Gari la Serikali lanaswa likisafirisha Bangi, dereva asimamishwa kazi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,441
Gari la Halmashauri ya Arusha linashikiliwa na Polisi Mkoani Kilimanjaro baada ya kukutwa likisafirisha shehena ya bangi kinyume cha sheria za Nchi.

Dereva wa gari hilo, Athuman Magio, anashikiliwa na polisi mkoani humo na tayari amesimamishwa kazi kwa kufanya biashara haramu.

Chanzo: Ngilisho TV

====================

Tukio hilo lilitokea Mei 10, 2022, jana Mei 11 kikafanyika kikao cha Baraza la Madiwani ambapo madiwani walimbana Mkurugenzi ambaye ndiye aliyetoa taarifa ya kuwa dereva amesimamishwa kazi na yupo kwenye mikono ya Jeshi la Polisi Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom