Gari la Mbunge wa Kibiti lakamatwa likisafirisha magendo

Ni gari la Mbunge Ally Ungando ambaye ni Mbunge wa Kibiti kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Gari hilo lilikuwa likisafirisha shehena ya Mbao kwa njia ya magendo kutoka Kibiti kwenda Dar es Salaam

Yeye asema dereva wake ndiye mhusika kwano yeye hakuwa na taarifa za mpango huo na asingeukubali
Ni kutaifisha mbao,gari na kesi juu......kama ni kweli lakini.
 
Hamna kesi hapo labda hilo gari lingekuwa ni la mbunge wa kutoka upinzani.

Jiulize kwanza habari ya Simbachaweni kupiga mtu na kuripotiwa Polisi imeishia wapi?
 
Gari la mbunge wa Kibiti, Ally Ungando - CCM limekamatwa likisafirisha mbao kwa njia ya magendo kutoka Kibiti kwenda Dar es Salaam huku likiwa linapeperusha bendera ya mbunge huyo, Ungando amekiri kukamatwa kwa dereva wake huku akisema yeye hahusiki na mpango huo #KwanzaHabari

Sasa hapo ' Logically ' tu Kichwa cha Habari kilitakiwa kiwe Dereva wa Gari ya Mbunge wa CCM akamatwa akisafirisha Magendo? au Gari ya Mbunge wa CCM yakamatwa ikisafirisha Magendo? Halafu tukisema ' Media ' ya Tanzania kwa sasa ipo ' ICU ' kuna Watu huwa hawatuelewi. Kichwa cha Habari cha hiyo taarifa kina nia tu moja ya Kumchafua Mheshimiwa Mbunge wa CCM ( imekaa Kisiasa zaidi ) ila hakikuandikwa Kiuhalisia na ' Professionally ' kabisa. Kazi ipo hakyanani!
 
Hamna kesi hapo labda angekuwa wa kutoka upinzani.

Jiulize kwanza habari ya Simbachaweni kupiga mtu na kuripotiwa Polisi imeishia wapi?
Kesi ipo mkuu. Uhalifu ni uhalifu tu haijalishi nani ameufanya. Sheria ichukuwe mkondo wake
 
Gari la mbunge wa Kibiti, Ally Ungando - CCM limekamatwa likisafirisha mbao kwa njia ya magendo kutoka Kibiti kwenda Dar es Salaam huku likiwa linapeperusha bendera ya mbunge huyo, Ungando amekiri kukamatwa kwa dereva wake huku akisema yeye hahusiki na mpango huo #KwanzaHabari
"Mbunge wa CCM akamatwa" = UONGO

aliekamatwa ni dereva ila Lori ndo la Mbunge

"Akipeperusha Bendera ya Mbunge " = UONGO ukweli wake lilikuwa Lori wala sio gari ya Mbunge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: e2n
Sasa hapo ' Logically ' tu Kichwa cha Habari kilitakiwa kiwe Dereva wa Gari ya Mbunge wa CCM akamatwa akisafirisha Magendo? au Gari ya Mbunge wa CCM yakamatwa ikisafirisha Magendo? Halafu tukisema ' Media ' ya Tanzania kwa sasa ipo ' ICU ' kuna Watu huwa hawatuelewi. Kichwa cha Habari cha hiyo taarifa kina nia tu moja ya Kumchafua Mheshimiwa Mbunge wa CCM ( imekaa Kisiasa zaidi ) ila hakikuandikwa Kiuhalisia na ' Professionally ' kabisa. Kazi ipo hakyanani!
Waandishi sasa hivi wanauza headings,heading iweze kuteka hisia za watu,mtu ashawishike kununua gazeti au kufungua link yenye heading ambayo ni ambigous,hii imekaa kibiashara zaidi na sio proffessionalism,kimsingi upo sahihi,ila uhalisia now uko hivi nilivyoeleza..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atapelekwa mahakamani,, then anaachiwa kwa kauli kwamba DPP hana nia kuendelea na kesi,, mshtakiwa apewe mali yake,,, ukiwa chama kile raha bwana
 
Ni gari la Mbunge Ally Ungando ambaye ni Mbunge wa Kibiti kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Gari hilo lilikuwa likisafirisha shehena ya Mbao kwa njia ya magendo kutoka Kibiti kwenda Dar es Salaam

Yeye asema dereva wake ndiye mhusika kwano yeye hakuwa na taarifa za mpango huo na asingeukubali
Umenikumbusha meli iliyokamatwa na meno ya tembo ya aliyekuwa katibu mkuu wa CCM
 
Sasa hapo ' Logically ' tu Kichwa cha Habari kilitakiwa kiwe Dereva wa Gari ya Mbunge wa CCM akamatwa akisafirisha Magendo? au Gari ya Mbunge wa CCM yakamatwa ikisafirisha Magendo? Halafu tukisema ' Media ' ya Tanzania kwa sasa ipo ' ICU ' kuna Watu huwa hawatuelewi. Kichwa cha Habari cha hiyo taarifa kina nia tu moja ya Kumchafua Mheshimiwa Mbunge wa CCM ( imekaa Kisiasa zaidi ) ila hakikuandikwa Kiuhalisia na ' Professionally ' kabisa. Kazi ipo hakyanani!
Kwani weredi ni uongo.... Sasa ulitaka kwa weredi angeandika Punda wa Mbunge au aandike pikipiki ya diwani???/ hapa tunataka habari ifike kama ilivyo.. Acha upuuzi huo wa professionalism bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani weredi ni uongo.... Sasa ulitaka kwa weredi angeandika Punda wa Mbunge au aandike pikipiki ya diwani???/ hapa tunataka habari ifike kama ilivyo.. Acha upuuzi huo wa professionalism bhana

Sent using Jamii Forums mobile app

Katika Kiswahili sanifu hatuna neno ' Weredi ' kama ulivyoandika hapo juu bali tuna neno sahihi la ' Weledi ' sawa?
 
Nimekumbuka kesi ya akina Kangi Lugola kipindi kile ya kuomba rushwa kwa DED wa Mkurugana Spora Liana!!!
 
Watapata tabu sana mwaka huu, wale waliozowea kuishi kimazowea! Nasema Watapata tabu sana safari hii.....

Back
Top Bottom