Gari la RC wa Shinyanga lagonga na kuua mmoja wilayani Kahama

Mkazi wa Kahama aliyejulikana kwa jina la Deogratius Landani (47) amefariki dunia baada ya kugongwa na gari mojawapo miongoni mwa magari yaliyokuwa katika msafara wa Rais John Pombe Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea Jumamosi Machi 10,2018 majira ya saa 7:00 mchana katika mtaa wa Shunu kwenye njia kuu ya kutoka Masumbwe kueleke Kahama wakati magari yakiwa kwenye msafara wa rais Magufuli wilayani Kahama.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Kasyombe Mwakyusa Chanzo ni mpanda baiskeli huyo Deogratius Landani kuingilia msafara kwa kuingia barabarani ghafla bila kuchukua tahadhali za kutosha.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mji Kahama kwa uchunguzi zaidi

maiti.jpg

Mwili wa Deogratius Landani (47) mkazi wa Kahama ukiwa barabarani baada ya kugongwa na gari kwenye msafara wa rais John Pombe Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga

Inna Lillah wahina lillah... lajun... tume mpoteza mpiga kura... tulitakiwa kumuacha mpiga kura apite kwanza...
 
Mkazi wa Kahama aliyejulikana kwa jina la Deogratius Landani (47) amefariki dunia baada ya kugongwa na gari mojawapo miongoni mwa magari yaliyokuwa katika msafara wa Rais John Pombe Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea Jumamosi Machi 10,2018 majira ya saa 7:00 mchana katika mtaa wa Shunu kwenye njia kuu ya kutoka Masumbwe kueleke Kahama wakati magari yakiwa kwenye msafara wa rais Magufuli wilayani Kahama.

Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga SSP Lutusyo Kasyombe Mwakyusa Chanzo ni mpanda baiskeli huyo Deogratius Landani kuingilia msafara kwa kuingia barabarani ghafla bila kuchukua tahadhali za kutosha.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mji Kahama kwa uchunguzi zaidi

View attachment 711517

Mwili wa Deogratius Landani (47) mkazi wa Kahama ukiwa barabarani baada ya kugongwa na gari kwenye msafara wa rais John Pombe Magufuli wilayani Kahama mkoani Shinyanga

Waandishi uchwara nao bhana!! Hii taarifa ililetwa jana ikisema ni gari la RC Shinyanga ndiyo lilimgonga wakati likitokea Shinyanga kwenda kumpokea Rais maeneo ya Kahama leo tena umekuwa msafara wa Rais?? Au mnafanya hivyo ili kuleta attention??
 
HOJA ni "kafa kwa kugongwa "ktk pilika pilika za ziara ya nani?
Gari ya nani/ipi ilimgonga so muhimu!

Vipi RPC ya Arusha kapona?
 
Back
Top Bottom