekamata gari moja la wizi kutoka nchini Kenya likiwa na mabango ya picha za mgombea ubunge jimbo la Nyamagana jijini Mwanza, ambaye pia ni waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha.

  Gari hilo aina ya Rav4 lilikamatwa Septemba 29 mwaka huu majira ya saa 7 mchana, katika kituo cha kuoshea magari kilichopo barabara ya Makongoro jijini hapa, ambapo ilikuwa limeibiwa na watu wasiojulkana jijini Nairobi, nchini Kenya.

  Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Nonosius Komba aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa gari hilo liliingia nchini siku hiyo hiyo (sept 29) likiwa na namba bandia za T 274 ACM.

  Kamanda Komba alisema gari hilo ni mali ya Peter Nisiah wa jijini Nairobi, namba zake halisi ni KBK 222 A, na kwamba kukamatwa kwake kulitokana na mawasiliano ya Satelaiti kati ya jeshi la polisi Mwanza na Nairobi Kenya……..

  …………Alisema namba hizo za bandia zilizotumiwa na ambazo zipo hadi sasa hivi kwenye gari hilo la wizi zinaonekana kwenye kumbukumbu ni gari moja aina ya Toyota Mac III lenye injini Na. IAZ4483564 linalomilikiwa na raia wa Kichina aliyetajwa kwa jina la Young Fredyong anayeishi jijini Dar es Salaam.

  Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa mabango ya kampeni ya picha za Waziri Masha yaliyobandikwa kwenye gari hilo la wizi, kamanda Kova aling’aka na kukataa kuzungumzia juu ya mabango hayo.

  “Usiniulize suala la mabango ya waziri Masha kuwepo kwenye gari hilo, wewe tambua tu kwamba tumelikamata, sisi hatujui hayo mabango yapo kwa minajili ipi,” alisema kwa ukali.

  Gazeti hili lilishuhudia kuwepo kwa picha moja ya Masha ambayo imebandikwa mbele ya gari hilo la wizi, huku mabango kadhaa yakiwa yamewekwa ndani ya gari hilo karibu na kiyoo cha mbele.

  Waziri Masha alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo ya kuwepo kwa mabango ya picha zake katika gari hilo la wizi hakuweza kupatikana mara moja.

  Chanzo: Tanzania Daima.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  siasa balaa
   
 3. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Masha Masha Masha Masha Masha Masha, na bado............!!!
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kitu kinachoshangaza ni kwamba huyo RPC Komba kwa nini hakuyanyofoa hayo mabango ya 'mwajiri' wake kutoka kwenye gari kabla ya kuita waandishi wa habari? Hivi anafikiria bado kibarua anacho?
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Gari la wizi likiwa limeibwa Nairobi Kenya, limekamatwa Septemba 29 mwaka huu na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, likiwa limepambwa na mabango ya kampeni ya Lawrence Masha Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye anawania ubunge Jimbo la Nyamagana, Mwanza, kupitia CCM. Gari hilo limekutwa likiwa na namba bandia za usajili T 274 ACM, baada ya
  kuibwa na watu wasiojulikana jijini Nairobi Kenya.Gari hilo liko Makao
  Makuu ya jeshi la polisi mkoani Mwanza. Gari hilo namba zake halisi za usajili ni KBK 222 A.

  ANGALIZO: Kukutwa kwa mabango ya kampeni katika gari hilo, kunaweza kuwa na maana mbili, kwanza sasa wahalifu kutumia kampeni za CCM kufanya uhalifu lakini pili inaweza kuwa kweli MAsha mwenyewe ana uhusiano na wahalifu. Ni yeye pekee na serikali wanaoweza kueleza ukweli kwa ushahidi kabla ya watu wenye taarifa zaidi kuanika kila kitu hadharani.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ni proof ya kile Dr slaa alichokisema akiwa Arusha, kwamba CCM ni kichaka cha wahalifu. Wahalifu wengi, wakiwemo majambazi, wanyang'anyi, wauaji wa albino, wizi wa magari etc hujificha nyuma ya pazia la CCM. Wanaoweka bendera za CCM kwenye sehemu zao za biashara wanaficha maovu. Hata muendesha daladala au texi akibandika picha ya JK utakuta gari hilo lina makosa kibao etc.
   
 7. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kila anayetaka kuiba, kufilisi nchi au kutenda dhambi nyingine lazima kwanza afake yeye CCM. Nakumbuka Kigoma watu wanafyeka mapori ili kuchoma mkaa. sasa nija rahisi ya kutobughudhiwa ni kutundika bendera ya kijanii (CCM). Kuanzia hapo pori utafyeka unavyotaka. So you are right
   
 8. NTINGINYA

  NTINGINYA JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wandugu hebukuweni makini kwani bango linahusiananini na ubiwaji wa hilo gari mbona mama lishe wanabandika kwenyemabenchi hapa igoma tunatandikiwa mabango ya dk silaa tunakalia wakati mengine ya masha tumewekewa juu kamakinga tusipatwe na jua hamkuona ajabu mabango yanagawiwa bure hayana uzibitwaji huyo alitumia janja ya nyani kulamaihindi mabichi lakini kumbe wenzake wapo zaid jamani tuwe na busara tusichukulie mpaka tukawa na chuki kiasi hicho
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,473
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Jamani mahita ameondoka na magari 25 ya wizi yakiwa na namba za bandia yalikamatwa baada ya muda yakauzwa mpaka leo hii anatanua na kula maisha nani masha jamani wapendwa
   
 10. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maashaaaaaaaaa! Kazi kweli kweli! Ukijipaka kinyesi inzi wadudu wabaya sana!
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mbona haueleweki unachokisema. Wewe ni product ya kata schools?
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hakuna siasa hapa ni uhalifu tu, hata kama Chadema wangekua madarakani, wezi wangetumia mabango ya kampeni kupita vikwazo vya polisi; Nafahamu hata maeneo yenye mageti ya polisi jamaa wanapamba gari na mabango ya "chagua Kikwete" na wengine huweka hata loud speaker na kupita kilaini!??? Ss kazi kweli kweli, usishangae hata magari ya polisi ama ya zimamoto na ambulance kutumika katika uhalifu. Lakni tusishangae pia ikawa mhusika anafanya kweli kampeni kumsaidia jamaa maana wahalifu nao ndio kipindi cha kujisogeza na pia anaweza kuwa mtu inocent akaingizwa mkenge na majizi akauziwa gari la wizi maana fedha za CCM huwa zinawafanya watu wehu na wahalifu hutumia nafasi hiuyo kujinufaisha. Tunakumbuka wakati wa operesheni ya kamata ya magari ya wizi toka Afrika Kusini, mengi yaliyokamatwa yalikua ya vigogo na wafanyabiashara maarufu. Kwa hiyo hili tukio ni alama ya jambo kubwa zaidi.
   
 13. W

  We know next JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tungekuwa Ulaya, Masha nje tayari ya uchanguzi kwa kashfa hiyo hata kama hausiki......
   
Loading...