Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,987
- 144,318
Mkono: Nina hofu na usalama wangu
MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM) amesema maisha yake yako hatarini, kutokana na kuwepo genge la watu ambalo amedai wana nia mbaya na yeye, hivyo ameomba jeshi la Polisi kuchunguza watu hao.
Mkono, ambaye amelazimika kufungua jarida la malalamiko kwenye Kituo cha Polisi Kawe jijini Dar es Salaam, KW/RB/12156/2014, alisema tukio hilo limemwongozea hofu juu ya maisha yake, kutokana na kufuatiliwa nyendo zake na watu asiowajua.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkono alidai juzi saa 4 asubuhi akiwa na wasaidizi wake wawili wakitokea Bagamoyo, wakiwa ndani ya gari lake dogo aina ya Mercedes Benz, walipofika maeneo ya Mbezi Tangi Bovu, ghafla yalitokea magari aina ya Prado na Land Cruiser CX na kufunga njia.
Mkono alisema hali hiyo ilisababisha wasiendelee na safari yao na ndipo dereva wake alipoamua kulitoa gari na kulipitisha pembeni na kufanikiwa kutoka katika maeneo hayo.
Taarifa hiyo ya Mkono ilifafanua kuwa wakiwa bado wako njiani, yalitokea tena hayo magari mawili yakiwa mwendo wa kasi, yakiwafukuza na ndipo kijana mmoja akiwa amevaa miwani myeusi, ambaye alikuwa ndani ya gari aina ya Land Cruiser VX, alishusha kioo na kuwaamuru wasimamishe gari lao.
"Katika hali hiyo dereva wangu aliendesha gari kwa kasi hadi njia panda ambako tulimkuta askari wa doria akiwa pembezoni mwa barabara, tukamweleza na kuomba msaada wake.
Baada ya sisi kusimama mbele ya askari huyo magari hayo yalipita kwa kasi na kuelekea maeneo ya Mbezi Beach," ilisema taarifa hiyo ya Mkono.
Alisema yeye na wasaidizi wake, walipomweleza yule askari wa doria yaliyowatokea njiani, aliwashauri kuwa ni vyema wakaenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi kilicho karibu na eneo la tukio kwa msaada zaidi.
"Kutokana na tukio hilo nilipata mshituko na kuwaomba wasaidizi wangu wanipeleke nyumbani kwangu Masaki kwa mapumziko," alidai Mkono.
Alisema alipofika nyumbani ndipo alimwagiza msaidizi wake aende kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha Kawe, kama alivyoshauriwa na askari aliyekuwa doria na kufungua jalada hilo.
Hilo ni tukio la pili ndani ya siku za hivi karibuni, ambalo Mkono amejitokeza kwenye vyombo vya habari na kueleza maisha yake kuwa hatarini. Tukio la kwanza Mkono alidai kulishwa sumu wakati akiwa safari ya kikazi na wabunge wenzake nchini Uingereza.
Chanzo:Habarileo
MY TAKE:
Mh.Kafulila,mwenzako akinyolewa,wewe tia maji.