Gari la Mwananchi lapata ajali, watatu wafariki papohapo, watano wajeruhiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la Mwananchi lapata ajali, watatu wafariki papohapo, watano wajeruhiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 26, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Florah Temba, Kilimanjaro Yetu


  WATU watatu wamefariki dunia papohapo na wengine Watano kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria lenye namba za usajili T336 BFU Isuzu Pick-up linalosafirisha Magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communication (MCL) kupata ajali.


  Gari hilo ambalo lilikuwa na magazeti likitokea jijini Dar es salaam kuelekea Moshi na Arusha kwa ajili ya kusambaza magazeti, limepata ajali eneo la Kirinjiko wilayani Same mkoani Kilimanjaro baada ya kuligonga kwa nyuma Lory lenye namba za usajili T 415 AAM/ T 411AAM Scania lililokuwa limeegeshwa pembeni.


  Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana eneo la tukio gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Wambura Ramadhani (32) lilitaka kuovateki gari iliyokuwa mbele yake na baadae kuona gari nyingine iliyokuwa ikija kwa mbele ndipo aliporudi na kuligonga Lory hilo.


  Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo Oktoba 26 majira saa kumi na moja alfajiri katika eneo la Kirinjiko wilayani Same Barabara kuu ya Tanga/Moshi.


  Kamanda Boaz amewataja waliofariki kuwa ni Ibrahim Mrutu (65) Mkazi wa wilayani Same, Abdalla Rajabu (49) Mkazi wa Majengo Mkoani Arusha na Robert Mnyeki (39).


  Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Rahim Bakari (28) mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam mfanyakazi wa kampuni ya Mwananchi, Juma Said (37) Dereva wa Simba Truck mkazi wa Arusha kwa Mrombo, Gasino Nguma (40) mwalimu mkazi wa Mlandizi jijini Dar es salaam, Hamza Omary (31) mfanyabiashara mkazi wa Buguruni jijini Dar es salaam pamoja na Sekero Musa (30) ambaye hali yake inaelezewa kuwa mbaya.


  Alisema Watu hao walikuwa ni abiria katika gari lililokuwa likisafirisha magazeti ambapo Majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Same na KCMC kwa ajili ya matibabu.


  Kamanda alisema Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari dogo na kwamba dereva wa gari hilo Wambura Ramadhani anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na pindi upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.


  Blogzamikoa
  www.blogszamikoa.blogspot.com   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hizi ajali kila ck zinatumaliza jamani,Aah rest in peace marehemu wote
   
 3. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Poleni mliojeruhiwa. RIP marehem wote.
   
 4. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  poleni wafiwa
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wapumzike kwa amani hao waliofariki. Tunawatakia quick recovery hao majeruhi.
   
 6. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pole kwa majeruhi Mungu awasaidie mpone haraka.
  R.I.P marehemu wote.
   
 7. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,399
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Pole wafiwa, na poleni majeruhi. Taabu ya hao madereva wa magari yanayopeleka magazeti ni mwendo kasi. Punguzeni hiyo mi-bio yenu, mnatumaliza!
   
 8. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  AgaKhan keshaanza kutoa kafara eh?
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Pamoja na Kutoa RIP kwa marehemu na POLE kwa waliojeruhiwa, kuna mambo kadhaa tunapaswa kuyaangalia katika jitihada zetu za kujaribu kupunguza Ahali zinazokatisha uhai wa ndugu zetu:

  -Hizi pick-up za magazeti zinatoka jijini kati ya saa NNE na SABA usiku mara tu baada ya magazeti kutoka na kwa maana hiyo zinapaswa kwenda mbio ili kuhakikisha kuwa zinawahisha magazeti Alfajiri Moshi, Arusha, Mbeya na Dodoma.

  Madereva wa Pick-Up hizi ni binadamu tu. Kuna uwezekano mkubwa wa kusinzia nyakati za alfajiri wakiwa barabarani.
  Hizi ni gari kwa ajili ya kusafirishia magazeti tu kwa maana hiyo zinapaswa sana sana kuwa na dereva na msaidizi wake. kwa wale ambao wameishaziona, hata muundo wake ni kwa ajili ya kazi hiyo tu.

  Kwa mujibu wa taarifa za Kipolisi ni kwamba gari hilo lilikuwa na biria NANE ambao kati yao waTatu wamepoteza Maisha.
  Hapa tayari Dereva atakuwa lawamani kwa sababu kwa vyovyote vile atakuwa alichukua abiria SITA kwenye gari ambalo halipaswi na halifai kupakia abiria. Hakupaswa kuvunja sheria za Kampuni na za Barabara kwa kisingizio cha Kujiongezea Kipato!

  Kampuni ya Mwananchi pia inapaswa kuangalia uwezekano sasa wa kuwekeza katika tekinolojia ya kufunga mitambo kwenye miji mikubwa ya Dodoma, Mwanza, Mbeya na Arusha ambayo itakuwa na kazi ya kuchapa magazeti wakati ule ule ambapo gazeti linachapwa kwenye mtambo mkuu uliopo Dar.

  Nchi nyingi zilizoendelea zinatumia tekinolojia hii badala ya hii ya madereva kukesha barabarani wakikimbiza magazeti mikoani na matokeo yake kuwa kama haya yaliyotokea.

  Pamoja na kwamba kuna utaratibu wa Makampuni yanayochapisha magazeti kuchangia gharama za kuwahisha magazeti hayo mikoani, bado kampuni hizo zinapaswa kuangalia katika kuchangia gharama za tekinolojia hiyo.
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Naye huwa anatoa kafara?
   
 11. sindano butu

  sindano butu JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 478
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  acha chuki zako binafsi . ivi wewe unawafahamu vizuri AGA KHAN ? laiti ungekuwa unafahamu kwa kina usinge lopoka!!!
   
Loading...