Gari la Waziri lapinduka, watatu wajeruhiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la Waziri lapinduka, watatu wajeruhiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Na Mustapha Kapalata Nzega
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, na Michezo Dk Fenella Mukangala jana alinusurika kifo baada ya gari lake STK 8780 alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kwenda Mwanza kupinduka mara mbili na kujeruhi watu watatu.

  Dk Mukangala alikuwa njiani kuelekea Mwanza kwa ajili ya ufunguzi wa Mashindano ya Mpira wa Vinyoya(Darts) ya Afrika Mashariki.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Tabora Antony Lutha alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa tatu na nusu asubuhi katika Kata ya Nyandekwa wilayani Igunga mkoani hapa.

  Kamanda Lutha alisema mara baada ya ajali hiyo Dk Mukangala alipelekwa Hospitali ya Wilaya hiyo kwa huduma ya kwanza na hali yake inaendelea vizuri huku harakati za kuwapeleka majeruhi katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma zilikuwa zikiendelea.

  Alisema ajali hiyo ilisababishwa na mwendo kasi wa dereva wa basi la Green Star lenye namba za usajili T939 lililokuwa likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam, ambapo dereva huyo alipita ubavuni mwa lori katika mlima huku gari la waziri likitokea upande wa pili.

  Kwa mujibu wa Kamanda Lutha dereva wa waziri Said Komando alijitahidi kulikwepa basi hilo na kujikuta gari hilo likipinduka mara mbili na kusababisha ajali hiyo.

  Alisema dereva wa basi la Green Star Daniel Chawa anashikiliwa na polisi wilayani hapa kwa tuhuma za kusababisha ajali hiyo pamoja na makosa mengine ya barabarani.

  Akizungumuza na Waandishi wa Habari jana kuhusu ajali hiyo Katibu wa Waziri Juma Mswadi alisema mara baada ya ajali kutokea dereva wa basi aliongeza mwendo kasi zaidi.

  "Tunamshukuru mungu kwa kweli tumeweza kupona kwani ukiliangalia gari letu huwezi kuamini kama tumepona, hiyo gari haitamaniki kabisa kwani imepinduka mara tatu mungu anatupenda bado’’alisema katibu huyo.

  Alisema taarifa hizo za ajali tayari zilikuwa zimetolewa kwenye idara husika na taratibu mbalimbali zilikuwa zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha hali ya matibabu , uchunguzi wa afya ya waziri pamoja na majeruhi wengine.

  Aidha Gazeti hili halikuweza kumpata waziri Mukangala ili kuzungumzia ajali hiyo kwa kuwa muda wote alikuwa na viongozi mbalimbali wa serikali waliokuwa wamefika kumjulia hali.
  Gari la Waziri lapinduka, watatu wajeruhiwa

   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Asharud dodoma huyo,,,alipata michubuko tu,,,,,
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  wangekufa ili tuagize wengine toka iran
   
Loading...