Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,949
- 4,444
Gari la hospitali ya wilaya ya Njombe likiwa katika foleni
kunyonya mafuta sheri.
Katika hali isiyo ya kawaida huku kila kukicha tukilalamika maisha ya Watazania yanateketea kwa kukosa huduma za afya kama Ambulance,madawa,madaktari n.k Lakini wenzetu wilaya ya Njombe wanatumia Ambulance kusafilisha wasimamizi wa mitihani wa darasa la saba.
Swali la kujiuliza hivi Halmashauri imekosa kweli pesa za kukodi usafiri mwingine kama kweli hawana magari ya kutosha katika Halmashauri?
Inatia uchungu kweli sasa itokee kuna mgonjwa hapo anahitajika kupelekwa haraka kuokoa maisha yake hospitalini hapo maanake ndo basi tena mauti yatamkuta.
Hivi jamani hawa watendaji bomu tutawakumbatia mpaka lini?
Tunaendelea mpaka lini kuwapigia makofi huku hawajui wajibu wao katika kazi?